bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 30
Job 30
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 31 →
1
“Lakini sasa watu wananidhihaki, tena watu walio wadogo kuliko mimi; watu ambao baba zao niliwaona hawafai hata kuwaangalia mbwa wangu wakilinda kondoo.
2
Ningepata faida gani mikononi mwao, watu ambao nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
3
Katika ufukara na njaa kali walitafutatafuta cha kutafuna nyikani sehemu tupu zisizokuwa na chakula.
4
Walichuma mimea jangwani na majani msituni wakala, walikula hata mizizi ya mti wa mfagio.
5
Walifukuzwa mbali na watu, watu waliwapigia kelele kama wezi.
6
Iliwapasa kutafuta usalama mapangoni, kwenye mashimo ardhini na miambani.
7
Huko vichakani walilia kama wanyama, walikusanyika pamoja chini ya upupu.
8
Walikuwa wapumbavu wakuu na mabaradhuli ambao walilazimika kufukuzwa nchini kwa kiboko.
9
“Na sasa wamenitungia wimbo wa kunizomea, nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.
10
Wananichukia na kuniepa; wakiniona tu wanatema mate.
11
Kwa kuwa Mungu amenidhoofisha na kuniaibisha, wamekuwa huru kunitendea wapendavyo.
12
Genge la watu lainuka kunishtaki likitafuta kuniangusha kwa kunitegea. Linanishambulia ili niangamie.
13
Watu hao hukata njia yangu huchochea balaa yangu, na hapana mtu wa kuwazuia.
14
Wanakuja kama kwenye ufa mkubwa, na baada ya shambulio wanasonga mbele.
15
Hofu kuu imenishika; hadhi yangu imetoweka kama kwa upepo, na ufanisi wangu umepita kama wingu.
16
“Sasa sina nguvu yoyote nafsini mwangu; siku za mateso zimenikumba.
17
Usiku mifupa yangu yote huuma, maumivu yanayonitafuna hayapoi.
18
Mungu amenikaba kwa mavazi yangu, amenibana kama ukosi wa shati langu.
19
Amenibwaga matopeni; nimekuwa kama majivu na mavumbi.
20
Nakulilia, lakini hunijibu, nasimama kuomba lakini hunisikilizi.
21
Umegeuka kuwa mkatili kwangu, wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu.
22
Wanitupa katika upepo na kunipeperusha; wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali.
23
Naam! Najua utanipeleka tu kifoni, mahali watakapokutana wote waishio.
24
“Je, mtu akikumbwa na maangamizi hainui mkono? Je, mtu akiwa taabuni haombi msaada
25
Je, sikuwalilia wale waliokuwa na taabu? Je, sikuona uchungu kwa ajili ya maskini?
26
Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinipata, nilipongojea mwanga, giza lilikuja.
27
Moyo wangu wahangaika wala hautulii kamwe; siku za mateso zimekumbana nami.
28
Napitapita nikiomboleza, kwangu hamna jua. Nasimama hadharani kuomba msaada.
29
Kwa kilio nimekuwa ndugu yake mbwamwitu, mimi na mbuni hamna tofauti.
30
Ngozi yangu imebambuka mifupa yangu inaungua kwa homa.
31
Kinubi changu kimekuwa cha kufanya matanga filimbi yangu kwa ajili ya kuomboleza.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42