bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 1
1 Samuel 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 2 →
1
Kulikuwa na mtu mmoja wa Ramataimu-Sofimu ulioko milimani kwa Efuraimu, jina lake ni Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, mtu wa Efuraimu.
2
Naye alikuwa na wanawake wawili, mmoja jina lake Hana, wa pili jina lake Penina; huyu Penina alikuwa ana watoto, naye Hana alikuwa hana watoto.
3
Yule mtu alitoka mwaka kwa mwaka mjini kwake akipanda kwenda Silo kumtambikia Bwana Mwenye vikosi na kumtolea ng'ombe ya tambiko. Huko wana wawili wa Eli, Hofuni na Pinehasi, walikuwa watambikaji wa Bwana.
4
Kila siku, Elkana alipotoa ng'ombe ya tambiko, akampa mkewe Penina na wanawe wa kiume na wa kike vipande vya nyama.
5
Naye Hana akampa kipande kimoja mara mbili, kwani alimpenda Hana, lakini Bwana alikuwa amelifunga tumbo lake.
6
Naye mchukivu wake akamsikitisha sana kwa kumchokoza, kwa kuwa Bwana alilifunga tumbo lake.
7
Ndivyo, alivyofanya mwaka kwa mwaka: kila alipopanda kuingia Nyumbani mwa Bwana, yule alimsikitisha, hata akalia machozi na kukataa kula.
8
Ndipo, Elkana alipomwuliza mkewe Hana: Mbona unalia? Mbona huli nyama? Mbona moyo wako unakuwa mbaya hivyo? Kumbe mimi si mwenzio mwema kuliko wana kumi?
9
Walipokwisha kula na kunywa huko Silo, Hana akaondoka; naye mtambikaji Eli alikwa amekaa katika kiti chake penye mhimili wa mlango wa Jumba la Bwana.
10
Roho yake Hana ilikuwa yenye uchungu, akamlalamikia Bwana na kulia machozi mengi;
11
akaaga kiagio na kusema: Bwana Mwenye vikosi, kama utautazama ukiwa wa kijakazi wako, ukinikumbuka, usimsahau kijakazi wako ukimpa kijakazi wako mwana wa kiume, nitamtoa, awe wako, Bwana, siku zote za maisha yake, nacho kinyoleo hakitafika kichwani pake.
12
Ikawa, alipozidi kumlalamikia Bwana, Eli alikuwa anakiangalia kinywa chake.
13
Lakini Hana alikuwa anasema humo ndani moyoni mwake, midomo yake ikachezacheza tu, lakini sauti yake haikusikilika; ndipo, Eli alipomwazia kuwa amelewa.
14
Eli akamwambia: Utalewa mpaka lini? Acha, mvinyo, uliyoinywa, ikuondokee!
15
Hana akajibu na kumwambia: Sivyo, bwana, mimi ni mwanamke mwenye roho nzito, mvinyo au kileo cho chote sikunywa, nitammwagia Bwana roho yangu tu.
16
Usimwazie kijakazi wako kuwa mwanamke asiyefaa! Kwani hata sasa nimesema kwa wasiwasi na kwa uchungu wangu mwingi.
17
Eli akajibu na kumwambia: Nenda na kutengemana! Mungu wa Isiraeli na akupe maombo yako, uliyomwomba.
18
Akasema: Kijakazi wako na ayaone macho yako, yakimtazama kwa upole. Kisha huyo mwanamke akaenda zake, hata kula akala, nao uso wake haukuwa tena kama hapo kwanza.
19
Kesho yake wakaamka na mapema, wakaja kumwangukia Bwana, kisha wakarudi kwenda nyumbani kwao huko Rama. Elkana alipomtambua mkewe Hana, Bwana naye akamkumbuka.
20
Ikawa, siku zilipotimia, Hana akapata mimba, akazaa mtoto mwanamume, akamwita jina lake Samweli (Nimesikiwa na Mungu) kwa kwamba: Nimemwomba kwa Bwana.
21
Kisha yule Elkana alipopanda pamoja nao wote walio wa mlango wake kumtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya zile siku, walizomwagia,
22
Hana hakupanda nao, kwani alimwambia mumewe: Sharti huyu mwana kwanza aliache ziwa Kisha nitampeleka, amtokee Bwana usoni pake, akae hapo siku zote.
23
Mumewe Elkana akamwambia: Yafanye yaliyo mema machoni pako! Kaa, mpaka umzoeze kuacha kunyonya! Naye Bwana na alitimize neno lako. Ndipo, mama ya mtoto alipokaa na kumnyonyesha mwanawe, mpaka akimzoeza kuacha kunyonya.
24
Kisha akapanda naye, alipokwisha kumzoeza kuacha kunyonya, akachukua hata ng'ombe watatu na kapu moja la unga na kiriba cha mvinyo, akampeleka Silo Nyumbani mwa Bwana, yule mtoto akingali mdogo.
25
Wakachinja ng'ombe, kisha wakampeleka yule mtoto kwa Eli.
26
Hana akamwambia: Bwana, hivyo roho yako, bwana wangu, ilivyo nzima bado, mimi ni mwanamke yule aliyesimama humu Nyumbani pamoja na wewe kumlalamikia Bwana.
27
Nalimlalamikia kwa ajili ya mtoto huyu, Bwana akanipa maombo yangu, niliyomwomba.
28
Mimi nami ninamtoa na kumpa Bwana, awe wake siku zote, atakazokuwapo, kwani ameombwa kwake Bwana. Kisha wakamtambikia Bwana huko.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31