bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 16
Revelation 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 17 →
1
Nikasikia sauti kuu iliyotoka Jumbani mwa Mungu, ikiwaambia wale malaika saba: Nendeni, mvimwage nchini vile vyano saba vya makali ya Mungu!
2
Pakaondoka wa kwanza, akakimwaga chano chake nchini. Ndipo, majipu maovu na mabaya yalipowatokea hao waliokuwa na chapa cha yule nyama, nao waliokiangukia kinyago chake.
3
Wa pili alipokimwaga chano chake baharini, ndipo, ilipogeuka kuwa damu kama ya mfu; kwa hiyo vikafa mle baharini vyote vilivyokuwamo vyenye uzima.
4
Wa tatu alipokimwaga chano chake katika mito na katika chemchemi za maji, ndipo, nayo yalipogeuka kuwa damu.
5
Kisha nikamsikia yule malaika wa maji, akisema: Wewe u mwongofu, uliopo, uliyekuwapo, unatakata, kwa kuwa umehukumu hivyo:
6
waliomwaga damu za watakatifu na za wafumbuaji umewapa damu, wazinywe; ndivyo, ilivyowapasa.
7
Kisha nikaisikia meza ya Bwana, ikisema: Kweli Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli na za wongofu.
8
Wa nne alipokimwaga chano chake juani, ndipo, lilipopewa kuwaunguza watu kwa moto.
9
Lakini watu walipounguzwa kwa kuchomwa na moto sana wakalitukana Jina la Mungu aliyekuwa na nguvu ya mapigo hayo, wakakataa kujuta na kumtukuza yeye.
10
Wa tano alipokimwaga chano chake kitini mwa kifalme mwa yule nyama, ndipo, ufalme wake ulipotiwa giza, wenyewe wakaziuma ndimi zao kwa kuumia sana,
11
wakamtukana Mungu wa mbingu kwa ajili ya maumivu yao, na ya majipu yao, wakakataa kujuta na kuyaacha matendo yao.
12
Wa sita alipokimwaga chano chake mle katika mto mkubwa wa Eufurati, ndipo, maji yake yalipokupwa, kusudi njia itengenezwe ya wafalme watakaotoka maawioni kwa jua.
13
Nikaona pepo tatu zenye uchafu, zikitoka domoni mwa yule joka namo domoni mwa yule nyama namo domoni mwa yule mfumbuaji wa uwongo, zikawa kama vyura;
14
kwani ndizo roho za pepo zinazofanya vielekezo. Zikawatokea wafalme wa ulimwengu wote, ziwakusanye kupiga vita, siku kubwa ya Mungu Mwenyezi itakapotimia.
15
Tazama, ninakuja kama mwizi. Mwenye shangwe ndiye atakayekesha na kuziangalia nguo zake, asitembee mwenye uchi, watu wakiyaona yake yenye soni.
16
Lakini zile pepo zikawakusanya wafalme mahali panapoitwa Kiebureo: Harmagedoni.
17
Wa saba alipokimwaga chano chake angani, ndipo, sauti kuu ilipotoka Jumbani mwa Mungu upande wa kiti cha kifalme ikisema: Imekwisha kufanyika!
18
Kukapiga umeme na uvumi na ngurumo, kisha kukawa tetemeko kubwa la nchi kupita yote yaliyokuwapo; tangu hapo, mtu alipokaa nchini, halikuwapo tetemeko lililokuwa kubwa kama hilo.
19
Ndipo, ule mji mkubwa ulipogawanyika kuwa mafungu matatu, hata miji ya wamizimu ikaanguka. Ndipo, nao mji mkubwa wa Babeli ulipokumbukwa mbele ya Mungu, upewe kinyweo cha mvinyo chungu ya makali yake.
20
Navyo visiwa vyote vikatoweka, hata milima haikuonekana tena.
21
Kisha mvua kubwa ya mawe mazito yalinganayo na makonde ikawanyeshea watu toka mbinguni. Lakini watu wakamtukana Mungu kwa ajili ya pigo kuu la mvua ya mawe, kwani pigo lake lilikuwa kubwa mno.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22