bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 21
Revelation 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 22 →
1
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwani mbingu za kwanza nazo nchi za kwanza zilikuwa zimetoweka, nayo bahari ilikuwa haiko tena.
2
Nikauona mji mtakatifu wa Yerusalemu mpya, ukishuka toka mbinguni kwake Mungu. Ulikuwa umetengenezwa kama mchumba mke aliyepambiwa mumewe.
3
Nikasikia sauti kuu iliyotoka kitini mwa kifalme, ikisema: Tazama, kituo chake Mungu cha kukaa pamoja na watu! Humo atatua pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu atakuwa pamoja nao,
4
atayafuta machoni mwao machozi yote, hata kufa hakutakuwapo tena, wala sikitiko, wala kilio, wala maumivu hayatakuwa tena. Kwani mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita.
5
Kisha yule aliyekaa kitini mwa kifalme akasema: Tazama, navifanya vyote kuwa vipya. Akasema: Andika! Kwani maneno haya yapasa kutegemewa, maana ni ya kweli.
6
Akaniambia: Yamekwisha kufanyika. Mimi ni A na O, ni kwamba: Mwanzo na mwisho. Aonaye kiu, mimi nitampa bure ya kunywa toka kisimani mwenye maji ya uzima.
7
Mwenye kushinda atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwana wangu.
8
Lakini walio waoga nao wakataao kunitegemea nao wachukizao kwa ubaya wao nao walio wauaji na wagoni na wachawi na watambikia vinyago na waongo wote fungu lao hao limo katika ziwa linalowaka moto wa viberitiberiti. Huko ndiko kufa kwa pili.
9
Pakaja mmoja wao wale malaika saba wenye vile vyano saba vilivyojaa mapigo saba ya mwisho, akasema nami akaniambia: Njoo! Nitakuonyesha mchumba aliye mkewe Mwana kondoo.
10
Akanichukua kiroho, akanipeleka juu ya mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu wa Yerusalemu ushukao toka mbinguni kwake Mungu.
11
Utukufu wake ni ule wa Mungu; mwanga uuangazao umefanana nao wake kile kito kivipitacho vito vyenziwe vyote, kilicho kama kijiwe cha yaspi kimulikacho.
12
Ulikuwa na boma ya mawe kubwa na refu, lililokuwa na malango kumi na mawili, napo malangoni juu palikuwa na malaika kumi na wawili. Hata majina yalikuwa yameandikwa humo malangoni, ndiyo yale ya mashina kumi na mawili ya wana wa Isiraeli.
13
Maawioni kwa jua kulikuwa na malango matatu, nako kaskazini malango matatu, nako kusini malango matatu, nako machweoni kwa jua malango matatu.
14
Hilo boma la mji lilikuwa lenye misingi kumi na miwili, namo misingini mlikuwamo majina kumi na mawili, ni ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana kondoo.
15
Yule aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu wa kupimia, apate kuupima mji na malango yake na boma lake.
16
Huo mji ulikuwa umejengwa kwenye pembe nne, urefu wake ni sawa na upana wake; akaupima mji kwa ule mwanzi, ukawa kama mwendo wa siku za mchana mia nne. Urefu wake na upana wake nao urefu wake wa juu ni sawa.
17
Akalipima boma lake, likawa la mikono 144 kwa kipimo cha mtu kilichokuwa cha malaika naye.
18
Hili boma lake lilikuwa limejengwa na mawe ya yaspi, nao mji ulikuwa wa dhahabu ionayo, kama kioo kinavyoona.
19
Misingi ya boma la mji ilikuwa imepambwa na vito vyote: msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili wa safiro, wa tatu wa kalkedoni, wa nne wa sumaradi,
20
wa tano wa sardoniki, wa sita wa sardio, wa saba wa krisolito, wa nane wa berilo, wa tisa wa topazio, wa kumi wa krisopuraso, wa kumi na moja wa yakuti, wa kumi na mbili wa ametisto.
21
Malango yake kumi na mawili yalikuwa lulu kumi na mbili, kila lango moja lilikuwa limetengenezwa kwa lulu moja. Hata uwanja mkuu wa mji ulikuwa wa dhahabu uonao, kama kioo kiangafu.
22
Jumba la kuombea sikuliona humo mwake, kwani Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana kondoo ni ombeo lao,
23
Tena mji hautumii jua wala mwezi, upate kuwa wenye mwanga. Kwani utukufu wa Mungu huuangaza, naye Mwana kondoo ni taa yake.
24
Nao wamizimu wataujia huo mwanga wake, nao wafalme wa nchi huuingiza utukufu wao mumo humo.
25
Hayo malango yake hayafungwi kamwe mchana, maana usiku haumo
26
Hata utukufu na urembo wa wamizimu wataungiza mwake.
27
Lakini kilicho kibaya cho chote hakitaingia kamwe mwake, wala mwenye kufanya machukizo na uwongo, ila wale tu walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22