bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 2
1 Samuel 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 3 →
1
Hana akaomba na kusema: Moyo wangu unashangilia kwa kuwa naye Bwana, pembe yangu imetukuka kwa nguvu za Bwana, nimeasama kinywa changu, kiwatishe wachukivu wangu, kwani ninaufurahia msaada wako.
2
Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana, kwani pasipo wewe hakuna Mungu, wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
3
Msizidi kusema makuu ya kujikuza, maneno makorofi yasitoke vinywani mwenu! Kwani Bwana ni Mungu mwenye ujuzi, kwake yeye hujaribiwa matendo ya watu.
4
Pindi za mafundi wa vita huvunjika, lakini waliokwazwa hujivika nguvu.
5
Walioshiba hufanya kazi, wapate chakula tu, lakini waliokuwa wenye njaa, njaa zao hukoma kabisa, mwanamke mgumba huzaa watoto saba, naye mwenye wana wengi hufifia.
6
Bwana huua, naye hurudisha uzimani, yeye hushusha kuzimuni, tena hupaza juu.
7
Bwana wengine huwakosesha mali, wengine huwazidishia, hunyenyekeza, tena hukuza;
8
mnyonge humwinua uvumbini, mkiwa humtoa jaani, awaketishe pamoja nao walio wakuu akiwapa kiti chenye utukufu, kiwe chao, kwani misingi ya nchi ni yake Bwana, juu yao ameuweka ulimwengu.
9
Huiangalia miguu yao wamchao, lakini wasiomcha huangamizwa penye giza, kwa kuwa hakuna mtu atakayeshinda kwa nguvu zake.
10
Watakaoshindana na Bwana watapondwa, atakapovumisha ngurumo juu yao mbinguni. Bwana atayahukumu mapeo ya nchi, naye mfalme wake atampa uwezo atakapoitukuza pembe yake yeye, aliyempaka mafuta.
11
Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake, lakini yule mtoto akawa akimtumikia Bwana machoni pake mtambikaji Eli.
12
Wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kabisa, hawakumjua Bwana,
13
wala haki za watambikaji, wala haki za watu: mtu ye yote alipotoa ng'ombe ya tambiko, nyama zilipotokota, mtumishi wa mtambikaji huja akishika mkononi uma mkubwa wenye michomo mitatu,
14
akakoroga nao chunguni au kaangoni au sufuriani au bakulini, nazo nyama zote, ule uma ulizozipandisha, mtambikaji huzichukua. Ndivyo, walivyowafanyizia Waisiraeli wote, wakija huko Silo.
15
Napo, walipokuwa hawajachoma mafuta, mtumishi wa mtambikaji huja, amwambie mwenye kutambika: Nipe nyama ya kumchomea mtambikaji! Naye hataki kwako nyama iliyopikwa, ila mbichi.
16
Yule mtu akimwambia: Leo watayachoma mafuta, kisha jichukulie, roho yako iyatakayo, humwambia: Sharti unipe sasa hivi! Kama hutaki, nitachukua kwa nguvu.
17
Kwa hiyo ukosaji wao hao vijana ukawa mkubwa sana machoni pake Bwana, kwani kwa hiyo watu wakavibeza vipaji vya tambiko, Bwana alivyotolewa.
18
Lakini mtoto Samweli akamtumikia Bwana, akawa amevikwa kisibau cha mtambikaji cha nguo ya ukonge.
19
Naye mama yake akamshonea kanzu ndogo, akampelekea mwaka kwa mwaka, alipopanda na mumewe kutoa ng'ombe ya tambiko ya mwaka.
20
Eli akambariki Elkana na mkewe akisema: Bwana na akupatie kizazi kwake mwanamke huyu cha kumlipa ombo lake, alilomwomba Bwana! Kisha wakaenda zao kufika kwao.
21
Naye Bwana akamkagua Hana, akapata mimba, akazaa watoto wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye mtoto Samweli akawako akikua machoni pake Bwana.
22
Eli akawa mkongwe kabisa; alipoyasikia yote, wanawe wanayowafanyizia Waisiraeli wote, tena ya kuwa hulala na wanawake wanaotumikia langoni penye Hema la Mkutano,
23
akawaambia: Mbona mnafanya mambo mabaya kama hayo, mimi ninayoyasikia na hawa watu wote, ya kuwa mnayafanya?
24
Msifanye hivyo wanangu! Kwani uvumi huu, ninaousikia mimi wa kuwakosesha watu wa Bwana, si mwema.
25
Mtu akimkosea mtu mwenziwe, Mungu atampatiliza, lakini akimkosea Bwana, yuko nani atakayemwombea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwani Bwana alitaka kuwaua.
26
Lakini mtoto Samweli akaendelea kukua na kuwa mwema machoni pake Bwana, napo machoni pa watu.
27
Kisha mtu wa Mungu akaja kwa Eli, akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kumbe sikujitokeza kwa mlango wa baba yako, walipoutumikia mlango wa Farao huko Misri?
28
Nikauchagua katika mashina yote ya Waisiraeli kuwa watambikaji, wapande pangu pa kutambikia na kuvukiza uvumba na kuvaa kisibau cha mtambikaji mbele yangu, nikaupa mlango wa baba yako ng'ombe zote za tambiko, wana wa Isiraeli wanazozitoa za kuteketezwa motoni.
29
Mbona mnazipiga mateke ng'ombe zangu za tambiko na vipaji vyangu vya tambiko, nilivyoagiza, wavitoe katika Kao langu? Unawacha wanao kuliko mimi, mpate kujinonesha na kuvila vipande vilivyo vizuri vya vipaji vyote vya tambiko vyao walio ukoo wangu wa Isiraeli.
30
Kwa hiyo ndivyo, asemavyo Bwana Mungu wa Isiraeli: Kweli nilisema, mlango wako na mlango wa baba yako na waendelee machoni pangu kale na kale. Lakini sasa ndivyo, asemavyo Bwana: Hili na liniendee mbali! Kwani anichaye nitampa macheo, lakini anibezaye atabezwa naye.
31
Utaona, siku zikija, nitakapoukata mkono wako nayo mikono yao walio wa mlango wa baba yako, asipatikane mzee katika mlango wako.
32
Ndipo, utakapoutazama ukiwa wa kao lako ukiona mema yote, atakayowafanyizia Waisiraeli, kwani siku hizo zote hatakuwapo mzee katika mlango wako.
33
Ijapo nisimwangamize ye yote wa kwako na kumtoa pangu pa kutambikia, atakuwa tu wa kuyafifiliza macho yako na wa kuikatisha roho yako tamaa, lakini wao wengi wa mlango wako watakufa watakapokuwa waume wazima.
34
Kielekezo chako yatakuwa hayo yatakayowapata wanao wawili Hofuni na Pinehasi: hao wawili watakufa siku moja.
35
kisha nitajiinulia mtambikaji mwelekevu atakayeyafanya mapenzi ya moyo wangu na ya Roho yangu; yeye nitamjengea nyumba ya kweli, aendelee siku zote machoni pake yule, nitakayempaka mafuta.
36
Nao wote watakaosazwa katika mlango wako watamjia na kumwangukia, wapate thumuni tu au mkate mdogo na kumwomba: Nipe kazi moja tu ya utambikaji, nipate kula kipande cha mkate!
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31