bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Leviticus 14
Leviticus 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 15 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Haya ndiyo maonyo yampasayo mtu mwenye ukoma siku ya kueuliwa kwake: sharti apelekwe kwa mtambikaji.
3
Naye mtambikaji na amtokee nje ya makambi; mtambikaji akimtazama na kuona, ya kama huyu mwenye ukoma amepona ugonjwa mbaya wa ukoma,
4
mtambikaji na aagize, wamletee huyo mwenye kueuliwa ndege wawili walio wazima walio wenye kutakata, tena kipande cha mwangati na nyuzi nyekundu na kivumbasi.
5
Kisha mtambikaji na aagize, ndege mmoja achinjwe juu ya mtungi wenye maji ya mtoni.
6
Naye ndege wa pili aliye mzima na amshike pamoja na kile kipande cha mwangati na zile nyuzi nyekundu na kile kivumbasi, avichovye vyote pamoja na ndege aliye mzima katika damu ya ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni.
7
Kisha amnyunyizie mara saba yule mwenye kueuliwa aliyepona ukoma. Akiisha kumweua hivyo na amwachilie huyo ndege aliye mzima, ajiendee maporini.
8
Kisha mwenye kueuliwa na azifue nguo zake, tena na azinyoe nywele zake zote, hata koga na aoge majini. Ndipo, atakapokuwa ametakata. Baadaye ataweza kuingia makambini na kukaa siku saba nje penye hema lake.
9
Siku ya saba na azinyoe nywele zake zote za kichwani pake na ndevu zake na nyushi za macho yake, nywele zake zote pia na azinyoe, nazo nguo zake na azifue, nao mwili wake auogeshe majini; ndipo, atakapokuwa ametakata.
10
Siku ya nane na achukue wana kondoo wawili wasio na kilema na kondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na kilema na vibaba kumi vya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko na nusu kibaba ya mafuta.
11
Kisha mtambikaji anayeeua na amsimamishe mwenye kueuliwa pamoja na hivyo vitu vyake mbele ya Bwana penye kuliingilia Hema la Mkutano.
12
Kisha mtambikaji na achukue mwana kondoo mmoja, amtoe kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi pamoja na ile nusu kibaba ya mafuta, ampitishe motoni mbele ya Bwana kuwa kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
13
Kisha na amchinje huyu mwana kondoo hapo mahali patakatifu, wanapochinja ng'ombe za tambiko za weuo nazo za kuteketezwa nzima. Kwani ng'ombe ya tambiko ya upozi ni yake mtambikaji kama ile ya weuo, ni takatifu yenyewe.
14
Kisha mtambikaji na achukue damu kidogo ya ng'ombe ya tambiko ya upozi, yeye mtambikaji ampake mwenye kueuliwa pembe ya chini ya sikio lake la kuume na dole gumba la mkono wake wa kuume nalo dole gumba la mguu wake wa kuume.
15
Kisha mtambikaji na achukue mafuta kidogo ya ile nusu kibaba, ayamimine katika gao lake mtambikaji la mkono wake wa kushoto.
16
Kisha mtambikaji na akichovye kidole chake cha kuume katika mafuta yaliyomo katika gao lake la kushoto, ayanyunyize mara saba mafuta hayo kwa kidole chake mbele ya Bwana.
17
Nayo mafuta yatakayosalia gaoni mwake mtambikaji mengine na ayatumie kumpaka mwenye kueuliwa pembe ya chini ya sikio lake la kuume na dole gumba la mkono wake wa kuume nalo dole gumba la mguu wake wa kuume juu ya damu ya ng'ombe ya tambiko ya upozi.
18
Nayo mafuta mengine yatakayosalia gaoni mwake mtambikaji na ampake mwenye kueuliwa kichwani; ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi mbele ya Bwana.
19
Kisha mtambikaji na aitengeneze ng'ombe ya tambiko ya weuo, ampatie huyo mwenye kueuliwa upozi, uchafu wake umtoke. Baadaye na aichinje ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima.
20
Kisha mtambikaji na aitoe hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na vilaji vya tambiko mezani pa kutambikia. Mtambikaji atakapokwisha kumpatia upozi hivyo, yule atakuwa ametakata.
21
Lakini akiwa mkiwa, mkono wake usiyafikilie haya, basi, na achukue mwana kondoo mmoja tu kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi ya kupitishwa motoni, ajipatie upozi, na vibaba vitatu tu vya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko na nusu kibaba ya mafuta,
22
tena hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga, kama mkono wake unavyoweza kufikilia, mmoja awe ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili awe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima.
23
Siku ya nane akiisha kuambiwa, ya kama ni mwenye kutakata, awapeleke kwa mtambikaji hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, mbele ya Bwana.
24
Naye mtambikaji na amchukue mwana kondoo aliye ng'ombe ya tambiko ya upozi pamoja na ile nusu kibaba ya mafuta, yeye mtambikaji ampitishe motoni mbele ya Bwana kuwa kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.
25
Kisha na amchinje huyu mwana kondoo aliye ng'ombe ya tambiko ya upozi, kisha mtambikaji na achukue damu kidogo ya hiyo ng'ombe ya tambiko ya upozi, ampake mwenye kueuliwa pembe ya chini ya sikio lake la kuume na dole gumba la mkono wake wa kuume nalo dole gumba la mguu wake wa kuume.
26
Kisha mtambikaji na amimine mafuta kidogo katika gao lake mtambikaji la mkono wake wa kushoto.
27
Kisha mtambikaji na anyunyize kwa kidole chake cha kuume mara saba mbele ya Bwana mafuta yaliyomo katika gao lake.
