bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 9
Revelation 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 10 →
1
Malaika wa tano alipopiga baragumu, nikaona nyota iliyokuwa imetoka mbinguni, ikaanguka nchini. Kisha ikapewa ufunguo wa kisima cha kuzimu,
2
ikakifungua hicho kisima cha kuzimu. Ndipo, ulipopanda moshi kutoka mle kisimani kama moshi wa jiko kubwa. Jua likatiwa giza, hata anga vilevile kwa ajili ya moshi huo wa kisimani.
3
Mle katika moshi mkatoka nzige, wakazifunika nchi, wakapewa nguvu, kama nge wa nchi walivyo na nguvu.
4
Wakaambiwa, wasiyapotoe majani ya nchi wala cho chote kilicho kibichi, wala miti yo yote, ila wawapotoe watu tu wasio na muhuri ya Mungu mapajani.
5
Hawakupewa kuwaua, ila walipewa, wawaumize tu miezi mitano. Maumivu hayo yalikuwa kama maumivu ya nge, akimwuma mtu.
6
Siku zile watu watakutafuta kufa, wasikuone; watakutunukia kufa, lakini kufa kutawakimbia.
7
Umbo la nzige hao lilikuwa limefanana kama la farasi walio tayari kupiga vita. Vichwani pao hapo juu palikuwa kama vilemba vilivyofanana na dhahabu. Nyuso zao lilikuwa kama nyuso za watu.
8
Nywele, walizokuwa nazo, zilikuwa kama nywele za wanawake, nayo meno yao yalikuwa kama meno ya simba.
9
Vifuani walikuwa na ngao kama ngao za vyuma. Uvumi wa mabawa yao ulikuwa kama uvumi wa magari yavutwayo mbiombio na farasi wengi kwenda vitani.
10
Walikuwa wenye mikia kama ya nge yenye machomeo; namo mikiani mwao ndimo, nguvu zao zilimokuwa za kuwapotoa watu miezi mitano.
11
Wana mfalme wao, ni malaika wa kuzimu, jina lake Kiebureo huitwa Abadoni, Kigiriki huitwa Apoloni.
12
Pigo la kwanza limekwisha pita; tazama, yako bado mawili, yanakuja baadaye.
13
Malaika wa sita alipopiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe nne za meza ya Bwana ya dhahabu iliyokuwako mbele ya Mungu,
14
ikamwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu: Wafungue wale makaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa wa Eufurati.
15
Ndipo, walipofunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekewa saa hii ya siku hii ya mwezi huu wa mwaka huu, waliue fungu la tatu la watu.
16
Hesabu ya vikosi vya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi (20000000); ndiyo hesabu yao, niliyoisikia.
17
Nilipowatazama wale farasi nao waliowapanda, nikawaona kuwa hivyo: walikuwa wamevaa nguo za vyuma kama za moto, nyingine nyeusi, nyingine za manjano. Vichwa vya farasi vilikuwa kama vya simba, tena katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na viberitiberiti.
18
Fungu la tatu la watu likauawa kwa mapigo hayo matatu, kwa moto na kwa moshi na kwa viberitiberiti vilivyotoka vinywani mwao.
19
Kwani nguvu za hao farasi zimo vinywani mwao namo mikiani mwao. Kwani mikia yao imefanana na nyoka wenye vichwa; hiyo ndiyo, waliyopotoa nayo.
20
Watu waliosalia, wasiouawa na mapigo hayo, hawakuyajutia matendo ya mikono yao, maana hawakuacha kutambikia mizimu na vinyago vya dhahabu na vya fedha na vya shaba na vya mawe na vya miti visivyoweza kuona wala kusikia wala kwenda.
21
Kwa hiyo hawakujutia wala uuaji wao wala uchawi wao wala ugoni wao wala wizi wao.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22