bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 24
Job 24
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 25 →
1
“Mbona Mungu Mwenye Nguvu haweki wakati maalumu wa hukumu; au kwa nini wamjuao hawazijui siku hizo zake?
2
Watu wanaoondoa alama za mipaka ya mashamba, na wengine huiba mifugo na kuilisha.
3
Huwanyanganya yatima punda wao, humweka rehani ng'ombe wa mjane.
4
Huwasukuma maskini kando ya barabara; maskini wa dunia hujificha mbele yao.
5
Kwa hiyo kama pundamwitu maskini hutafuta chakula jangwani wapate chochote cha kuwalisha watoto wao.
6
Maskini wanalazimika kuokota mabaki ya mavuno mashambani, wanaokota katika mashamba ya mizabibu ya waovu.
7
Usiku kucha hulala uchi bila nguo wakati wa baridi hawana cha kujifunikia.
8
Wamelowa kwa mvua ya milimani, hujibanza miambani kujificha wasilowe.
9
Wapo na wanaowanyakua watoto yatima vifuani mwa mama yao. Wengine huwaweka rehani watoto wa maskini.
10
Watoto hao hufanywa waende uchi bila nguo, wakivuna ngano huku njaa imewabana,
11
wakiwatengenezea waovu mafuta yao, au kukamua divai bila hata kuionja.
12
Kutoka mjini kilio cha wanaokufa chasikika, na walioumizwa hupaza sauti kuomba msaada; lakini Mungu hasikilizi kabisa sala zao.
13
“Wapo wengine waovu wasiopenda mwanga, wasiozifahamu njia za mwanga, na hawapendi kuzishika njia zake.
14
Mwuaji huamka mapema alfajiri, ili kwenda kuwaua maskini na fukara, na usiku ukifika, kazi yake ni kuiba.
15
Mzinifu naye hungojea giza liingie; akisema, ‘Hakuna atakayeniona;’ kisha huuficha uso wake kwa nguo.
16
Usiku wezi huvunja nyumba, lakini mchana hujifungia ndani; wala hawajui kabisa mwanga ni nini.
17
Kwao wote giza nene ni mwanga wa asubuhi; wao ni marafiki wa vitisho vya giza nene.
18
“Lakini mwasema: ‘Waovu huchukuliwa haraka na mafuriko ya maji, makao yao hubaki kuwa nchi iliyolaaniwa; hakuna aendaye kwenye mashamba yao ya mizabibu.’
19
Kama theluji inavyoyeyuka katika joto na ukame ndivyo Kuzimu kunavyowanyakua waovu.
20
Maana mzazi wao huwasahau watu hao, hakuna atakayewakumbuka tena. Ndivyo uovu ulivyovunjwa kama mti.
21
“Waovu huwadhulumu wanawake wasiopata watoto. Wala hawawatendei wema wanawake wajane.
22
Mungu, kwa nguvu yake huwaangamiza wenye uwezo, huinuka nao hukata tamaa ya kuishi.
23
Huwaacha waovu wajione salama, lakini macho yake huchunguza mienendo yao.
24
Waovu hufana kwa muda tu, kisha hutoweka, hunyauka na kufifia kama jani, hukatiliwa mbali kama masuke ya ngano.
25
Nani basi, awezaye kuhakikisha kuwa mimi ni mwongo na kuonesha kwamba maneno yangu si kweli?”
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42