bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 1
John 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 2 →
1
Hapo mwanzo palikuwapo Neno; hilo Neno lilikuwapo kwa Mungu, naye Mungu ndiye aliyekuwa Neno.
2
Hilo lilikuwapo hapo mwanzo kwa Mungu.
3
Vyote viliumbwa nalo, pasipo hilo hakuna hata kimoja kilichoumbwa.
4
Mwake hilo ndimo, uzima ulimokuwa, nao uzima ulikuwa mwanga wa watu.
5
Mwanga huu humulika gizani, lakini giza haikuushika.
6
Palitokea mtu aliyetumwa na Mungu, jina lake Yohana.
7
Huyo alijia kushuhudu, aushuhudie mwanga, wote wapate kuutegemea kwa ajili yake.
8
Mwenyewe hakuwa mwanga, alikuja tu, aushuhudie mwanga.
9
Ndio mwanga wa kweli unaomwangaza kila mtu, tena ndio uliokuwa ukija ulimwenguni.
10
Ulikuwamo ulimwenguni, nao ulimwengu uliumbwa nao, lakini ulimwengu haukuutambua.
11
Alipofika mwake, wao waliokuwa wake hawakumpokea.
12
Lakini wo wote waliompokea aliwapa nguvu, wapate kuwa wana wa Mungu, ndio wale waliolitegemea Jina lake.
13
Hao hawakuzaliwa na damu wala na pendo la mwili wa mtu wala na pendo la mwanamume, ila wamezaliwa na Mungu.
14
Neno lilipopata kuwa mtu, akatua kwetu, nasi tukauona utukufu wake, ni utukufu kama wa mwana aliyezaliwa wa pekee na baba yake, kwani alikuwa mwenye magawio na kweli yote.*
15
*Yohana akamshuhudia yeye na kupaza sauti akisema: Huyu ndiye, niliyemsema: Ajaye nyuma yangu alikuwa mbele yangu, kwani ni mtangulizi wangu.
16
Kwani katika mema yake yaliyo mengi sisi sote tumetwaa magawio kwa magawio.
17
Kwani Maonyo tulipewa na Mose, lakini ugawiaji na ukweli umekuja na Yesu Kristo.
18
Hakuna mtu aliyemwona Mungu hapo kale po pote, Mwana wa Mungu aliyezaliwa wa pekee, aliyeambatana na Baba, ndiye aliyetusimulia.*
19
*Huu ndio ushahidi wa Yohana, Wayuda walipotuma kwake toka Yerusalemu watambikaji na Walawi, wamwulize: Wewe ndiwe nani?
20
Akaungama pasipo kukana, akaungama: Mimi siye Kristo.
21
Walipomwuliza: Sasa je? Ndiwe Elia? akasema: Mimi siye. Ndiwe mfumbuaji? akajibu: Hapana.
22
Wakamwambia: Ndiwe nani? tupate kuwajibu waliotutuma; wajisemaje?
23
Akasema: Ndimi sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Inyosheni njia ya Bwana, kama alivyosema mfumbuaji Yesaya.
24
Nao waliotumwa walikuwa wa Mafariseo.
25
Walipomwuliza wakimwambia: Mbona unabatiza, kama wewe siwe Kristo wala Elia wala mfumbuaji?
26
Yohana akawajibu: Mimi nabatiza katika maji; lakini kati yenu amesimama, msiyemjua ninyi,
27
ndiye anayekuja nyuma yangu, nami sifai kumfungulia ukanda wa kiatu chake.
28
Haya yalikuwapo huko Betania, ng'ambo ya Yordani, Yohana alikokuwa akibatiza.*
29
Kesho yake akamwona Yesu, akija kwake, akasema: Mtazameni mwana kondoo wa Mungu anayeyaondoa makosa ya ulimwengu!
30
Huyu ndiye, niliyemsema mimi: Nyuma yangu anakuja mtu aliyekuwa mbele yangu, kwani ni mtangulizi wangu.
31
Hata mimi sikumjua; ila kusudi afunuliwe Waisiraeli, ndiyo niliyojia na kubatiza katika maji.
32
Kisha Yohana akamshuhudia akisema: Nimemwona Roho, anavyoshuka toka mbinguni kama njiwa na kumkalia.
33
Nami sikumjua, lakini aliyenituma kubatiza katika maji ndiye aliyeniambia: Utakayemwona, Roho akimshukia na kumkalia, huyo ndiye anayebatiza katika Roho takatifu.
34
Nami nimemwona, nikamshuhudia: Huyu ndiye Mwana wa Mungu.
35
*Kesho yake Yohana akasimama tena na wanafunzi wake wawili,
36
akamtazama Yesu, akitembea, akasema: Mtazameni mwana kondoo wa Mungu!
37
Wale wanafunzi wake wawili waliposikia, akisema hivyo, wakamfuata Yesu.
38
Yesu akageuka, akawatazama, wanavyomfuata, akawauliza: Mwatafuta nini? Nao walipomwuliza: Rabi (maana yake ni kwamba: Mfunzi mkuu), unakaa wapi?
39
akawaambia: Njoni, mwone! Basi, wakaja, wakapaona, anapokaa, wakakaa kwake siku ile, ikawa kama saa kumi.
40
Mmoja wao hao wawili walioyasikia maneno ya Yohana na kumfuata Yesu alikuwa Anderea, ndugu ya Simoni Petero.
41
Huyu akaanza kumwona Simoni aliyekuwa ndugu yake mwenyewe, akamwambia: Tumemwona Masiya (maana yake ni Kristo).
42
Alipokwenda naye kwa Yesu, Yesu akamtazama, akasema: Wewe ndiwe Simoni, mwana wa Yohana, wewe utaitwa Kefa (maana yake: Petero - Mwamba).*
43
*Kesho yake Yesu alipotaka kutoka kwenda Galilea akamwona Filipo, akamwambia: Nifuata!
44
Lakini Filipo alikuwa mtu wa Beti-Saida, ni mji wao Anderea na Petero.
45
Filipo akamwona Natanaeli, akamwambia: Tumemwona, ambaye mambo yake aliyaandika Mose katika Maonyo, hata Wafumbuaji, ndiye Yesu, mwana wa Yosefu wa Nasareti.
46
Natanaeli alipomwambia: Je? Kiko chema kinachoweza kutoka Nasareti? Filipo akamwambia: Njoo, uone!
47
Yesu alipomwona Natanaeli, akija kwake, akasema na kumwelekea kwamba: Tazameni! Mwisiraeli wa kweli asiye na udanganyifu!
48
Natanaeli alipomwuliza: Umenitambua tangu lini? Yesu akajibu, akamwambia: Filipo alipokuwa hajakuita bado, ulipokuwa chini ya mkuyu, hapo nimekuona.
49
Ndipo, Natanaeli alipomjibu: Mfunzi mkuu, wewe ndiwe Mwana wa Mungu, wewe ndiwe mfalme wa Isiraeli.
50
Yesu akajibu, akamwambia: Unanitegemea, kwa sababu nimekuambia: Nimekuona chini ya mkuyu; utaona makubwa kuliko hayo.
51
Kisha akamwambia: Kweli kweli nawaambiani: Mtaona, mbingu zitakavyokuwa zimefunuka, nao malaika wa Mungu wanavyopanda, tena wanavyomshukia Mwana wa mtu.*
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21