bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 12
Job 12
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 13 →
1
Ndipo Yobu akajibu:
2
“Sawa! Nyinyi ni watu wa hekima. Hekima itakufa wakati ule mtakapokufa.
3
Mimi nami ni mwelewa kama nyinyi. Mimi si mtu duni kuliko nyinyi. Yote mliyosema kila mtu anajua.
4
Nimekuwa kichekesho kwa rafiki zangu: Mimi niliyemwomba Mungu na akanijibu; mimi niliye mwadilifu na bila lawama, nimekuwa kichekesho kwa watu.
5
Mtu anayestarehe hudharau msiba; kwake, msiba huwajia wale wanaoteleza.
6
Makao ya wanyanganyi yana amani; wenye kumchokoza Mungu wako salama, nguvu yao ni mungu wao.
7
Lakini waulize wanyama nao watakufunza; waulize ndege nao watakuambia.
8
Au iulize mimea nayo itakufundisha; sema na samaki nao watakuarifu.
9
Nani kati ya viumbe hivyo, asiyejua kwamba Mwenyezi-Mungu ametenda hayo?
10
Uhai wa kila kiumbe hai umo mikononi mwake; kadhalika na pumzi ya uhai wa binadamu.
11
Je, sikio haliyapimi maneno kama ulimi uonjavyo chakula?
12
Hekima iko kwa watu wazee, maarifa kwao walioishi muda mrefu.
13
Lakini hekima na uwezo ni vyake Mungu, yeye ana maarifa na ujuzi.
14
Akibomoa, hakuna awezaye kujenga upya; akimfunga mtu, hakuna awezaye kumfungua.
15
Akizuia mvua, twapata ukame; akiifungulia, nchi hupata mafuriko.
16
Yeye ana nguvu na hekima; wanaodanganywa na wanaodanganya ni wake.
17
Huwaacha washauri waende zao uchi, huwafanya waamuzi kuwa wapumbavu.
18
Huwavua wafalme vilemba vyao; na kuwafunga viunoni kamba za wafungwa;
19
Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu.
20
Huwanyanganya washauri kipawa chao cha kuongea, huwapokonya wazee hekima yao.
21
Huwamwagia wakuu aibu, huwaondolea wenye uwezo nguvu zao.
22
Huvifunua vilindi vya giza, na kuleta mwangani yaliyokuwa gizani.
23
Huyakuza mataifa kisha huyaangamiza, huyafanya yapanuke kisha huyatawanya.
24
Huwaondolea viongozi wa watu ujuzi wao, huwafanya watangetange nyikani kusiko na njia,
25
wakapapasapapasa gizani kusiko na mwanga; na kuwafanya wapepesuke kama walevi.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42