bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 14
Job 14
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 15 →
1
“Mtu ni mtoto tu wa mwanamke; huishi siku chache tena zilizojaa taabu.
2
Huchanua kama ua, kisha hunyauka. Hukimbia kama kivuli na kutoweka.
3
Ee Mungu, kwa nini unajali hata kumwangalia na kuanza kuhojiana naye?
4
Nani awezaye kutoa kitu kisafi kutoka kitu kichafu? Hakuna anayeweza.
5
Siku za kuishi binadamu zimepimwa; ee, Mungu umeipanga idadi ya miezi yake; hawezi kupita kikomo ulichomwekea.
6
Angalia pembeni basi, umwache; ili apate kufurahia siku zake kama kibarua.
7
Maana mti ukikatwa lipo tumaini la kuota, waweza kuchipua tena.
8
Japo mizizi yake itazeeka udongoni, na shina lake kufia ardhini,
9
lakini kwa harufu tu ya maji utachipua; utatoa matawi kama chipukizi.
10
Lakini mtu hufa na huo ndio mwisho wake. Akisha toa roho anabakiwa na nini tena?
11
“Kama vile maji yakaukavyo ziwani, na mto unavyokoma kutiririka,
12
ndivyo anavyokufa mtu, wala haamki tena; hataamka tena wala kugutuka, hata hapo mbingu zitakapotoweka.
13
“Laiti ungenificha kuzimu; ungenificha hadi ghadhabu yako ipoe; nao muda ulionipimia ukiisha ungenikumbuka.
14
Je, mtu akifa anaweza kuishi tena? Siku zangu zote za kazi ningekungoja hadi wakati wa kufunguliwa ufike.
15
Hapo ungeniita, nami ningeitika, wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako.
16
Ndipo ungeweza kuzihesabu hatua zangu, ungeacha kuzichunguza dhambi zangu.
17
Makosa yangu yangefungiwa katika mfuko, nawe ungeufunika uovu wangu.
18
“Lakini milima huanguka majabali hungoka mahali pake.
19
Mtiririko wa maji hula miamba, mvua kubwa hufanya mmomonyoko wa ardhi. Ndivyo nawe unavyoharibu tumaini la binadamu.
20
Wewe wamwangusha binadamu, naye akatoweka milele; waubadilisha uso wake na kumtupilia mbali.
21
Watoto wake wakiheshimika, yeye hana habari. Wakiporomoshwa, yeye haoni kabisa.
22
Huhisi tu maumivu ya mwili wake, na kuomboleza tu hali yake mbaya.”
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42