bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 31
Job 31
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 32 →
1
“Nimejifunga rasmi mimi mwenyewe, macho yangu yasimtazame msichana kwa tamaa.
2
Au je, nangojea nini kutoka kwa Mungu aliye juu? Mungu Mwenye Nguvu ameniwekea kitu gani?
3
Je, maafa hayawapati watu waovu na maangamizi wale watendao mabaya?
4
Je, Mungu haoni njia zangu, na kujua hatua zangu zote?
5
“Kama nimeishi kwa kufuata uongo, kama nimekuwa mbioni kudanganya watu,
6
Mungu na anipime katika mizani ya haki, naye ataona kwamba sina hatia.
7
Kama hatua zangu zimepotoka, moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu; kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi,
8
jasho langu na liliwe na mtu mwingine, mazao yangu shambani na yangolewe.
9
“Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu, kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu,
10
basi, mke wangu na ampikie mume mwingine, na wanaume wengine wamtumie.
11
Jambo hilo ni kosa kuu la jinai, uovu ambao hakimu lazima atoe adhabu.
12
Kosa langu lingekuwa kama moto, wa kuniteketeza na kuangamiza, na kuchoma kabisa mapato yangu yote.
13
Kama nimekataa kesi ya mtumishi wangu wa kiume au wa kike, waliponiletea malalamiko yao,
14
nitafanya nini basi Mungu atakaponikabili? Je, akinichunguza nitamjibu nini?
15
Maana Mungu ndiye aliyeniumba mimi na mtumishi wangu; yeye ndiye aliyetuumba sisi wote.
16
“Je, nimepata kumnyima maskini mahitaji yake au kuwafanya wajane watumaini bure?
17
Je, nimekula chakula changu peke yangu, bila kuwaachia yatima nao wapate chochote?
18
La! Tangu ujana wangu nimekuwa mlezi wao, tangu utoto wangu nimewaongoza wajane.
19
Je, nilimwona mtu anakufa kwa kukosa nguo, au maskini ambaye hana nguo ya kuvaa,
20
bila kumpa joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo wangu naye akanitakia baraka za shukrani ya moyo?
21
Kama nimenyosha mkono mahakamani dhidi ya yatima, nikijua nitapendelewa na mahakimu,
22
basi, bega langu na lingoke, mkono wangu na ukwanyuke kiwikoni mwake.
23
Maana maafa kutoka kwa Mungu ni kitisho kwangu; mimi siwezi kuukabili ukuu wake.
24
“Je, tumaini langu nimeliweka katika dhahabu, au, nimeiambia dhahabu safi, ‘Wewe ni usalama wangu?’
25
Je, nimepata kufurahia wingi wa utajiri wangu au kujivunia mapato ya mikono yangu?
26
Kama nimeliangalia jua likiangaza, na mwezi ukipita katika uzuri wake,
27
na moyo wangu ukashawishika kuviabudu, nami nikaibusu mikono yangu kwa heshima yake,
28
huo pia ungekuwa uovu wa kuadhibiwa na mahakimu maana ningekuwa mwongo mbele ya Mungu aliye juu.
29
“Je, nimefurahia kuangamia kwa adui yangu, au kufurahi alipopatwa na maafa?
30
La! Sikuruhusu kinywa changu kumtakia mabaya, kwa kumlaani ili afe.
31
Watumishi wangu wote wanasema wazi kila mgeni amekaribishwa nyumbani mwangu.
32
Msafiri hakulala nje ya nyumba yangu, nilimfungulia mlango mpita njia.
33
Je nimeficha makosa yangu kama wengine? Je nimekataa kukiri dhambi zangu?
34
Sijaogopa kusimama mbele ya umati wa watu, wala kukaa kimya au kujifungia ndani, eti kwa kuogopa kutishwa na dharau zao.
35
Laiti angekuwapo mtu wa kunisikiliza! Naweza kutia sahihi yangu katika kila nilichosema. Namwambia Mungu Mwenye Nguvu anijibu! Laiti mashtaka wanayonitolea maadui zangu yangeandikwa!
36
Ningeyavaa kwa maringo mabegani na kujivisha kichwani kama taji.
37
Ningemhesabia Mungu kila kitu nilichofanya, ningemwendea kama mwana wa mfalme.
38
Kama nimeiiba ardhi ninayoilima, nikasababisha mifereji yake iomboleze,
39
kwa kufaidika na mazao yake bila kulipa na kusababisha kifo cha wenyewe,
40
basi miiba na iote humo badala ya ngano, na magugu badala ya shayiri.” Mwisho wa hoja za Yobu.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42