bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 8
1 Samuel 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 9 →
1
Ikawa, Samweli alipokuwa mzee, akawaweka wanawe wawili kuwa waamuzi wa Waisiraeli.
2
Jina la mwanawe wa kwanza ni Yoeli, nalo lake wa pili ni Abia, nao walikaa Beri-Seba, walipokuwa waamuzi.
3
Lakini wanawe hawakuendelea na kuzishika njia zake, maana waligeukia kutafuta mali, kwa hiyo wakachukua fedha za kupenyezewa, wakayapotoa mashauri.
4
Ndipo, wazee wote wa Waisiraeli walipokusanyika, wakaja Rama kwa Samweli,
5
wakamwambia: Tazama! Wewe umekwisha kuwa mzee, nao wanao hawaendelei na kuzishika njia zako, sasa tuwekee mfalme wa kutuamulia, kama mataifa yote yanavyoamuliwa!
6
Neno hili likawa baya machoni pake Samweli, kwa kuwa wamesema: Tupe mfalme wa kutuamulia! Kwa hiyo Samweli akamwomba Bwana.
7
Bwana akamwambia Samweli: Viitikie vinywa vyao watu hawa ukiyafanya yote, waliyokuambia! Kwani hawakukatai wewe, ila ni mimi, waliyenikataa kuwa mfalme wao.
8
Ndivyo, matendo yao yote yalivyo, waliyoyatenda tangu siku ile, nilipowatoa Misri, mpaka siku hii ya leo wakiniacha na kutumikia miungu mingine. Hivi ndivyo, wanavyokufanyia hata wewe.
9
Sasa viitikie vinywa vyao! Lakini sharti uwashuhudie vema na kuieleza haki yake mfalme atakayewatawala.
10
Kisha Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme haya maneno yote ya Bwana
11
akisema: Hii ndiyo haki yake mfalme atakayewatawala: atawachukua wana wenu wa kiume, awaweke katika magari yake wa kuyaendesha, wengine atawapandisha farasi, wengine atawaweka kuyatangulia magari yake kwa kupiga mbio.
12
Wengine atawaweka kuwa wakuu wa maelfu na wakuu wa hamsini tu; wengine atawaweka kuyalima mashamba yake na kuyavuna mavuno yake na kuyatengeneza mata ya vita vyake na vyombo vya magari yake.
13
Nao wana wenu wa kike atawachukua, wawe watengeneza manukato na wapishi na waoka mikate.
14
Nayo mashamba na mizabibu na michekele yenu iliyo mizuri zaidi ataichukua na kuwapa watumishi wake.
15
Tena mbegu zenu na mizabibu yenu atatoza mafungu ya kumi, awape watumishi wake wa nyumbani na watumishi wake wengine.
16
Nao watumishi wenu wa kiume na wa kike na vijana wenu walio wazuri zaidi na punda wenu atachukua, awatumie katika kazi zake.
17
Mbuzi na kondoo wenu atatoza mafungu ya kumi, nanyi sharti mmtumikie kitumwa.
18
Tena siku hiyo, mtakapolia kwa ajili ya mfalme wenu, mliyejichagulia, siku hiyo Bwana hatawajibu.
19
Lakini watu wakakataa kukiitikia kinywa cha Samweli, wakasema: Haidhuru, sharti tuwe na mfalme wa kututawala!
20
Nasi tunataka kuwa kama mataifa yote, mfalme wetu atukatie mashauri yetu, tena atutangulie, avipige vita vyetu.
21
Samweli alipokwisha kuyasikia maneno yote ya watu, akaja kuyasema masikioni mwa Bwana.
22
Bwana akamwambia Samweli: Viitikie vinywa vyao na kuwapatia mfalme! Ndipo, Samweli alipowaambia waume wa Waisiraeli: Nendeni zenu kila mtu mjini kwake!
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31