bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 40
Job 40
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 41 →
1
Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Yobu:
2
“Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu? Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!”
3
Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu:
4
“Mimi sifai kitu nitakujibu nini? Naufunga mdomo wangu.
5
Nilithubutu kusema na sitasema tena. Nilisisitiza lakini sitaendelea kusema zaidi.”
6
Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga:
7
“Jikaze kama mwanamume. Nitakuuliza, nawe utanijibu.
8
Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu, kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia?
9
Je, una nguvu kama mimi Mungu? Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu?
10
“Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu, ujipambe kwa utukufu na fahari.
11
Wamwagie watu hasira yako kuu; mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha.
12
Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha, uwakanyage waovu mahali walipo.
13
Wazike wote pamoja ardhini; mfunge kila mmoja kwa kifungo cha kifo.
14
Hapo nitakutambua, kwamba nguvu yako mwenyewe imekupa ushindi.
15
“Liangalie lile dude Behemothi, nililoliumba kama nilivyokuumba wewe. Hilo hula nyasi kama ng'ombe,
16
lakini mwilini lina nguvu ajabu, na misuli ya tumbo lake ni imara.
17
Huufanya mkia wake mgumu kama mwerezi, mishipa ya mapaja yake imeshonwa pamoja.
18
Mifupa yake ni mabomba ya shaba, viungo vyake ni kama pao za chuma.
19
“Hilo ni la kwanza la ajabu kati ya viumbe vyangu! Ni mimi Muumba wake niwezaye kulishinda.
20
Milima wanamocheza wanyama wote wa porini hutoa chakula chake.
21
Hujilaza chini ya vichaka vya miiba, na kujificha kati ya matete mabwawani.
22
Hujisitiri katika vivuli vya vichaka vya miiba na vya miti iotayo kando ya vijito.
23
Mto ukifurika haliogopi, halitishiki hata mto Yordani ukilifurikia kinywani.
24
Nani awezaye kuliziba macho na kuliteka? Nani awezaye kulitoboa pua kwa mtego?
25
Je, waweza kuvua dude Lewiyathani kwa ndoana, au kuufunga ulimi wake kwa kamba?
26
Je, unaweza kulitia kamba puani mwake, au kulitoboa taya kwa kulabu?
27
Je, wadhani litakusihi uliachilie? Je, litazungumza nawe kwa upole?
28
Je, litafanya mapatano nawe, ulichukue kuwa mtumishi wako milele?
29
Je, utacheza nalo kama ndege, au kulifunga kamba licheze na wajakazi wako?
30
Wadhani wavuvi watashindania bei yake? Je, wafanyabiashara watathubutu kulikata na kugawana?
31
Je, waweza kuichoma ngozi yake kwa mikuki, au kichwa chake kwa mfumo wa kuvua samaki?
32
Jaribu tu kuligusa, uone cha mtema kuni; Kamwe hutarudia tena kufanya hivyo!
← Chapter 39
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 41 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42