bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 22
Revelation 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
1
Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima wenye kumetuka kama kito, ulitoka penye kiti cha kifalme cha Mungu na cha Mwana kondoo.
2
Uwanjani katikati na kandokando ya mto pande zote mbili kulikuwa na miti ya uzima izaayo matunda mara kumi na mbili, kila mwezi hutoa matunda yao, nayo majani ya miti ndiyo yanayowapa wamizimu uzima.
3
Hapatakuwapo tena chenye mwiko cho chote. Kiti cha kifalme cha Mungu na cha Mwana kondoo kitakuwamo humo mwake, nao watumwa wake watamtumikia
4
na kumwona uso wake, hata Jina lake litakuwa mapajini pao.
5
Usiku hautakuwapo tena, wala hawatautumia tena mwanga wa taa wala mwanga wa jua, kwani Bwana Mungu atawamulikia; hivyo watatawala kale na kale pasipo mwisho.
6
Kisha akaniambia: Maneno haya yapasa kutegemewa, maana ni ya kweli, naye Bwana Mungu wa roho za wafumbuaji amemtuma malaika wake, awaonyeshe watumwa wake yatakayofanyika upesi.
7
Tazama, ninakuja upesi! Mwenye shangwe ndiye atakayeyashika maneno ya ufumbuo wa kitabu hiki.
8
Nami Yohana nimeyasikia, tena nimeyaona mambo haya. Nami nilipoyasikia na kuyaona nikaanguka kusujudu penye miguu ya yule malaika aliyenionyesha mambo haya.
9
Akaniambia: Angalia, sivyo! Mimi ni mtumwa mwenzenu wewe na ndugu zako walio wafumbuaji nao wanaoyashika maneno ya kitabu hiki. Umwangukie Mungu!
10
Kisha akaniambia: Usiyafiche maneno ya ufumbuo wa kitabu hiki na kuyafunga kwa kutia muhuri! Kwani siku ziko karibu.
11
Mwenye kupotoa na afulize kupotoa! Naye mwenye uchafu na afulize kujichafua! Lakini mwenye wongofu na afulize kuyafanya yaongokayo! Naye mwenye kutakata na afulize kujitakasa!
12
Tazama, naja upesi, nao mshahara wangu wa kuwalipa ninyi uko pamoja nami, nimlipe kila mmoja, kama kazi yake ilivyo.
13
Mimi ni A na O, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.
14
Wenye shangwe ndio waliozifua nguo zao, wapewe kuufikia mti wa uzima na kuingia malangoni mwa ule mji.
15
Nje wako mbwa na wachawi na wagoni na wauaji na watambikia vinyago, nao wote wapendao uwongo na kuufanya.
16
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu, awashuhudie haya penye wateule. Mimi ni mzizi na mzao wa Dawidi, ile nyota imulikayo mapema.
17
Roho naye mchumba mke wanasema: Njoo! Naye mwenye kusikia na aseme: Njoo! Naye mwenye kuona kiu na aje! Naye ayatakaye na ateke bure maji ya uzima!
18
Mimi namshuhudia kila ayasikiaye maneno ya ufumbuo wa kitabu hiki: Mtu atakayeyaongeza maneno haya, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19
Naye atakayeyapunguza maneno ya kitabu cha ufumbuo huu, Mungu ataliondoa fungu lake penye mti wa uzima namo mwenye mji mtakatifu, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki.
20
Anayeyashuhudia haya anasema: Kweli, ninakuja upesi, Amin. Njoo, Bwana Yesu!
21
Upole wa Bwana Yesu uwakalie ninyi nyote! Amin.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22