bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 13
Revelation 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 14 →
1
Nikaona nyama mkali, akitoka baharini mwenye pembe kumi na vichwa saba; juu hizo pembe zake zilikuwa na vilemba kumi vya kifalme, napo vichwani pake palikuwa na majina ya kumtukana Mungu.
2
Huyu nyama, niliyemwona, alifanana na chui, lakini miguu yake ilikuwa kama ya nyegere; nacho kinywa chake kilikuwa kama kinywa cha simba. Yule joka akampa uwezo wake na kiti chake cha kifalme na nguvu nyingi.
3
Miongoni mwa vichwa vyake nikaona kimoja kilichokuwa, kama kimepasuliwa kwa kuuawa, lakini donda lake la kuuawa lilikuwa limepona. Ulimwengu wote ukamtazama yule nyama na kumstuka,
4
kisha wakamwangukia yule joka, kwa sababu alimpa yule nyama nguvu zake, wakamwangukia naye yule nyama wakisema: Yuko nani anayefanana na nyama huyu? Tena yuko nani anayeweza kupiga vita naye?
5
Kisha akapewa domo la kusema makuu ya kumtukana Mungu, akapewa nguvu ya kuyafanya hayo mambo yake miezi 42.
6
Ndipo, alipolifunua domo lake, amtukane Mungu, alitukane nalo Jina lake na tuo lake nao wakaao mbinguni.
7
Tena akapewa kufanya vita nao watakatifu na kuwashinda, akapewa nguvu ya kushinda hata mashina na makabila na misemo na wamizimu wote.
8
Kwa hiyo watamwangukia yeye wote wakaao nchini, ambao tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa, hawakuandikwa majina yao katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa.
9
Mtu akiwa na masikio na asikie!
10
Kama yuko mwenye kuteka, naye atatekwa; kama yuko mwenye kuua kwa upanga, naye sharti auawe kwa upanga. Hapo ndipo, watakatifu watakapovumilia kwa kumtegemea Mungu.
11
Nikaona nyama mwingine, akitoka katika nchi; huyu alikuwa na pembe mbili kama mwana kondoo, akasema kama joka.
12
Hata nguvu zote za yule nyama wa kwanza aliyemtangulia huzitumia, aishurutishe nchi nao wakaao nchini, wamwangukie yule nyama wa kwanza aliyepona donda lake la kuuawa.
13
Hufanya vielekezo vikubwa, hata kushusha moto toka mbinguni, uanguke nchini machoni pa watu.
14
Kwa hivyo vielekezo, alivyopewa kuvifanya mbele ya yule nyama, huwadanganya wakaao nchini akiwaambia wale wakaao nchini, wafanye kinyago cha mfano wa yule nyama aliyekuwa na kidonda cha upanga, akapata kupona.
15
Kisha akapewa kukitia pumzi kinyago cha yule nyama, hicho kinyago cha yule nyama kiseme; kwa hiyo nguvu yake wakauawa wote wasiokiangukia kinyago hicho cha yule nyama.
16
Kwani anawashurutisha wote, wadogo na wakubwa, wenye mali na wakosao mali, waungwana na watumwa, wajitie chapa mikononi mwao mwa kuume au mapajini pao,
17
maana mtu asiweze kununua au kuuza kitu, asipokuwa na chapa cha jina la yule nyama au kiwango cha jina lake.
18
Hapa ndipo panapotakwa werevu wa kweli; aliye mwenye akili na akifumbue kiwango cha yule nyama! Nacho kiwango chake ndicho mia sita na sitini na sita (666).
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22