bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 11
Revelation 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 12 →
1
Kisha nikapewa mwanzi uliofanana na fimbo, nikaambiwa: Inuka, ulipime Jumba la Mungu na meza ya Bwana nao wenye kutambikia mlemle!
2
Lakini ua ulioko nje penye Jumba la Mungu uuache nje, usiupime! Kwani huo wamizimu wamepewa, waukanyage mji mtakatifu miezi 42.
3
Nami nitawapa mashahidi wangu wawili, wawafumbulie siku 1260 wakiwa wamevaa magunia.
4
Hao ndio ile michekele miwili na ile mienge miwili iliyosimama mbele ya Bwana wa nchi.
5
Tena mtu akitaka kuwapotoa, hutoka moto vinywani mwao na kuwala hao wachukivu wao. Kila atakaye kuwapotoa sharti auawe hivyo.
6
Hao wanazo nguvu za kuzifunga mbingu, mvua isinye siku za ufumbuaji wao. Tena wanazo nguvu za maji za kuyageuza kuwa damu na za kuipiga nchi mapigo yo yote napo po pote, watakapotaka.
7
Nao watakapoumalizia ushahidi wao, patatoka nyama mkali kuzimuni, atafanya vita nao, mpaka awashinde, awaue.
8
Kisha mizoga yao itakaa katika njia ya mji ule mkubwa unaoitwa kiroho Sodomu na Misri; ndipo, naye Bwana wao alipowambwa msalabani.
9
Nao watu wa makabila na wa mashina na wa misemo na wa wamizimu wataiona mizoga yao siku tatu na nusu, lakini hawataacha, mizoga yao izikwe kaburini.
10
Kwa hiyo wakaao nchini watashangilia kwa ajili yao na kupiga vigelegele na kupelekeana matunzo, kwa sababu wafumbuaji wale wawili waliwatesa wakaao nchini.
11
Lakini siku tatu na nusu zilipopita, roho ya uzima ilitoka kwa Mungu, ikawaingia; ndipo, waliposimama kwa miguu yao, woga mwingi ukawaguia waliowaona.
12
Kisha wakasikia sauti kuu toka mbinguni iliyowaambia: Pandeni huku! Walipopanda mbinguni katika wingu, wachukivu wao walikuwa wanawatazama.
13
Saa ileile pakawa tetemeko kubwa la nchi, nalo fungu la kumi la mji likafudikizwa, watu waliouawa na hilo tetemeko la nchi majina yao yalikuwa 7000. Nao waliosalia wakashikwa na woga, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
14
Pigo la pili limekwisha kupita. Tazama, la tatu linakuja upesi.
15
Malaika wa saba alipopiga baragumu, kukawa na sauti kuu nyingi mbinguni zikisema: Ufalme wa ulimwengu umekwisha kuwa wake Bwana wetu na wa Kristo wake; ndiye atakayetawala kale na kale pasipo mwisho.
16
Ndipo, wale wazee 24 waliokaa mbele ya Mungu katika viti vyao vya kifalme walipoanguka nyusoni pao, wakamsujudia Mungu
17
na kusema: Twayavumisha mema yako wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, Ndiwe aliopo naye aliyekuwapo! Umekwisha kuutwaa ufalme kwa uwezo wako mwingi.
18
Wamizimu walipopatwa na makali ndipo, makali, yako yalipotokea, ndipo, siku yako ilipotimia ya kuwahukumu wafu na ya kuwapokeza watumwa wako walio wafumbuaji nao watakatifu nao walioliogopa Jina lako, walio wadogo nao walio wakubwa. Siku imetimia ya kuwaangamiza wenye kuiangamiza nchi.
19
Kisha Jumba la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, mkaonekana mlemle Jumbani mwa Mungu Sanduku la Agano lake. Kukapiga umeme na uvumi na ngurumo, kukawa na tetemeko la nchi na mvua nyingi sana ya mawe.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22