bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 10
Job 10
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 11 →
1
“Nayachukia maisha yangu! Malalamiko yangu nitayasema bila kizuizi. Nitasema kwa uchungu wa moyo wangu.
2
Nitamwambia Mungu: Usinihukumu. Nijulishe kisa cha kupingana nami.
3
Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu?
4
Je, una macho kama ya binadamu? Je, waona kama binadamu aonavyo?
5
Je, siku zako ni kama za binadamu? Au miaka yako kama ya binadamu,
6
hata uuchunguze uovu wangu, na kuitafuta dhambi yangu?
7
Wewe wajua kwamba mimi sina hatia, na hakuna wa kuniokoa mikononi mwako.
8
Mikono yako iliniunda na kuniumba, lakini sasa wageuka kuniangamiza.
9
Kumbuka kwamba uliniumba kwa udongo. Je, utanirudisha tena mavumbini?
10
Je, si wewe uliyenimimina kama maziwa, na kunigandisha kama jibini?
11
Uliuumba mwili wangu kwa mifupa na mishipa, ukaifunika mifupa yangu kwa nyama na ngozi.
12
Umenijalia uhai na fadhili, uangalifu wako umeisalimisha nafsi yangu.
13
Hata hivyo mambo haya uliyaficha moyoni. Lakini najua kuwa hiyo ilikuwa nia yako.
14
Ulikuwa unangojea uone kama nitatenda dhambi, ili ukatae kunisamehe uovu wangu.
15
Kama mimi ni mwovu, ole wangu! Kama mimi ni mwadilifu, siwezi kujisifu; kwani nimejaa fedheha, nikiyatazama mateso yangu.
16
Nikiinua kichwa tu waniwinda kama simba na kuniponda tena kwa maajabu yako.
17
Kila mara unao ushahidi dhidi yangu; waiongeza hasira yako dhidi yangu, waniletea maadui wapya wanishambulie.
18
“Ee Mungu, kwa nini ulinitoa tumboni mwa mama? Afadhali ningekufa kabla ya watu kuniona.
19
Ningepelekwa moja kwa moja kaburini, nikawa kama mtu asiyepata kuwako.
20
Je, siku za maisha yangu si chache? Niachie nipate faraja kidogo,
21
kabla ya kwenda huko ambako sitarudi, huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;
22
nchi ya huzuni na fujo, ambako mwanga wake ni kama giza.”
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42