bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 29
1 Samuel 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 30 →
1
Wafilisti wakavikusanya vikosi vyao vyote Afeki, nao Waisiraeli wakapiga makambi yao kwenye chemchemi iliyoko Izireeli.
2
Wao wakuu wa Wafilisti wakafika hapo kuyapanga mamia na maelfu yao; naye Dawidi akafika na watu wake kuwapanga nyuma ya Akisi.
3
Lakini wakuu wa Wafilisti wakasema: Hawa Waebureo ni wa nini? Akisi akawaambia wakuu wa Wafilisti: Huyu siye Dawidi, mtumishi wa Sauli, mfalme wa Waisiraeli? Amekuwa kwangu siku hizi nayo miaka hii, nami sikuona kwake cho chote tangu siku ile, aliponiangukia, hata siku hii ya leo.
4
Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia, nao hao wakuu wa Wafilisti wakamwambia: Mrudishe mtu huyu, akae mahali pake, ulipompatia! Asishuke pamoja nasi kupigana, asiwe mpingani wetu kwenye mapigano. Kwani liko jambo gani liwezalo kumpatia upendeleo wa bwana wake, lisipokuwa hilo la kuvitoa vichwa vya watu hawa?
5
Je? Huyu Dawidi siye, waliyemwimbia na kuitikiana katika michezo kwamba: Sauli ameua elfu lake, lakini Dawidi ameua maelfu yake kumi?
6
Ndipo, Akisi alipomwita Dawidi, akamwambia: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, wewe u mtu mnyofu! Kwa hiyo ilifaa machoni pangu, utoke pamoja nami, uingie katika vita hivi pamoja nami, kwani sikuona kwako kibaya cho chote tangu siku hiyo, ulipokuja kwangu, hata siku hii ya leo; lakini machoni pao wakuu wewe hufai.
7
Sasa rudi, ujiendee na kutengemana, usifanye kilicho kibaya machoni pao wakuu wa Wafilisti!
8
Ndipo, Dawidi alipomwambia Akisi: Nimefanya nini? Au umeona nini kwa mtumishi wako tangu siku hiyo, nilipokutokea, hata siku hii ya leo, nisije kupiga vita nao adui wa bwana wangu mfalme?
9
Akisi akamjibu na kumwambia: Ninakujua, ya kuwa wewe u mwema machoni pangu kama malaika wa Mungu; ni wao wakuu wa Wafilisti waliosema: Asipande pamoja nasi kupiga vita!
10
Sasa uamke na mapema! Nao watumishi wa bwana wako waliokuja pamoja nawe nanyi mwamke na mapema, mkipata kuona, mwende zenu!
11
Kwa hiyo yeye Dawidi na watu wake wakaamka na mapema kwenda zao, warudi katika nchi ya Wafilisti, nao Wafilisti wakapanda kwenda Izireeli.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31