bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Revelation 10
Revelation 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 11 →
1
Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu aliyeshuka toka mbinguni; vazi lake lilikuwa wingu, kofia la kichwani pake lilikuwa upindi wa Mungu, uso wake ulikuwa kama jua, miguu yake ilikuwa kama nguzo zenye moto.
2
Mkononi mwake alishika kitabu kidogo kilichokuwa kimefunuka. Mguu wake wa kuume ulikanyaga juu ya bahari, wa kushoto juu ya nchi.
3
Akapaza sauti kuu, kama simba anavyolia. Naye alipopaza sauti, ngurumo saba zilizitoa sauti zao.
4
Hizo ngurumo saba zilipokwisha sema, nalitaka kuandika. Ndipo, niliposikia sauti toka mbinguni, ikisema: Yafiche na kuyatia muhuri, hizo ngurumo saba ziliyoyasema, lakini usiyaandike!
5
Naye malaika, niliyemwona, alivyosimama mguu mmoja baharini na mmoja nchini, akauelekeza mkono wake wa kuume mbinguni,
6
akaapa na kumtaja yeye aliye Mwenye uzima kale na kale pasipo mwisho, aliyeziumba mbingu navyo vilivyomo ndani yake, hata nchi navyo vilivyomo ndani yake, hata bahari navyo vilivyomo ndani yake, akisema: Hapatakuwa siku tena,
7
ila siku ya sauti ya malaika wa saba, atakapopiga baragumu, ndipo, patakapotimia fumbo la Mungu, kama alivyowapigia mbiu njema wale wafumbuaji waliokuwa watumwa wake.
8
Ndipo, ile sauti, niliyoisikia toka mbinguni, iliposema tena nami kwamba: Nenda, ukitwae kile kitabu kidogo kilichokuwa kimefunuka, kilichomo mkononi mwa malaika aliyesimama mguu mmoja baharini na mmoja nchini!
9
Nikaenda kwa yule malaika, nikamwambia, anipe kile kitabu kidogo. Naye akaniambia: Kitwae, kile! Kitakutia uchungu tumboni mwako, lakini kinywani mwako kitakuwa kitamu kama asali.
10
Nikakitwaa kile kitabu kidogo mkononi mwa yule malaika, nikakimeza, nacho kilikuwa kitamu kama asali kinywani mwangu; lakini nilipokwisha kukimeza nikatiwa uchungu tumboni mwangu.
11
Wakaniambia: Wewe imekupasa kufumbulia tena makabila mengi na wamizimu wengi na wenye misemo mingi na wafalme wengi.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22