bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 39
Job 39
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 40 →
1
“Je, wajua mbuzi wa milimani huzaa lini, au umewahi kuona kulungu akizaa?
2
Je, wajua huchukua mimba kwa muda gani, au siku yenyewe ya kuzaa waijua?
3
“Wajua wakati watakapochuchumaa kuzaa, wakati wa kuzaa watoto wao?
4
Watoto wao hupata nguvu, hukua hukohuko porini, kisha huwaacha mama zao na kwenda zao.
5
“Nani aliyemwacha huru pundamwitu? Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?
6
Mimi niliwapa jangwa liwe makao yao, mbuga zenye chumvi kuwa makazi yao.
7
Hujitenga kabisa na makelele ya miji, hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi.
8
Hutembeatembea milimani kupata malisho, na kutafuta chochote kilicho kibichi.
9
“Je, nyati atakubali kukutumikia? Au je, atakubali kulala zizini mwako?
10
Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba, au avute jembe la kulimia?
11
Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingi na kumwacha akufanyie kazi zako nzito?
12
Je, wamtazamia nyati akuvunie mavuno yako, na kuleta nafaka mahali pa kupuria?
13
“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha, lakini hawezi kuruka kama korongo.
14
Mbuni huyaacha mayai yake juu ya ardhi ili yapate joto mchangani;
15
lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa, au kuvunjwa na mnyama wa porini.
16
Mbuni huwatendea wanawe ukatili kama si wake, hata kazi yake ikiharibika yeye hana wasiwasi;
17
kwa sababu nilimfanya asahau hekima yake, wala sikumpa sehemu yoyote ya akili.
18
Lakini akianza kukimbia, humcheka hata farasi na mpandafarasi.
19
“Je, Yobu, ndiwe uliyewapa farasi nguvu, ukawavika shingoni manyoya marefu?
20
Je, ni wewe unayemfanya farasi aruke kama nzige? Mlio wake wa maringo ni wa ajabu!
21
Huparapara ardhi mabondeni kwa pupa; hukimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote.
22
Farasi huicheka hofu, na hatishiki; wala upanga hauwezi kumrudisha nyuma.
23
Silaha wachukuazo wapandafarasi, hugongana kwa sauti na kungaa juani.
24
Farasi husonga mbele, akitetemeka kwa hasira; tarumbeta iliapo, yeye hasimami.
25
Kila ipigwapo tarumbeta, yeye hutoa sauti; huisikia harufu ya vita toka mbali, huusikia mshindo wa makamanda wakitoa amri kwa makelele.
26
“Je, mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka, na kunyosha mabawa yake kuelekea kusini?
27
Je, tai hupaa juu kwa amri yako, na kuweka kiota chake juu milimani?
28
Tai hufanya makazi yake juu ya miamba mirefu, na ncha kali za majabali ndizo ngome zake.
29
Kutoka huko huotea mawindo, macho yake huyaona kutoka mbali.
30
Makinda yake hufyonza damu; pale ulipo mzoga ndipo alipo tai.”
← Chapter 38
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 40 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42