bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
/
Job 41
Job 41
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
← Chapter 40
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 42 →
1
“Yeyote anayeliona hilo dude, hufa moyo na kuzirai.
2
Hakuna mtu yeyote mkali athubutuye kulishtua. Nani, basi awezaye kusimama mbele yangu?
3
Nani aliyenipa kitu, ili nitakiwe kumrudishia? Chochote kilicho chini ya mbingu ni changu.
4
“Sitaacha kukueleza juu ya viungo vya hilo dude au juu ya nguvu zake na umbo lake zuri.
5
Nani awezaye kumbambua vazi lake la nje? Nani awezaye kutoboa deraya lililovaa?
6
Nani awezaye kufungua kinywa chake? Meno yake pande zote ni kitisho!
7
Mgongo wake umefanywa kwa safu za ngao zilizoshikamana pamoja kama kwa mhuri,
8
Kila moja imeshikamana na nyingine, hata hewa haiwezi kupenya katikati yake.
9
Yameunganishwa pamoja, hata haiwezekani kuyatenganisha.
10
Likipiga chafya, mwanga huchomoza, macho yake humetameta kama jua lichomozapo.
11
Kinywani mwake hutoka mienge iwakayo, cheche za moto huruka nje.
12
Puani mwake hufuka moshi, kama vile chungu kinachochemka; kama vile magugu yawakayo.
13
Pumzi yake huwasha makaa; mwali wa moto hutoka kinywani mwake.
14
Shingo yake ina nguvu ajabu, litokeapo watu hukumbwa na hofu.
15
Misuli yake imeshikamana pamoja, imara kama chuma wala haitikisiki.
16
Moyo wake ni mgumu kama jiwe, mgumu kama jiwe la kusagia.
17
Linapoinuka, mashujaa hushikwa na woga, kwa pigo moja huwa wamezirai.
18
Hakuna upanga uwezao kulijeruhi, wala mkuki, mshale au fumo.
19
Kwake chuma ni laini kama unyasi, na shaba kama mti uliooza.
20
Mshale hauwezi kulifanya likimbie; akitupiwa mawe ya teo huyaona kama makapi.
21
Kwake, rungu ni kama kipande cha bua, hucheka likitupiwa fumo kwa wingi.
22
Tumbo lake ni kama limefunikwa na vigae vikali; hukwaruza na kurarua udongo kama chombo cha kupuria.
23
Bahari huisukasuka kama maji yachemkayo, huifanya itoe povu kama chupa ya mafuta.
24
Lipitapo huacha nyuma alama inayongaa; povu jeupe huonekana limeelea baharini.
25
Duniani hakuna kinachofanana nalo; hilo ni kiumbe kisicho na hofu.
26
Huwaona kuwa si kitu wote wenye kiburi; hilo ni mfalme wa wanyama wote wakali.”
← Chapter 40
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 42 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42