bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 34
Job 34
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 35 →
1
Kisha Elihu akaendelea kusema:
2
“Sikilizeni maneno yangu enyi wenye hekima, nitegeeni masikio yenu, nyinyi wenye ujuzi.
3
Sikio huyapima maneno, kama vile ulimi uonjavyo chakula.
4
Basi, na tuchague lililo sawa, tuamue miongoni mwetu lililo jema.
5
Basi, Yobu ametamka: ‘Mimi Yobu sina hatia, Mungu ameniondolea haki yangu.
6
Ingawa sina hatia naonekana kuwa mwongo; kidonda changu hakiponyeki ingawa sina kosa.’
7
Ni nani aliye kama Yobu ambaye kwake ubaradhuli ni kama kunywa maji?
8
Huandamana na watenda maovu hutembea na watu waovu.
9
Maana amesema, ‘Mtu hapati faida yoyote, kujisumbua kumpendeza Mungu.’
10
“Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye ujuzi. Mungu kamwe hawezi kufanya uovu; Mungu Mwenye Nguvu hawezi kufanya kosa.
11
Mungu atamlipa mtu kadiri ya matendo yake, atamlipiza kulingana na mwenendo wake.
12
Ni ukweli mtupu: Mungu hafanyi ovu; Mungu Mwenye Nguvu kamwe hapotoshi haki.
13
Je, kuna aliyemkabidhi mamlaka juu ya dunia? Uwezo wake juu ya ulimwengu ni wake peke yake.
14
Kama Mungu angejifikiria tu yeye mwenyewe, akiondoa pumzi yake ya uhai duniani,
15
viumbe vyote vingeangamia kabisa, naye binadamu angerudi mavumbini.
16
“Kama una akili sikiliza; sikiliza ninachokuambia.
17
Je, anayetawala ulimwengu kwa sheria zake anachukia haki? Je, utathubutu kumhukumu mwadilifu na mwenye nguvu?
18
Amwambiaye mfalme, ‘Wewe ni takataka!’ Na watu mashuhuri, ‘Nyinyi ni waovu!’
19
Yeye hawapendelei wakuu, wala kuwajali matajiri kuliko maskini, maana wote hao ni kazi ya mikono yake.
20
Kufumba na kufumbua hao wamekufa; hutikiswa usiku na kuaga dunia; nao wenye nguvu hufutiliwa mbali bila kutumia nguvu za mtu.
21
“Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu; yeye huziona hatua zao zote.
22
Hakuna weusi wala giza nene ambamo watenda maovu waweza kujificha.
23
Mungu hahitaji kumjulisha mtu wakati wa kumleta mbele ya mahakama yake.
24
Huwaangamiza wenye nguvu bila uchunguzi, na kuwaweka wengine mahali pao.
25
Kwa kuwa anayajua matendo yao yote, huwaporomosha usiku wakaangamia.
26
Huwachapa hadharani kwa ajili ya uovu wao,
27
kwa sababu wameacha kumfuata yeye, wakazipuuza njia zake zote.
28
Hata wakasababisha kilio cha maskini kimfikie Mungu, Mungu akasikiliza kilio chao hao walioteswa.
29
Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu? Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona,
30
liwe ni taifa au mtu mmojammoja? Hufanya hivyo, mtu mbaya asitawale, au wale wahatarishao maisha ya watu.
31
“Tuseme mtu amemwambia Mungu, ‘Nimekosa, sitatenda dhambi tena.
32
Nioneshe makosa nisiyoweza kuyaona kama nimetenda mabaya sitayarudia tena.’
33
Je, Mungu atapaswa kumwadhibu kama uonavyo wewe? Wewe ndiwe unayeamua, sio mimi. Basi, sema unachofikiri wewe.
34
Mtu yeyote mwenye akili, na kila mwenye hekima anayenisikiliza atasema:
35
‘Yobu anaongea bila kutumia akili, maneno yake hayana maana.’
36
Laiti Yobu angechunguzwa mpaka mwisho, kwa maana anajibu kama watu waovu.
37
Huongeza uasi juu ya dhambi zake; anaeneza mashaka kati yetu, na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42