bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 14
Revelation 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 15 →
1
Kisha nikamwona Mwana kondoo, akisimama mlimani kwa Sioni juu. Pamoja naye kulikuwako watu 144000 waliokuwa wameandikwa Jina lake na Jina la Baba yake mapajini pao.
2
Nikasikia sauti toka mbinguni kama uvumi wa maji mengi na kama uvumi wa ngurumo kuu. Hizo sauti, nilizozisikia, zilikuwa kama za wapiga mazeze, wakiyapiga mazeze yao.
3
Wakaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha kifalme penye wale nyama wanne na wale wazee. Hakuwako mtu aliyeweza kujifunza ule wimbo, wasipokuwa wale 144000 waliokombolewa na kuondolewa nchini.
4
Hawa ndio wasiochafuliwa na wanawake; kwa hiyo huwa kama vijana. Tena ndio wamfuatao Mwana kondoo po pote, anapokwenda, kwa kuwa walikombolewa kwenye watu, wawe malimbuko yake Mungu nayo yake Mwana kondoo.
5
Vinywani mwao hamkuonekana uwongo; wako pasipo kilema.
6
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka mbinguni kati na kuushika Utume mwema wa kale na kale wa kuwatangazia nchini wamizimu wote na mashina yote na misemo yote na makabila yote.
7
Naye akasema kwa sauti kuu: Mcheni Mungu na kumtukuza! Kwani saa ya hukumu yake imekuja. Mwangukieni yeye aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji!
8
Pakafuata mwingine, ni malaika wa pili, akasema: Umeanguka! Umeanguka mji mkubwa wa Babeli uliowanywesha wamizimu wote mvinyo ya ugoni wake itokezayo makali.
9
Pakawafuata mwingine, ni malaika wa tatu, akasema kwa sauti kuu: Mtu akimwangukia yule nyama na kinyago chake na kujitia chapa chake pajini pake au mkononi pake,
10
huyo atakunywa mvinyo yenye makali ya Mungu, iliyoandaliwa pasipo kuchanganywa na maji katika kinyweo cha makali yake, kisha ataumizwa motoni mwenye viberitiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya Mwana kondoo.
11
Moshi wa maumivu yao hupanda kale na kale, hawapati mapumziko mchana na usiku hao waliomwangukia yule nyama na kinyago chake, nao waliojitia chapa cha jina lake.
12
Hapa ndipo, watakatifu watakapovumilia, wayashikao maagizo ya Mungu wakifuliza kumtegemea Yesu.
13
Kisha nikasikia sauti toka mbinguni, ikisema: Andika: Wenye shangwe ni wafu waliokufa na kumtegemea Bwana tangu sasa. Kweli Roho anasema: Huyapumzikia masumbuko yao, kwani matendo yao hufuatana nao.
14
Nilipotazama tena nikaona wingu jeupe, humo winguni juu palikaa aliyefanana na mwana wa mtu; alikuwa na kilemba cha dhahabu kichwani pake, mkononi mwake alishika mndu mkali.
15
Hapo akatoka malaika mwingine Jumbani mwa Mungu, akapiga sauti kuu ya kumwambia yule aliyekaa winguni juu kwamba: Tuma mndu wako, uvune! Kwani saa ya kuvuna imekuja, kwa kuwa mavuno yaliyoko nchini yamekauka.
16
Ndipo, yule aliyekaa winguni juu alipoutupa mndu wake nchini, nayo nchi ikavunwa.
17
Kisha pakatoka malaika mwingine katika Jumba la Mungu lililoko mbinguni, huyu naye alishika mndu mkali.
18
Pakatoka na malaika mwingine penye meza ya Bwana; yeye alikuwa na nguvu ya moto, akapiga sauti kuu ya kumwambia mwenye mndu mkali akisema: Tuma mndu wako mkali, uvichume vichala vya mizabibu ya nchini, kwani zabibu zake zimeiva.
19
Ndipo, malaika alipoutupa mndu wake nchini, akazichuma zabibu zilizoko nchini, akazitia katika kamulio kubwa lililojaa makali ya Mungu.
20
Namo humo kamulioni zikakamuliwa nje ya mji, ndipo, humo kamulioni mlipotoka damu, ikapajaa, ikafika mpaka penye hatamu za farasi; mtu akipazunguka ni mwendo wa siku mbili mchana kutwa.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22