bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 12
Revelation 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 13 →
1
Kisha kukaonekana kielekezo kikubwa mbinguni: mwanamke aliyekuwa amevikwa jua alikuwa anao mwezi chini miguuni pake, napo kichwani pake alikuwa na kilemba cha nyota kumi na mbili.
2
Kwa kuwa ana mimba, akalia kwa kuona uchungu na maumivu ya kuzaa.
3
Kisha kukaonekana kielekezo kingine mbinguni, ni joka kubwa lililo jekundu kama moto; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, tena vichwani pake alikuwa mwenye vilemba saba vya kifalme.
4
Mkia wake ulikokota fungu la tatu la nyota za mbinguni, ukazibwaga nchini. Kisha huyo joka akaja kusimama mbele ya yule mwanamke aliyetaka kuzaa, kusudi hapo, atakapozaa, ammeze mtoto wake.
5
Ndivyo, alivyozaa mwana wa kiume atakayewachunga wamizimu wote kwa fimbo ya chuma. Huyu mtoto wake akapokonywa, akapelekwa kwake Mungu penye kiti chake cha kifalme,
6
naye mwanamke akakimbilia nyikani, alipokuwa na mahali, alipotengenezewa na Mungu, wamlishe hapo siku 1260.
7
Kukawa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakaja kupigana na yule joka; yule joka na malaika zake walipopiga vita,
8
hawakushinda, tena hapakuonekana mahali pao pa kukaa mbinguni.
9
Kisha yule joka kubwa akabwagwa nchini, ni yule nyoka wa kale aitwaye Msengenyaji na Satani aliyeupoteza ulimwengu wote, akabwagwa nchini, nao malaika zake wakabwagwa pamoja naye.
10
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: Sasa wokovu na uwezo na ufalme umekuwa wa Mungu wetu, nazo nguvu zimekuwa zake Kristo wake, kwani msutaji wa ndugu zetu amebwagwa nchini; ndiye aliyewasuta mbele ya Mungu wetu mchana na usiku.
11
Nao wamemshinda kwa nguvu ya damu ya Mwana kondoo na kwa nguvu ya neno la ushahidi wao. Nao hawakujipenda wenyewe mpaka kufa.
12
Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu nanyi mkaao mwake! Lakini ninyi nchi na bahari, yatawapata! Kwani Msengenyaji ameshuka kwenu ninyi mwenye makali mengi moyoni, kwani ajua, ya kuwa siku zake ni chache tu.
13
Yule joka alipoona, ya kuwa amebwagwa nchini, ndipo, alipomkimbiza yule mwanamke aliyemzaa yule mtoto wa kiume.
14
Lakini mwanamke akapewa mabawa mawili ya yule tai mkibwa, aende nyikani na kuruka, apafikie mahali pake, anapolishwa siku hizi nazo zitakazokuja nacho kipande cha siku zitakazosalia, atoke usoni pake yule joka.
15
Ndipo, yule joka alipotoa maji kinywani mwake kama mto, akamtemea yule mwanamke kwamba amtose mle mtoni.
16
Lakini nchi ikamsaidia yule mwanamke, maana hiyo nchi ikakifumbua kinywa chake, ikaunywa ule mto, yule joka alioutoa kinywani mwake.
17
Kwa hiyo yule joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake kufanya vita nao waliosalia wa uzao wake, ndio wale walioyashika maagizo yake Mungu, waliofuliza kumshuhudia Yesu.
18
Kisha nikapelekwa kusimama ufukoni penye bahari.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22