bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 9
1 Samuel 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 10 →
1
Kulikuwa na mtu wa Benyamini, jina lake Kisi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorati, mwana wa Afia, mwana wa mtu wa Benyamini, naye alikuwa fundi wa vita mwenye nguvu.
2
Alikuwa na mwana wa kiume, jina lake Sauli, naye alikuwa kijana mzuri mno, kwa Waisireli hakuwako mtu mzuri zaidi kuliko yeye, naye aliwapita watu wote kwa urefu wa kichwa kimoja, kikianza kupimwa mabegani.
3
Punda wa kike wa Kisi, babake Sauli, walipopotea, Kisi akamwambia mwanawe Sauli: Chukua mmoja wao vijana, uondoke kwenda kuwatafuta hao punda!
4
Basi, akapitia milimani kwa Efuraimu, kisha akapitia hata katika nchi ya Salisa, lakini hakuwaona. Kisha akapitia katika nchi ya Saalimu, nako walikuwa hawako. Kisha akapitia katika nchi ya Benyamini, lakini hawakuwaona.
5
Kisha wakaingia katika nchi ya Sufu; ndipo, Sauli alipomwambia yule kijana, aliyekuwa naye: Haya! Na turudi, baba asiwaache wale punda, akatuhangaikia sisi.
6
Naye akamwambia: Tazama! Humu mjini yumo mtu wa Mungu, naye ni mwenye macheo, kwani yote, anayoyasema, hutimia; sasa twende huko, labda atatuonyesha njia, tutakayoishika.
7
Sauli akamwambia huyo kijana wake: Tazama! Tukienda, tutampelekea nini yule mtu? Kwani pamba zetu zimekwisha katika vyombo vyetu, hata tunzo hatunalo la kumpelekea yule mtu wa Mungu. Kiko nini, tulicho hacho?
8
Yule kijana akamjibu Sauli tena akisema: Tazama, mkononi mwangu imeonekana thumuni! Hii nitampa yule mtu wa Mungu, atuonyeshe njia yetu.
9
Hapo kale kwao Waisiraeli mtu alipokwenda kumwuliza Mungu husema: Haya! Twende kwa mtazamaji! Kwani mfumbuaji wa leo kale huitwa mtazamaji.
10
Sauli akamwambia kijana wake: Neno lako ni jema; haya! Twende! Wakaja mle mjini, yule mtu wa Mungu alimokuwa.
11
Wao walipokwea hapo pa kupandia kwenda mjini wakaona vijana wa kike waliotoka kuchota maji, wakawauliza hao: Mtazamaji yuko wapi humu?
12
Wakawajibu na kuwaambia: Tazama, yuko mbele yako! Piga mbio sana! Kwani ameingia leo humu mjini, kwa kuwa leo watu wanatambika huko kilimani pa kutambikia.
13
Mtakapoingia mjini, mtamkuta, hajapanda kilimani kula, kwani watu hawali, mpaka aje, kwani yeye kwanza sharti aibariki ng'ombe ya tambiko, kisha waalikwao hula. Sasa pandeni! Kwani siku kama hii ya leo mtamwona.
14
Walipopanda mjini na kuingia humo mjini kati, mara Samweli akatokea, akakutana nao akitaka kupanda kilimani pa kutambikia.
15
Nayo siku hiyo iliyotangulia kufika kwake Sauli Bwana alikuwa amemfumbulia Samweli masikioni mwake kwamba:
16
Kesho wakati huu nitatuma kwako mtu wa nchi ya Benyamini; yeye ndiye, utakayempaka mafuta, awe mkuu wao walio ukoo wangu wa Waisiraeli. Naye ndiye atakayewaokoa walio ukoo wangu mikononi mwa Wafilisti, kwani nimewaona walio ukoo wangu, navyo vilio vyao vimefika kwangu.
17
Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia: Tazama, yule mtu, niliyekuambia, anakuja kwako! Yeye ndiye atayewatawala walio ukoo wangu.
18
Sauli akamkaribia Samweli langoni katikati na kumwambia: Niambie, nyumba ya mtazamaji iliko!
19
Samweli akamjibu Sauli kwamba: Mtazamaji ni mimi; unitangulie kwenda huko kilimani pa kutambikia! Leo mtakula pamoja nami, kesho nitakuaga nikiisha kukuambia yote yaliyomo moyoni mwako.
20
Nao wale punda wa kike waliokupotelea leo siku ya tatu usiwahangaikie moyoni mwako! kwani wameonekana. Kumbe mema yote ya Waisiraeli siyo yako na ya mlango wote wa baba yako?
21
Sauli akajibu kwamba: Mimi si mwana wa Benyamini, nalo silo shina lililo dogo kuliko mengine ya Waisiraeli? Nao ukoo wangu ni mdogo kuliko koo zote za shina la Benyamini, mbona unaniambia maneno kama hayo?
22
Kisha Samweli akamchukua Sauli na kijana wake, akawapeleka chumbani, walimolia ng'ombe ya tambiko, akawaketisha juu kwao walioalikwa, nao walikuwa kama watu 30.
23
Samweli akamwambia mpishi: Lete hicho kipande, nilichokupa na kukuambia: Kiweke kwako!
24
Mpishi akachukua paja pamoja na nyama zilizoshikana nalo, akamwandalia Sauli. Samweli akamwambia Sauli: Tazama iliyosazwa! Jiandalie, ule! Kwani niliposema: Nimewaalika watu, umewekewa nyama hii kuwa ya saa hiihii. Basi, siku hiyo Sauli akala pamoja na Samweli.
25
Kisha wakatelemka wakitoka kilimani pa kutambikia kwenda mjini, naye Samweli akaja kuongea na Sauli darini.
26
Walipoamka asubuhi, mapambazuko yalipotokea, Samweli akamwita Sauli huko darini kwamba: Inuka, nikusindikize! Ndipo, Sauli alipoinuka, wakatoka wote wawili, yeye na Samweli, kwenda nje.
27
Walipotelemka, wafike mwishoni kwa mji, Samweli akamwambia Sauli: Mwambie kijana huyu, apite kwenda mbele yetu! Alipopita kwenda mbele, akasema: Lakini wewe simama sasa, nikuambie neno la Mungu!
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31