bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 19
Revelation 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 20 →
1
Kisha nikasikia uvumi mkuu kama wa makundi mengi ya watu waliomo mbinguni, wakisema: Haleluya! Wokovu na utukufu na uwezo ni wa Mungu wetu,
2
kwani hukumu zake ni za kweli na za wongofu. Kwani amemhukumu yule mgoni mkuu wa kike aliyeiangamiza nchi kwa ugoni wake, akamlipiza damu za watumwa wake waliouawa na mkono wake yeye.
3
Wakasema mara ya pili: Haleluya! Moshi wake hupanda juu kale na kale pasipo mwisho.
4
Ndipo, wale wazee 24 nao wale nyama wanne walipoanguka chini na kumsujudia Mungu aliyekaa kitini mwa kifalme wakisema: Amin, Haleluya!
5
Sauti ikatoka kitini mwa kifalme ikisema: Mvumisheni Mungu wetu, enyi watumwa wake nyote mnaomwogopa yeye, mlio wadogo na wakubwa!
6
Nikasikia uvumi kama wa makundi mengi na kama uvumi wa maji mengi na kama uvumi wa ngurumo yenye nguvu wa kwamba: Haleluya! Kwani mfalme ni Bwana Mungu wetu aliye Mwenyezi.
7
Tushangilie na kupiga vigelegele na kumtukuza yeye! Kwani ndoa ya Mwana kondoo imefika, naye mkewe amejitengeneza,
8
akapewa kuvaa nguo za bafta zing'aazo na kumetuka. Maana hizi nguo za bafta ndio wongofu, watakatifu waliopewa.
9
Akaniambia: Andika! Wenye shangwe ndio walioitiwa vyakula vya arusi ya Mwana kondoo. Akaniambia: Maneno haya ni yake Mungu kweli.
10
Nikaanguka miguuni pake, nimsujudie. Ndipo, aliponiambia: Angalia, sivyo! Mimi ni mtumwa mwenzenu wewe na ndugu zako walioushika ushuhuda wa Yesu; umwangukie Mungu! Kwani ule ushuhuda wa Yesu ndio Roho ya ufumbuaji.
11
Kisha nikaziona mbingu, zikifunuka, nikaona farasi mweupe; mwenye kumpanda anaitwa mwelekevu na mkweli, maana huamua kwa wongofu wa kuupigia vita.
12
Macho yake ni moto unaowaka, kichwani pake anavyo vilemba vingi vya kifalme. Analo jina, aliloandikwa; hakuna aliyelijua pasipo yeye mwenyewe.
13
Amevaa nguo iliyochovywa katika damu. Jina lake huitwa Neno la Mungu.
14
Makundi ya mbinguni yakafuatana naye, wakiwa wamepanda farasi weupe waliovikwa nguo za bafta zing'aazo na kumetuka.
15
Kinywani mwake mkatoka upanga mkali wa kuwapiga wamizimu akiwachunga kwa fimbo ya chuma. Yeye ndiye atakayekamua kamulioni mwenye mvinyo chungu ya makali ya Mungu Mwenyezi.
16
Naye alikuwa ameandikwa jina katika nguo yake penye kiuno: MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
17
Kisha nikaona malaika mmoja aliyesimama katika jua na kupaza sauti kuu akiwaambia ndege wote warukao mbinguni kati: Njoni, mkusanyikie vyakula vingi vya Mungu,
18
mpate kula nyama za miili ya wafalme na nyama za miili ya wakuu na nyama za miili ya wanguvu na nyama za miili ya farasi na ya wale waliowapanda na nyama za miili yawaungwana na ya watumwa wote walio wadogo na wakubwa!
19
Nikamwona yule nyama na wafalme wa nchini na vikosi vyao vikikusanyika, wampelekee vita yeye aliyempanda yule farasi na makundi yake.
20
Ndipo, yule nyama alipokamatwa pamoja na mfumbuaji wa uwongo; ni yule aliyevifanya vielekezo mbele yake vya kuwapoteza navyo wale waliojitia chapa cha yule nyama nao waliokiangukia kinyago chake. Wakingali wa hai hao wawili wakatupwa ziwani mwenye moto uwakao kwa nguvu za viberitiberiti vilivyomo.
21
Nao waliosalia wakauawa kwa upanga uliotoka kinywani mwake yeye aliyempanda yule farasi. Nao ndege wote wakashiba nyama za miili yao.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22