bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Samuel 3
1 Samuel 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 4 →
1
Mtoto Samweli alipomtumikia Bwana machoni pa Eli, Neno la Bwana lilimkalia mmojammoja tu, hayakuwako maono ya wachunguzaji yaliyoenea po pote.
2
Ikawa siku zile, Eli alikuwa amelala mahali pake, nayo macho yalikuwa yameanza kuguiwa na giza, asiweze kuona vema.
3
Nayo taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, naye Samweli alikuwa amelala Jumbani mwa Bwana, Sanduku la Mungu lilimokuwa.
4
Ndipo, Bwana alipomwita Samweli, naye akaitikia: Mimi hapa!
5
Akamtokea Eli upesi, akamwambia: Mimi hapa! kwani umeniita. Akajibu: Sikukuita, rudi, ulale! Akaenda zake, akalala.
6
Bwana akaita tena mara ya pili: Samweli! Samweli akaamka, akaja kwake Eli na kumwambia: Mimi hapa! kwani umeniita. Akajibu: Sikukuita, mwanangu; rudi, ulale!
7
Naye Samweli alikuwa hajamjua Bwana bado, nalo Neno la Bwana halijamtokea bado.
8
Bwana akaendelea kuita mara ya tatu: Samweli! Akaamka, akaenda kwake Eli na kumwambia: Mimi hapa! kwani umeniita. Ndipo, Eli alipotambua, ya kuwa ni Bwana aliyemwita mtoto.
9
Kisha Eli akamwambia Samweli: Nenda, ulale! Itakapokuwa, akuite tena, itikia kwamba: Sema, Bwana! kwani mtumishi wako anasikia. Samweli akaenda, akalala mahali pake.
10
Bwana akaja, akasimama, akaita, kama alivyoita mara za kwanza: Samweli! Samweli! Samweli akaitikia: Sema! kwani mtumishi wako anasikia.
11
Bwana akamwambia Samweli: Utaniona, nikifanya jambo kwao Waisiraeli, nao wote watakaolisikia masikio yao yote mawili yatawavuma.
12
Siku hiyo nitamtimilizia Eli yote, niliyoyasema ya mlango wake, toka mwanzo hata mwisho.
13
Kwani nimempasha habari, ya kuwa nitauhukumu mlango wake kale na kale kwa ajili ya manza, walizozikora; kwani alijua, ya kuwa wanawe wanajipatia kiapizo, lakini hakuwakaripia.
14
Kwa hiyo nimeuapiza mlango wa Eli kwamba: Manza, walizozikora wao wa mlango wa Eli, hazitawezekana kale na kale kupatiwa upozi, wala kwa ng'ombe ya tambiko, wala kwa kipaji cha tambiko cho chote.
15
Kisha Samweli akaja kulala, mpaka kuche, kisha akaifungua milango ya Nyumba ya Bwana; lakini Samweli akaogopa kumsimulia Eli, aliyoyaona.
16
Eli akamwita Samweli, akasema: Mwanagu, Samweli! Akaitikia: Mimi hapa!
17
Eli akamwuliza: Ni neno gani, alilokuambia? Usinifiche kamwe! Mungu na akufanyizie hivi na hivi, ukinificha neno moja tu la hayo maneno yote, aliyokuambia.
18
Ndipo, Samweli alipomsimulia hayo maneno yote, hakumficha. Akajibu: Yeye ni Bwana, na ayafanye yaliyo mema machoni pake.
19
Samweli akakua, Bwana akiwa pamoja naye; nayo maneno yake yote hakuna hata moja, aliloliangusha chini.
20
Waisiraeli wote toka Dani hata Beri-Seba wakatambua, ya kuwa Samweli amekwisha kuelekezwa kuwa mfumbuaji wa Bwana.
21
Bwana akaendelea kuonekana huko Silo, kwani Bwana alimtokea Samweli huko Silo, kama Bwana alivyosema; kisha neno la Samweli likawajia Waisiraeli wote.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31