bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 3
John 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 4 →
1
*Kulikuwa na mtu wa Mafariseo, jina lake Nikodemo, aliyekuwa mkuu wa Wayuda.
2
Huyo akamjia na usiku, akamwambia: Mfunzi mkuu, tunajua, ya kuwa wewe u mfunzi aliyetoka kwa Mungu, kwani hakuna mtu anayeweza kuvifanya vielekezo hivyo, unavyovifanya wewe, Mungu asipokuwa naye.
3
Yesu akajibu, akamwambia: Kweli kweli nakuambia: Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4
Nikodemo akamwambia: Mtu atawezaje kuzaliwa akiisha kuwa mzee? Ataweza kuingia tena tumboni mwa mama yake, apate kuzaliwa?
5
Yesu akajibu: Kweli kweli nakuambia: Mtu asipozaliwa majini na Rohoni, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu;
6
kilichozaliwa na mwili ni mwili, nacho kilichozaliwa na Roho ni roho.
7
Usistaajabu, nikikuambia: Sharti mzaliwe mara ya pili!
8
Upepo huvuma, upendako, nawe huusikia uvumi wake, lakini hujui, uanziako wala ukomeako. Hivyo ndivyo, kila aliyezaliwa Rohoni alivyo.
9
Nikodemo alipojibu na kumwuliza: Haya yawezekanaje kuwapo?
10
Yesu akajibu, akamwambia: Je? Wewe u mfunzi wa Isiraeli, tena haya huyatambui?
11
Kweli kweli nakuambia: Sisi huyasema, tuyajuayo; huyashuhudia, tuliyoyaona, lakini hamwupokei ushuhuda wetu!
12
Msiponitegemea, nikiwaambia mambo ya ulimwenguni, mtanitegemeaje, nikiwaambia mambo ya mbinguni?
13
Tena hakuna aliyepaa mbinguni, asipokuwa Mwana wa mtu aliyeshuka toka mbinguni.
14
Kama Mose alivyokweza nyoka jangwani, vivyo hivyo hata Mwana wa mtu sharti akwezwe,
15
kila amtegemeaye apate uzima wa kale na kale.*
16
*Kwani kwa hivyo, Mungu alivyoupenda ulimwengu, alimtoa Mwana wake wa pekee, kila amtegemeaye asiangamie, ila apate uzima wa kale na kale.
17
Kwani Mungu hakumtuma Mwana wake ulimwenguni, auhukumu ulimwengu, ila ulimwengu upate kuokolewa naye.
18
Amtegemeaye hahukumiwi; asiyemtegemea amekwisha kuhukumiwa, kwani hakulitegemea Jina la Mwana wa Pekee wa Mungu
19
Nayo hukumu ndiyo hii: mwanga ulikuja ulimwenguni, lakini watu waliipenda giza kuliko mwanga, kwa sababu matendo yao yalikuwa mabaya,
20
kwani kila mwenye kutenda maovu huuchukia mwanga, haji mwangani, matendo yake yasipatilizwe;
21
lakini mwenye kuyafanya yaliyo ya kweli huja mwangani, matendo yake yaonekane, ya kuwa yametendeka katika Mungu.*
22
Kisha Yesu na wanafunzi wake wakaenda katika nchi ya Yudea, akashinda kule pamoja nao akibatiza.
23
Lakini Yohana alikuwa akibatizia Enoni karibu ya Salemu, kwani kule kulikuwa na maji mengi, tena ndiko, watu walikomwendea, wakabatizwa naye,
24
maana Yohana alikuwa hajatiwa bado kifungoni.
25
Ikawa, wanafunzi wa Yohana walipobishana na Myuda kwa sababu ya maosho,
26
wakaja kwa Yohana, wakamwambia: Mfunzi mkuu, aliyekuwa pamoja na wewe kule ng'ambo ya Yordani, yule uliyemshuhudia wewe, tazama, huyo anabatiza, watu wote wakimwendea.
27
Yohana akajibu, akasema: Hakuna, mtu awezacho kukitwaa, asichopewa toka mbinguni.
28
Ninyi wenyewe mwanishuhudia, ya kuwa nalisema: Mimi siye Kristo ila nimetumwa, nimtangulie yeye.
29
Aliye mwenye mchumba ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama na kumsikiliza hufurahi sana kwa kuisikia sauti yake bwana arusi; basi, hiyo furaha yangu imetimia.
30
Yeye sharti akue, nami sharti nipunguke.
31
Anayekuja toka juu ni mkuu kuliko wote; aliyetoka chini ni wa nchini, husema yaliyo ya nchini; anayekuja toka mbinguni ni mkuu kuliko wote.
32
Aliyoyaona nayo aliyoyasikia, ndiyo, anayoyashuhudia, lakini hakuna anayeupokea ushuhuda wake.
33
Aupokeaye ushuhuda wake huyu anamtambulisha Mungu waziwazi, kuwa ni wa kweli;
34
kwani aliyetumwa na Mungu huyasema maneno yake Mungu, naye Mungu haigawii Roho kwa kuipima.
35
Baba humpenda Mwana, akampa yote mkononi mwake.
36
Amtegemeaye Mwana anao uzima wa kale na kale, lakini asiyemtii Mwana hataona uzima, ila makali ya Mungu humkalia.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21