bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 7
1 Samuel 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
1
Watu wa Kiriati-Yearimu wakaja, wakalichukua Sanduku la Bwana kwao, wakaliingiza nyumbani mwa Abinadabu kilimani juu, naye mwanawe Elazari wakamweua, aliangalie Sanduku la Bwana.
2
Tangu siku hiyo, Sanduku la Bwana lilipokuja kukaa Kiriati-Yearimu, siku zikapita nyingi, zikawa miaka 20. Kisha mlango wote wa Waisiraeli wakageuka kumfuata Bwana na kumlilia.
3
Ndipo, Samweli alipouambia mlango wote wa Waisiraeli kwamba: Ninyi mkimgeukia Bwana kwa mioyo yote, iondoeni miungu migeni kwenu pamoja na Maastaroti! Kisha ielekezeni mioyo yenu kwake Bwana na kumtumikia yeye peke yake! Ndivyo, atakavyowaponya mikononi mwa wafilisti.
4
Ndipo, wana wa Isiraeli walipoyaondoa Mabaali na Maastaroti, wakamtumikia Bwana peke yake.
5
Kisha Samweli akasema: Wakusanyeni Waisiraeli wote Misipa, niwaombee kwake Bwana!
6
Wakakusanyika Misipa, wakachota maji, wakayamwaga mbele ya Bwana na kufunga mfungo siku hiyo na kusema huko: Tumemkosea Bwana! Kisha Samweli akawakatia wana wa Isiraeli mashauri huko Misipa.
7
Wafilisti waliposikia, ya kuwa wana wa Isiraeli wamekusanyika Misipa, wakuu wa Wafilisti wakawapandia Waisiraeli; nao Waisiraeli walipovisikia, wakawaogopa Wafilisti.
8
Ndipo, wana wa Isiraeli walipomwambia Samweli: Usikome kumlilia Bwana Mungu wetu kwa ajili yetu, atuokoe mikononi mwa Wafilisti!
9
Samweli akachukua mwana kondoo mwenye kunyonya, akamatolea Bwana kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima; samweli alipomlilia Bwana hivyo kwa ajili ya Waisiraeli, Bwana akamwitikia.
10
Ikawa, Samweli alipoiteketeza hiyo ng'ombe ya tambiko, Wafilisti wakafika kupigana nao Waisiraeli. Papo hapo Bwana akanguruma kwa sauti kubwa sana juu ya Wafilisti; ndivyo, alivyowastusha sana, kwa hiyo wakapigwa mbele yao Waisiraeli.
11
Kisha waume wa Waisiraeli wakatoka Misipa, wakawakimbiza na kuwapiga hata chini ya Beti-Kari.
12
Ndipo, Samweli alipotwaa jiwe moja, akalisimika katikati ya Misipa na Seni, akaliita jina lake Ebeni-Ezeri (Jiwe la Msaada) akisema: Bwana ametusaidia mpaka hapa.
13
Ndivyo, Wafilisti walivyonyenyekezwa, hawakurudi tena kuingia katika mipaka ya Waisiraeli, nao mkono wa Bwana ukawapinga Wafilisti siku zote za Samweli.
14
Nayo miji, Wafilisti waliyoichukua kwa Waisiraeli, ikarudi tena kuwa yao Waisiraeli toka Ekroni hata Gati, nazo nchi zao Waisiraeli wakaziponya mikononi mwa Wafilisti. Tena Waisiraeli na Waamori walikuwa wakipatana.
15
Naye Samweli akawa mwamuzi wa Waisiraeli siku zote za maisha yake.
16
Mwaka kwa mwaka akaenda kuzunguka Beteli na Gilgali na Misipa, akikata mashauri yao Waisiraeli mahali hapo pote.
17
Kisha hurudi Rama, kwani ndiko, nyumba yake ilikokuwa, tena ndiko, alikowaamulia Waisiraeli. Kisha akajenga huko pa kumtambikia Bwana.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31