bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 29
Job 29
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 30 →
1
Kisha Yobu akaendelea na hoja yake, akasema:
2
“Laiti ningekuwa kama zamani, wakati ule ambapo Mungu alinichunga;
3
wakati taa yake iliponiangazia kichwani, na kwa mwanga wake nikatembea gizani.
4
Wakati huo nilifikia ukamilifu wa maisha, wakati urafiki wa Mungu ulikaa nyumbani kwangu.
5
Mungu Mwenye Nguvu alikuwa bado pamoja nami, na watoto wangu walinizunguka.
6
Nyakati hizo niliogelea kwenye ufanisi, miamba ilinitiririshia vijito vya mafuta!
7
Nilipokutana na wazee langoni mwa mji na kuchukua nafasi yangu mkutanoni,
8
vijana waliponiona walisimama kando, na wazee walisimama wima kwa heshima.
9
Wakuu waliponiona waliacha kuzungumza waliweka mikono juu ya midomo kuwataka watu wakae kimya.
10
Sauti za waheshimiwa zilinyamazishwa, na vinywa vyao vikafumbwa.
11
Kila aliyesikia habari zangu alinitakia heri na aliponiona, alikubali habari hizo kuwa kweli:
12
Nilimwokoa maskini aliyenililia msaada, kadhalika na yatima asiyekuwa na wa kumsaidia.
13
Waliokuwa karibu kuangamia walinitakia baraka, niliwafanya wajane waone tena furaha moyoni.
14
Uadilifu ulikuwa vazi langu; kutenda haki kulikuwa kama joho na kilemba changu.
15
Kwa vipofu nilikuwa macho ya kuwaonesha njia, kwa viwete nilikuwa miguu yao.
16
Kwa maskini nilikuwa baba yao, nilifanya bidii kutetea haki za watu nisiowajua.
17
Nilizivunja nguvu za watu waovu, nikawafanya wawaachilie mateka wao.
18
Kisha nikafikiri: Nitafia kiotani mwangu nimetulia; siku za maisha yangu zitaongezeka kama mchanga.
19
Mimi ni kama mti uliotandaza mizizi majini, umande wa usiku huburudisha matawi yangu.
20
Napata fahari mpya daima, na nguvu zangu tayari kama mshale na upinde.
21
“Wakati huo watu walinisikiliza na kungoja, walikaa kimya kungojea shauri langu.
22
Nilipomaliza kusema hawakuwa na cha kuongeza, maneno yangu yaliwakolea kama matone ya mvua.
23
Watu waliningojea kama wangojeavyo mvua, walikuwa kama watu wanaotazamia msimu wa vuli.
24
Walipokata tamaa niliwaonesha uso wa furaha, uchangamfu wa uso wangu wakaungangania.
25
Niliwatangulia kuwaongoza, nikawaonesha njia; nilikuwa kwao kama mfalme kati ya majeshi yake; kama mtu anayewafariji wenye msiba.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42