bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 1
Revelation 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 2 →
1
Huu ndio ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu, awaonyeshe watumwa wake mambo yatakayo kufanyika upesi. Ndipo, alipomtuma malaika wake, amweleze mtumwa wake Yohana, hayo mambo.
2
Yeye ndiye aliyelishuhudia Neno la Mungu, hata ushuhuda wa Yesu Kristo, maana aliyaona yote.
3
Wenye shangwe ndio wanaoyasoma nao wanaoyasikia maneno ya ufumbuo huu na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwani siku ziko karibu.
4
Mimi Yohana nawasalimu ninyi makundi saba ya wateule yaliyoko Asia. Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwake yeye aliopo, aliyekuwapo, atakayekuja! Tena unatoka nako kwao roho saba walioko mbele ya kiti chake cha kifalme,
5
nako kwa Yesu Kristo; huyu ni shahidi mwelekevu na mzaliwa wa kwanza wa wafu na mkuu wa wafalme wa nchini. Yeye alitupenda, akatukomboa katika makosa yetu kwa damu yake,
6
akatupatia ufalme, tuwe watambikaji wa Baba yake Mungu. Wake yeye ni utukufu na uwezo kale na kale pasio mwisho. Amin.
7
Tazameni, anakuja mawinguni, macho yote yatamwona, nayo yao waliomchoma; ndipo, makabila yote ya nchini yatakapomlilia. Ndio, ni kweli.
8
Mimi ni A na O, ni kwamba: Mwanzo na Mwisho; ndivyo, Bwana Mungu anavyosema aliopo, aliyekuwapo, atakayekuja, aliye Mwenyezi.
9
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenzenu wa maumivu na wa ufalme na wa uvumilivu, tupewao na Yesu, nilikuwa katika kisiwa kinachoitwa Patimo. Nilikuwako, maana nalilitangaza Neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.
10
Nikawapo kiroho penye siku ya Bwana, nikasikia nyuma yangu sauti kuu kama ya baragumu,
11
kwamba: Mimi ni A na O, wa kwanza na wa mwisho; unayoyaona, yaandike katika kitabu, ukitume kwa yale makundi saba ya wateule yaliyoko Efeso na Simirna na Pergamo na Tiatira na Sarde na Filadelfia na Laodikia!
12
Nikapinduka, nione, kama ni sauti ya nani iliyosema nami. Nami nilipopinduka nikaona taa saba za dhahabu.
13
Katikati ya hizo taa nikaona mwenye kufanana na Mwana wa mtu. Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu, napo kifuani alikuwa amejifunga mkanda wa dhahabu.
14
Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama pamba au kama theluji, macho yake yalikuwa kama moto unaowaka.
15
Miguu yake ilifanana na shaba nyekundu imulikayo motoni mwa jikoni, sauti yake ilikuwa kama uvumi wa maji mengi.
16
Namo mkononi mwake mwa kuume alishika nyota saba, namo kinywani mwake mlitoka upanga mkali ulio na makali pande mbili. Nao uso wake ulikuwa kama jua, liking'aa kwa nguvu zake.
17
Nami nilipomwona nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Ndipo, aliponibandikia mkono wake wa kuume, akasema: Usiogope! Mimi ndiye wa kwanza na wa mwisho
18
na mwenye uzima. Nalikuwa nimekufa, tena tazama, mimi niko, ni mwenye uzima kale na kale pasipo mwisho. Ninazo funguo za kifo na za kuzimu.
19
Basi, yaandike mambo, uliyoyaona, nayo yaliyopo nayo yatakayokuwapo, haya yatakapokwisha!
20
Liandike fumbo la zile nyota saba, ulizoziona mkononi mwangu mwa kuume, nalo fumbo la zile taa saba za dhahabu. Zile nyota saba ndio malaika wa makundi saba ya wateule, nazo taa saba ndio makundi saba ya wateule.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22