28
Kisha mtambikaji hayo mafuta yaliyomo katika gao lake mengine na ayatumie kumpaka mwenye kueuliwa pembe ya chini ya sikio lake la kuume, nalo dole gumba la mkono wake wa kuume, nalo dole gumba la mguu wake wa kuume hapo penye damu ya ng'ombe ya tambiko ya upozi.
29
Nayo mafuta mengine yatakayosalia gaoni mwake mtambikaji na ampake mwenye kueuliwa kichwani, ampatie upozi mbele ya Bwana.
30
Kisha mtambikaji na atengeneze hua mmoja au kinda moja la njiwa manga, mkono wake yule ulioweza kuwatoa.
31
Hawa, mkono wake yule ulioweza kuwatoa, mmoja awe ng'ombe ya tambiko ya weuo, wa pili awe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima pamoja na vilaji vya tambiko; hivyo ndivyo, mtambikaji atakavyompatia mwenye kueuliwa upozi mbele ya Bwana.
32
Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya mtu aliyepatwa na ugonjwa huo mbaya wa ukoma, ambaye mkono wake hauwezi kuyatoa yaupasayo weuo wake.
33
Bwana akamwambia Mose na Haroni kwamba:
34
Mtakapoiingia nchi ya Kanaani, nitakayowapa kuwa yenu, itakuwa, nipige nyumba ya hiyo nchi, ikiisha kuwa yenu, hiyo nyumba ipatwe na ukoma;
35
ndipo mwenye nyumba na afike kwa mtambikaji kumpasha habari kwamba: Nyumbani mwangu mna kitu kinachoonekana kuwa kama ugonjwa mbaya.
36
Naye mtambikaji na aagize, watoe humo nyumbani yaliyomo, yeye mtambikaji akiwa hajafika bado kuutazama huo ugonjwa mbaya, kusudi yote yaliyomo humo nyumbani yasipate kuwa yenye uchafu. Baadaye mtambikaji na aingie kuitazama hiyo nyumba.
37
Akipatazama hapo palipopatwa na ugonjwa huo mbaya na kuona, ya kama ugonjwa huo mbaya umezipata kuta za hiyo nyumba na kutia vishimoshimo vyenye madoadoa ya kimajanijani au ya damudamu, navyo vikionekana kuwa vinabonyea ukutani,
38
mtambikaji na atoke humo nyumbani na kupitia hapo pa kuiingilia nyumba hiyo, kisha hiyo nyumba na aifunge siku saba.
39
Mtambikaji atakaporudi siku ya saba, akiitazama na kuona, ya kama huo ugonjwa mbaya umeendelea katika kuta za nyumba hiyo,
40
mtambikaji na aagize, wayatoe hayo mawe yaliyopatwa na huo ugonjwa mbaya, wayatupie mahali penye uchafu nje ya mji.
41
Kisha hiyo nyumba na waikwangue po pote upande wa ndani, nazo takataka, watakazokwangua, na wazimwage mahali penye uchafu nje ya mji.
42
Kisha na wachukue mawe mengine, wayatie hapo, yale mawe yalipokuwa, kisha wachukue udongo mwingine wa kuipaka hiyo nyumba.
43
Ugonjwa huo mbaya utakaporudi na kutokea tena humo nyumbani, wakiisha kuyatoa mawe yote na kuikwangua hiyo nyumba na kuipaka tena,
44
mtambikaji sharti aje tena; akiitazama na kuona, ya kama ugonjwa huo mbaya umeendelea humo nyumbani, basi, ndio ukoma unaokula humo nyumbani, kwa hiyo nyumba ni yenye uchafu.
45
Kwa sababu hii hawana budi kuibomoa hiyo nyumba, nayo mawe yake na miti yake na takataka zote za hiyo nyumba sharti wazipeleke nje ya mji na kuzitupia mahali penye uchafu.
46
Naye atakayeingia humo nyumbani, siku zote ikiwa imefungwa, atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni.
47
Naye atakayelala humo nyumbani sharti azifue nguo zake, naye atakayekula humo nyumbani sharti azifue nguo zake.
48
Lakini mtambikaji akiingia humo na kutazama, basi, akiona, ya kama huo ugonjwa mbaya haukuendelea humo nyumbani, walipokwisha kuipaka tena, mtambikaji hana budi kusema, ya kama hiyo nyumba imekwisha kutakata, kwa kuwa ugonjwa huo mbaya umepona.
49
Kisha na achukue ndege wawili na kipande cha mwangati na nyuzi nyekundu na kivumbasi.
50
Ndege mmoja na amchinje juu ya mtungi wenye maji ya mtoni.
51
Kisha na akichukue kile kipande cha mwangati na kile kivumbasi na hizo nyuzi nyekundu pamoja na yule ndege aliye mzima, vyote pamoja avichovye katika damu ya ndege aliyechinjwa, hata katika yale maji ya mtoni, kisha ainyunyizie hiyo nyumba mara saba.
52
Ndivyo, atakavyoieua hiyo nyumba kwa damu ya ndege na kwa maji ya mtoni na kwa ndege aliye mzima na k kipande cha mwangati na kwa kivumbasi na kwa nyuzi nyekundu.
53
Kisha na amwachilie yule ndege aliye mzima, ajiendee nje ya mji maporini. Ndivyo, atakavyoipatia hiyo nyumba upozi, ipate kuwa yenye kutakata.
54
Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya kila namna ya ugonjwa huo mbaya wa ukoma na wa upele mbaya,
55
hata wa ukoma wa nguo na wa nyumba na wa kivimbe na wa kipele na wa balanga, watu wapate kufundishwa siku za kuwa wenye uchafu nazo siku za kuwa wenye kutakata. Haya ndiyo maonyo ya kufundisha mambo ya ukoma.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27