bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 32
Job 32
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 33 →
1
Basi hawa watu watatu: Elifazi, Bildadi na Sofari, wakaacha kumjibu Yobu kwa vile alijiona kuwa mwema.
2
Ndipo Elihu, mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa ukoo wa Rama, akakasirika. Alimkasirikia Yobu kwa sababu Yobu alijiona yeye mwadilifu na sio Mungu.
3
Pia, aliwakasirikia rafiki watatu wa Yobu kwa sababu hawakuwa na la kumjibu Yobu, na hivyo kuonesha kwamba Mungu amekosa.
4
Elihu alikuwa amekaa kimya wakati hao wazee waliposema na Yobu kwa kuwa yeye alikuwa kijana kuliko wao.
5
Lakini alipoona hao watu watatu wameshindwa kumjibu Yobu, aliwaka hasira.
6
Basi, Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi akaanza kusema: “Mimi ni kijana, nyinyi ni wazee zaidi; kwa hiyo niliogopa kuwaambieni mawazo yangu.
7
Nilisema moyoni: ‘Waache wenye siku nyingi waseme, wenye miaka mingi wafundishe hekima.’
8
Lakini hiyo roho iliyomo ndani ya mtu, hiyo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu, ndio inayomwezesha mwanadamu kufahamu.
9
Si lazima kuwa mzee ili uwe na hekima wala wazee siyo wenye kufahamu lililo sawa.
10
Kwa hiyo nasema, ‘Nisikilizeni, acheni nami nitoe maoni yangu.’
11
“Basi, mimi nilingojea mlichotaka kusema, nilisikiliza misemo yenu ya hekima, mlipokuwa mnajaribu kutafuta la kusema.
12
Niliwasikiliza kwa makini sana, lakini hakuna mmoja wenu aliyemshinda Yobu; nyote mlishindwa kuyajibu maneno yake.
13
Jihadharini msije mkasema, ‘Sasa tumepata hekima. Atakayemshinda ni Mungu, sio binadamu.’
14
Maneno ya Yobu hayakuwa kwa ajili yangu, kwa hiyo sitamjibu kama mlivyomjibu nyinyi.
15
“Nyinyi mmeduwaa; mmeshindwa, nyinyi hamna cha kusema zaidi.
16
Je, ningoje tu kwa vile hamsemi, kwa sababu mnakaa tu bila kujibu kitu?
17
Mimi pia nitatoa jibu langu; mimi nitatoa pia maoni yangu.
18
Ninayo maneno mengi sana, roho yangu yanisukuma kusema.
19
Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka.
20
Ni lazima niseme ili nipate nafuu; yanipasa kufungua kinywa changu na kujibu.
21
Sitampendelea mtu yeyote wala kutumia maneno ya kubembeleza mtu.
22
Maana mimi sijui kubembeleza mtu, la sivyo, Muumba wangu angeniangamiza.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42