bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 4
1 Samuel 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 5 →
1
Waisiraeli wakatoka kupigana na Wafilisti, wakapiga makambi huko Ebeni-Ezeri; nao Wafilisti wakapiga makambi Afeki.
2
Kisha Wafilisti wakajipanga kuwaelekea Waisiraeli; mapigano yalipoenea pakubwa, Waisiraeli wakapigwa na Wafilisti, hao wakaua watu kama 4000 papo hapo porini, walipojipanga kupigana.
3
Watu walipokuja kuingia makambini, wazee wa Waisiraeli wakasema: Sababu gani Bwana ametupiga leo machoni pao Wafilisti? Na tulichukue huko Silo Sanduku la Agano la Bwana, lije lituokoe mikononi mwa adui zetu.
4
Ndipo, watu walipotuma Silo, wakalichukua huko Sanduku la Agano la Bwana Mwenye vikosi akaaye juu ya Makerubi; nao wale wana wawili wa Eli, Hofuni na Pinehasi, wakatoka huko wakilisimamia Sanduku la Agano la Mungu.
5
Ikawa, Sanduku la Agano la Bwana lilipoingia makambini, Waisiraeli wote wakapaza sauti sana na kupiga yowe, hata nchi ikatutuma.
6
Wafilisti walipozisikia sauti zao za yowe wakaulizana: Sauti hizi kuu za yowe makambini mwa Waebureo ni za nini? Wakatambua, ya kuwa Sanduku la Bwana limeingia makambini.
7
Wafilisti wakashikwa na woga, kwani walisema: Mungu ameingia makambini! Yametupata sasa! Kwani jambo kama hilo halijafanyika zamani zote.
8
Yametupata sasa! Yuko nani atakayetuponya mkononi mwake Mungu huyu mwenye nguvu? Huyu ni Mungu yule aliyewapiga Wamisri mapigo yote nyikani.
9
Lakini ninyi Wafilisti jipeni mioyo, mwe waume, msije kuwatumikia Waebureo, kama wao wanavyowatumikia ninyi. Mwe waume, mje kupigana nao!
10
Basi, Wafilisti walipopigana nao, Waisiraeli wakapigwa, wakakimbilia kwao kila mtu hemani kwake; likawa pigo kubwa sana, kwao Waisiraeli wakauawa 30000 waliokwenda kwa miguu.
11
Hata Sanduku la Mungu likatekwa, nao wale wana wawili wa Eli, Hofuni na Pinehasi, wakafa.
12
Mtu wa Benyamini akatoka hapo, walipojipanga kupigana, akapiga mbio kufika Silo siku ileile; nguo zake zilikuwa zimerarukararuka, napo juu kichwani pake palikuwa na mavumbi.
13
Alipofika akamwona Eli, akikaa langoni katika kiti chake cha ukuu kando ya njia na kuchungulia njiani, kwani moyo wake ulikuwa umehangaika kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Yule mtu alipoingia mjini kupasha habari, watu wote wa mjini wakalia.
14
Eli alipozisikia sauti za kilio akauliza: Sauti hizi za huo mtutumo ni za nini? Ndipo, yule mtu alipopiga mbio kufika kwake na kumpasha Eli hizo habari.
15
Naye Eli alikuwa mwenye miaka 98, macho yake yalikuwa yametenda kiwi, asiweze kuona.
16
Yule mtu akamwambia Eli: Mimi nimetoka hapo, walipojipanga kupigana; nami nimekimbia leo hivi kutoka hapo, walipojipanga kupigana. Akauliza: Mambo ya huko yako namna gani, mwanangu?
17
Mwenye kuleta habari akajibu na kusema: Waisiraeli wamekimbizwa na Wafilisti, likawa pigo kubwa sana kwao, nao wanao wawili, Hofuni na Pinehasi, wamekufa, hata Sanduku la Mungu limetekwa.
18
Ikawa, alipolitaja Sanduku la Mungu, ndipo, Eli alipoanguka chali hapo kitini kando ya lango, shingo lake likavunjika, akafa, kwani alikuwa mzee na mtu mnene sana. Nayo miaka, aliyokuwa mwamuzi wa Waisiraeli, ilikuwa 40.
19
Mkwewe, mkewe Pinehasi, alikuwa mwenye mimba iliyokomaa; alipopashwa hizo habari za kutekwa kwake Sanduku la Mungu nazo za kufa kwake mkwewe na mumewe, akaanguka magotini, akazaa, kwani alishikwa na uchungu wake wa kuzaa.
20
Hapo, alipotaka kufa, wanawake waliomsimamia wakamwambia: Usiogope! Kwani umezaa mtoto wa kiume; lakini hakujibu neno, wala hakusikiliza.
21
Lakini mtoto akamwita jina lake Ikabodi ni kwamba: Utukufu umeondoka kwao Waisiraeli, kwa kuwa Sanduku la Mungu lilikuwa limetekwa, nao mkwewe na mumewe walikuwa wamekufa.
22
Akasema: Utukufu umeondoka kwao Waisiraeli, kwani Sanduku la Mungu limetekwa.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31