bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 20
Revelation 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 21 →
1
Kisha nikaona malaika aliyeshuka toka mbinguni; alikuwa ameushika ufunguo wa kuzimu na mnyororo mnene mkononi mwake.
2
Akamkamata yule joka, ni yule nyoka wa kale aitwaye Msengenyaji na Satani; akamfunga miaka elfu.
3
Akamtupa kuzimuni, akamfungia lango, akatia muhuri juu yake, kusudi asiwadanganye wamizimu tena, mpaka ile miaka elfu imalizike. Itakapokwisha kutimia, sharti afunguliwe siku kidogo.
4
Kisha nikaona viti vya kifalme, tena walikuwako wenye kuvikalia; hao wakapewa nguvu za kuhukumu. Nikaziona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na kwa ajili ya Neno la Mungu, nao wasiomwangukia yule nyama wala kinyago chake waliokataa kujitia vyapa vyao mapajini pao na mikononi pao. Wakawapo na kutawala pamoja na Kristo miaka elfu.
5
Wafu waliosalia hawakurudi uzimani, mpaka ile miaka elfu ilipomalizika. Huo ndio ufufuko wa kwanza.
6
Mwenye shangwe na mwenye kutakata ndiye anayeingia katika ufufuko wa kwanza. Kufa kwa pili hakuna nguvu nao hao, ila watakuwa watambikaji wa Mungu na wa Kristo wa kutawala pamoja naye miaka elfu.
7
Hiyo miaka elfu itakapomalizika, Satani atafunguliwa kifungoni mwake;
8
ndipo, atakapotoka kuwadanganya wamizimu walioko katika pembe nne za nchi, ni wale wa Gogi na wa Magogi, awakusanye kupiga vita, nao watakuwa wengi kama mchanga wa ufukoni.
9
Wakapanda, wakafika katika nchi, ilipokuwa penye papana sana, wakalizunguka kambi la watakatifu na mji uliopendwa; ndipo, moto uliposhuka toka mbinguni, ukawala.
10
Kisha Msengenyaji aliyewadanganya akawatupa ziwani mwenye moto wa viberitiberiti, walimo yule nyama na yule mfumbuaji wa uwongo; ndiko, watakakoteswa mchana na usiku kale na kale.
11
Kisha nikaona kiti cheupe kikubwa cha kifalme naye yeye aliyekikalia. Usoni pake nchi na mbingu zikakimbia, lakini hazikuonewa mahali pao pa kuwapo.
12
Nikawaona wafu, walio wakubwa na wadogo, walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha kifalme; ndipo, vitabu vilipofunuliwa. Kulikuwako na kitabu kingine, nacho kikafunuliwa, ni kile cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa kwa yale yaliyoandikwa mle vitabuni, kama matendo yao yalivyokuwa.
13
Hata bahari ikawatoa wafu waliokuwamo mwake, nako kufa na kuzimu kukawatoa wafu waliokuwamo mwao, wakahukumiwa kila mmoja, kama matendo yao yalivyokuwa.
14
Kisha kufa na kuzimu kukatupwa ziwani mwenye moto. Huku ndiko kufa kwa pili, ni lile ziwa lenye moto.
15
Mtu asipoonekana, ya kuwa ameandikwa katika kitabu cha uzima, akatupwa ziwani mwenye moto.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22