bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 8
Revelation 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 9 →
1
Alipoifungua muhuri ya saba, vyote vilivyomo mbinguni vikawa kimya kama nusu saa.
2
Nikawaona wale malaika saba waliosimama mbele ya Mungu, wakipewa mabaragumu saba.
3
Kisha akaja malaika mwingine, akasimama mbele ya meza ya Bwana; huyu alikuwa na chetezo cha dhahabu cha kuvukizia. Akapewa uvumba mwingi, auvukize juu ya meza ya Bwana iliyo ya dhahabu, iliyoko mbele ya kiti cha kifalme, watakatifu wote watakapoomba.
4
Moshi wa uvumba ulipopanda kutoka mkononi mwa huyo malaika pamoja na maombo ya watakatifu, ukamfikia Mungu.
5
Kisha malaika akakitwaa kile chetezo cha kuvukizia, akakijaza moto uliokuwako juu ya meza ya Bwana, akakibwaga nchini. Kukawa na ngurumo na uvumi na umeme na tetemeko la nchi.
6
Ndipo, wale malaika saba waliokuwa na yale mabaragumu saba walipojiweka tayari kuyapiga.
7
Wa kwanza alipopiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na ya moto iliyochanganyika na damu, ikabwagwa nchini. Pakateketea fungu la tatu la nchi, hata fungu la tatu la miti likateketea, hata majani mabichi yote yakateketea.
8
Malaika wa pili alipopiga baragumu, pakatupwa baharini yaliyokuwa kama mlima mkubwa uliowaka moto. Ndipo, fungu la tatu la bahari lilipokuwa damu;
9
hata fungu la tatu la viumbe vya baharini vilivyokuwa vyenye uzima vikafa, hata fungu la tatu la vyombo vikaangamia.
10
Malaika wa tatu alipopiga baragumu, pakaanguka toka mbinguni nyota kubwa iliyowaka moto kama wa mwenge, ikaanguka penye fungu la tatu la mito na la chemchemi za maji.
11
Nyota hiyo jina lake huitwa Abisinto. Ndipo, fungu la tatu la maji lilipokuwa na uchungu sana. Watu wengi wakafa kwa yale maji, kwa sababu yalikuwa yenye uchungu uuao.
12
Malaika wa nne alipopiga baragumu, pakapigwa fungu la tatu la jua na fungu la tatu la mwezi na fungu la tatu la nyota; hayo mafungu yao ya tatu yakawa yenye giza, yasiangaze mchana wala usiku vilevile.
13
Nikaona, nikasikia, tai mmoja aliyeruka mbinguni kati akisema kwa sauti kuu: Kondo! Kondo! Kondo! Zitawapata wakaao katika nchi, yatakapolia mabaragumu yaliyosalia ya wale malaika watatu waendao kuyapiga!
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22