bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
/
Job 38
Job 38
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 39 →
1
Halafu Yawe akamujibu Yobu kutoka katika zoruba:
2
Nani wewe unayevuruga mipango yangu kwa maneno yasiyokuwa na akili?
3
Ujikaze kama mwanaume, nami nitakuuliza nawe utanijibu.
4
Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Uniambie, kama una maarifa.
5
Ni nani aliyeweka vipimo vyake, unajua bila shaka! Au nani aliyenyoosha kamba juu yake kwa kuipima?
6
Nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini, au nani aliyeliweka jiwe lake la musingi,
7
nyota za asubui zilipokuwa zikiimba pamoja, na wana wa Mungu wakapiga vigelegele vya shangwe?
8
Ni nani aliyefunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka katika vilindi?
9
Ni nani aliyefunika bahari kwa mawingu na kuiviringishia giza kubwa,
10
aliyeiwekea bahari mipaka na kuizuia kwa vifungio na milango
11
na kuiambia: “Mwisho wako ni hapa, si zaidi! Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!”
12
Yobu, tangu uzaliwe umekwisha kuamuru kupambazuke na kufanya mapambazuko yajue pahali pake,
13
kusudi yapate kukamata dunia kwa pembe zake na kuwatikisa watenda mabaya?
14
Dunia inageuka na kupata rangi kama nguo; kama udongo wa mufinyanzi unavyogeuzwa na muhuri.
15
Lakini waovu watanyimwa mwangaza wao, mukono wanaonyoosha kwa kupiga watu utavunjwa.
16
Umepata kufika kwenye chemichemi za bahari au kutembea juu ya sakafu ya kilindi cha bahari?
17
Umekwisha kuonyeshwa milango ya kifo au kuona milango ya makao ya giza kubwa?
18
Unajua ukubwa wa dunia? Uniambie kama unajua haya yote.
19
Makao ya mwangaza yako wapi? Kwenye nyumba ya giza ni wapi,
20
kusudi upate kupeleka kwenye makao yake, na kuifahamu njia ya kwenda kule kwake.
21
Wewe unapaswa kujua, wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi!
22
Umekwisha kuingia katika akiba za teluji, au kuona akiba za mvua ya mawe
23
ambavyo nimeviweka kwa ajili ya wakati wa fujo, kwa ajili ya siku ya mapigano na vita?
24
Unajua mwangaza unagawanywa kwa njia gani, au namna gani upepo wa mashariki unavyosambazwa katika dunia?
25
Nani aliyechora katika anga njia kwa ajili ya mvua? Nani aliyeonyesha radi njia yake katika mawingu,
26
nayo ikasababisha mvua kunyesha katika inchi kusikoishi mutu na katika jangwa ambako hakuna mutu,
27
kusudi ikunyweshe inchi kavu na yenye kukauka na kuifanya ioteshe majani?
28
Mvua ina baba? Au nani amezaa matone ya umande?
29
Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Nani aliyezaa teluji?
30
Maji yanageuka kuwa magumu kama jiwe, na uso wa bahari unaganda.
31
Angalia makundi ya nyota: Unaweza kuifunga minyororo Kilimia, au kuviregeza vifungo vya Orioni?
32
Unaweza kuongoza nyota kwa wakati wake, au kumwongoza Dubu pamoja na vitoto vyake?
33
Unayajua maagizo ya mbingu? Unaweza kuzipangia utaratibu wao katika dunia?
34
Unaweza kupiga vigelegele na kuyaamuru mawingu yakufunike kwa mutiririko wa mvua?
35
Wewe ukiamuru umeme uangaze, utakufikia na kusema: “Nipo hapa”?
36
Ni nani aliyemujulisha kwarara kujaa kwa muto Nili au aliyemwambia jogoo kwamba mvua inakuja?
37
Nani mwenye akili ya kuweza kuhesabu mawingu au kuinamisha vibuyu vya maji kule katika mbingu
38
kusudi mavumbi katika dunia yagandamane na udongo ushikamane na kuwa matope?
39
Unaweza kumwindia simba dike au kuishibisha hamu ya simba wakali
40
wanapojificha ndani ya matundu yao, au kulala katika maficho wakivizia?
41
Ni nani anayewapa vibombobombo chakula chao, vitoto vyao vinaponililia mimi Mungu, na kurukaruka huku na kule kwa njaa?
← Chapter 37
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 39 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42