bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 2
Revelation 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 3 →
1
Malaika wa wateule walioko Efeso mwandikie: Ndivyo, anavyosema yeye anayezishika zile nyota saba mkononi mwake mwa kuume, anayekwenda katikati ya zile taa saba za dhahabu:
2
Nayajua matendo yako na usumbufu na uvumilivu wako; nakujua: huwezi kuwavumilia waovu, ukawajaribu wale wanaojisema kuwa mitume, lakini sio mitume; nawe uliwaona kuwa waongo.
3
Ukavumilia ulipoumizwa kwa ajili ya Jina langu, hukuchoka.
4
Lakini ninakuonya, ya kuwa umeuacha upendo wako wa kwanza.
5
Kumbuka, uliyoyapoteza ulipoanguka! Kisha juta, uyafanye yale matendo ya kwanza! Usipoyafanya, nitakujia, niiondoe taa yako mahali pake, ukiwa hukujuta.
6
Lakini neno hili unalo, ya kuwa unayachukia matendo yao Wanikolai, ninayoyachukia hata mimi.
7
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule! Mwenye kushinda nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulioko katika paradiso ya Mungu.
8
*Malaika wa wateule walioko Simirna mwandikie: Ndivyo, anavyosema yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, akapata kuishi tena:
9
Nayajua matendo na maumivu yako na umaskini wako, lakini u mwenye mali nyingi. Nakujua, unavyotukanwa nao wajisemao kuwa Wayuda, lakini sio, ila ni wanafuzi wake Satani.
10
Usiyaogope, utakayoteswa! Tazama, Msengenyaji atawatia wengine wenu kifungoni, mpate kujaribiwa. Nanyi mtaumizwa siku kumi. Uwe mwelekevu mpaka kufa! Ndipo, nitakapokupa kilemba cha uzima.
11
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule! Mwenye kushinda hatapotolewa na kufa kwa pili.*
12
Malaika wa wateule walioko Pergamo mwandikie: Ndivyo, anavyosema mwenye ule upanga mkali wenye makali pande mbili:
13
Napajua, unapokaa. Ni hapo, kiti cha kifalme cha Satani kilipo. Lakini unalishika sana Jina langu, hukukana, ya kuwa unanitegemea mimi, hata siku zile, shahidi wangu mwelekevu Antipa alipouawa huko kwenu, Satani anakokaa.
14
Lakini ninayokuonya, ni machache, ya kuwa unao kwako wanaoushika ufundisho wa Bileamu aliyemfundisha Balaka kukwaza wana wa Isiraeli, akiwafundisha kula nyama za tambiko na kufanya ugoni.
15
Vivyo hivyo hata wewe unao wanaoyashika mafundisho ya Wanikolai yaliyo hivyo.
16
Sasa juta! Usipojuta, nitakujia upesi, nipigane nao kwa upanga uliomo kinywani mwangu.
17
Mwenye masikio na asikie, Roho anavyowaambia wateule! Mwenye kushinda nitamgawia ile Mana iliyofichwa, kisha nitampa kijiwe cheupe, namo katika kijiwe hiki limeandikwa jina jipya lisilojulika kwa mtu, asipokuwa mwenye kulipata.
18
Malaika wa wateule walioko Tiatira mwandikie: Ndivyo, anavyosema Mwana wa Mungu aliye mwenye macho yaliyo kama moto unaowaka, ambaye miguu yake imefanana na shaba nyekundu:
19
Nayajua matendo yako ya kupenda na ya kumtegemea Mungu na ya kutumikia na ya kuvumilia kwako. Tena najua: kazi zako za mwisho ni nyingi kuliko za kwanza.
20
Lakini ninakuonya, ya kuwa humkatai mwanamke Izebeli anayejisema kuwa mfumbuaji, akiwafundisha na kuwapoteza watumwa wangu, wafanye ugoni, tena wale nyama za tambiko.
21
Nimempa siku za kujuta, lakini hataki kujuta na kuuacha ugoni wake.
22
Tazama, nitambwaga kitandani, nao waliofanya naye ugoni vilevile, waumizwe sana, wasipojuta na kuyaacha matendo yake.
23
Hata watoto wake nitawaua, wafe. Ndipo, wateule wote watakaponitambua, ya kuwa mimi ni mwenye kuyapeleleza mafigo, hata mioyo. Nami nitawapa ninyi kila mmoja, kama matendo yenu yalivyo.
24
Wengine wenu ninyi, mlioko Tiatira, msioyafuata hayo mafundisho, msiovitambua vilindi vya Satani, nawaambia ninyi kwa mfano: Siwatwiki mzigo wa wengine,
25
ila hicho, mlicho nacho, kishikeni, mpaka nitakapokuja!
26
Mwenye kushinda na kuzishika kazi zangu mpaka mwisho nitampa kuwa mkuu wa wamizimu;
27
naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, awapondeponde kama vyungu vya udongo.
28
Kama nami nilivyopewa na Baba yangu, nitampa naye nyota ya mapema.
29
Mwenye masikio na asikie, Roho anayowaambia wateule!
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22