bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 15
Leviticus 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 16 →
1
Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
2
Semeni na wana wa Isiraeli na kuwaambia: Mtu mume ye yote akiwa mwenye kisonono mwilini mwake ni mwenye uchafu kwa ajili ya hicho kisonono chake.
3
Nao uchafu, anaoupata kwa kisonono chake, ni wa namna hii: kama mwili wake unachuruzika usaha wa kisonono chake, au kama mwili wake unaukomeshakomesha, uchafu ni uo huo.
4
Kilalo cho chote, mwenye kisonono atakachokilalia, ni chenye uchafu.
5
Naye mtu atakayekigusa kilalo chake sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
6
Naye atakayekalia kitu, mwenye kisonono alichokikalia, sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
7
Naye atakayeugusa mwili wake mwenye kisonono sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
8
Naye mwenye kisonono akitemea mate mwenye kutakata, huyo sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
9
Nayo matandiko yo yote, mwenye kisonono atakayoyakalia akipanda, yatakuwa yenye uchafu.
10
Naye kila atakayegusa cho chote kilichokuwa chini yake atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni, naye atakayevichukua vilivyo hivyo sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
11
Naye kila mtu, mwenye kisonono atakayemgusa pasipo kunawa kwanza mikono yake kwa maji, sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
12
Nacho chombo cha udongo, mwenye kisonono atakachokigusa, sharti kivunjwe, nacho kila chombo cha mti sharti kioshwe majini.
13
Lakini mwenye kisonono akipata kutakata, kwa kuwa kisonono chake kimekoma, sharti ahesabu siku saba kuanzia hapo, alipopata kutakata, kisha sharti azifue nguo zake pamoja na koga katika maji ya mtoni; ndipo, atakapokuwa mwenye kutakata.
14
Siku ya nane na achukue hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga, amtokee Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, ndipo ampe mtambikaji wale ndege.
15
Naye mtambikaji na awatengeneze, mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi mbele ya Bwana kwa ajili ya kisonono chake.
16
Lakini mtu akitokwa na mbegu akilala sharti auogeshe mwili wake wote mzima majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
17
Nazo nguo zote na ngozi zote zilizonyewa na hizo mbegu sharti zifuliwe majini, nazo zitakuwa zenye uchafu mpaka jioni.
18
Tena mtu aliye hivyo akilala na mwanamke, sharti wote wawili na waoge majini, kisha watakuwa wenye uchafu mpaka jioni.
19
Mwanamke akiingia miezini, atokwe na damu mwilini mwake, sharti atengwe siku saba, naye kila atakayemgusa atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
20
Nayo yote, atakayoyalalia siku hizo za kutengwa kwake, yatakuwa yenye uchafu; nayo yote, atakayoyakalia, yatakuwa yenye uchafu.
21
Naye kila atakayekigusa kilalo chake sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
22
Naye kila atakayegusa cho chote, alichokikalia, sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
23
Naye atakayegusa cho chote kilichoko juu ya kilalo chake au juu ya kitu, alichokikalia, atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
24
Tena mtu akilala naye, akiwa miezini, atakuwa mwenye uchafu siku saba, hata kilalo chake, atakachokilalia, kitakuwa chenye uchafu.
25
Mwanamke akitoka damu zake siku nyingi zisizo zake za kuwa miezini, au kama anatoka damu kuzipita hizo siku za kuwa miezini, basi siku zote za kutoka damu ni mwenye uchafu; kama alivyo akiwa miezini, ndivyo, mwenye uchafu alivyo siku hizo nazo.
26
Kilalo cho chote, atakachokilalia siku zote za kutoka damu zake, ni chenye uchafu, kama kilalo chake cha kuwa miezini kilivyo chenye uchafu; nacho kitu cho chote, atakachokikalia, ni chenye uchafu, kama kilivyo chenye uchafu siku zake za kuwa miezini.
27
Naye kila atakayevigusa atakuwa mwenye uchafu, sharti azifue nguo zake pamoja na koga majini, kisha atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
28
Lakini akipata kutakata, kwa kuwa damu yake imekoma, sharti ahesabu siku saba, halafu atakuwa ametakata.
29
Siku ya nane na achukue hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga, awapeleke kwa mtambikaji penye kuliingilia Hema la Mkutano.
30
Naye mtambikaji na atengeneze mmoja kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi mbele ya Bwana kwa ajili ya uchafu wake, damu zake ziliomtia.
31
Hivi ndivyo, mtakavyowatengesha wana wa Isiraeli na uchafu wao, wasife kwa ajili ya uchafu wao wakilichafua Kao langu lililoko katikati yao.
32
Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya mwenye kisonono nayo yake anayejipatia uchafu kwa kutokwa na mbegu akilala;
33
tena ya mwanamke akiingia miezini, nayo ya kila mwenye kisonono, kama ni mtu mume, au kama ni mtu mke, nayo ya mtu anayelala na mwanamke aliye mwenye uchafu.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27