bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 9
John 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 10 →
1
Alipokuwa akitambea akaona amtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa.
2
Wanafunzi wakamwuliza wakisema: Mfunzi mkuu, aliyekosa ni nani? Huyu au wazazi wake, akizaliwa kipofu?
3
Yesu akajibu: Hawakukosa wala huyu wala wazazi wake, ila alizaliwa hivyo, kazi ya Mungu ionekane kwake.
4
Sisi sharti tuzifanye kazi zake aliyenituma, mchana ukingali upo. Usiku unakuja, pasipowezekana kufanya kazi.
5
Nikingali ulimwenguni, mimi ndio mwanga wa ulimwengu.
6
Alipokwisha kuyasema haya akatena mate chini, akayavuruga hayo mate kuwa kitope, nacho kitope akampaka machoni,
7
akamwambia: Nenda, unawe katika ziwa la Siloa, ni kwamba: Aliyetumwa. Basi, akaenda, akanawa, akarudi mwenye kuona.
8
Majirani zake nao waliomwona siku zote, alivyokaa na kuombaomba, wakasema: Huyu siye aliyekuwa amekaa na kuombaomba?
9
Wengine wakasema: Ndiye; wengine wakasema: Siye, wamefanana tu; yeye akasema: Mimi ndiye.
10
Basi, wakamwuliza: Macho yako yamefumbukaje?
11
Akajibu: Yule mtu anayeitwa Yesu alivuruga kitope, akanipaka machoni, akaniambia: Uende penye ziwa la Siloa, unawe! Nikaenda, nikanawa, nikapata kuona.
12
Walipomwuliza: Yuko wapi huyo? akasema: Sijui.
13
Wakampeleka kwa Mafariseo yule aliyekuwa ni kipofu.
14
Lakini siku, Yesu alipokivuruga kitope na kumfumbua macho yake, ilikuwa ya mapumziko.
15
Mafariseo walipomwuliza tena, alivyopata kuona, akawaambia: Alinipaka kitope machoni, nikanawa, ndio naona.
16
Kwao Mafariseo walikuwako waliosema: Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwani haishiki miiko ya siku ya mapumziko. Wengine waliposema: Mtu mkosaji awezaje kuvifanya vielekezo kama hivyo? wakakosana wao kwa wao.
17
Kwa hiyo wakamwambia kipofu tena: Wewe unamwona kuwa nani, kwa sababu alikufumbua macho? Naye akasema: Ni mfumbuaji.
18
Basi, Wayuda hawakulisadiki neno lake, ya kuwa alikuwa ni kipofu, akapata kuona, mpaka walipowaita wazazi wake yeye aliyepata kuona;
19
wakawauliza: Huyu ndiye mwana wenu, mnayemsema: Alizaliwa kipofu? Sasa amepataje kuona?
20
Wazazi wake wakajibu, wakasema: Twajua, huyu ni mwana wetu, naye alizaliwa kipofu;
21
lakini hatujui, jinsi alivyopata kuona sasa, wala hatumjui sisi aliyemfumbua macho. Mwulizeni mwenyewe! Ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe.
22
Wazazi wake walisema hivyo kwa kuwaogopa Wayuda, kwani Wayuda walikuwa wamekula njama ya kwamba: Mtu atakayemwungama, kuwa ni Kristo, akatazwe kuiingia nyumba ya kuombea.
23
Kwa hiyo wazazi wake walisema: Ni mtu mzima, mwulizeni mwenyewe!
24
*Kisha wakamwita mara ya pili yule mtu aliyekuwa ni kipofu, wakamwambia: Mtukuze Mungu! Sisi twajua: Mtu huyo ni mkosaji.
25
Yule akajibu: Kama ni mkosaji, sijui; ninalolijua, ni hili moja: Mimi niliyekuwa kipofu naona sasa.
26
Walipomwuliza: Amekufanyia nini? Amekufumbua macho jinsi gani?
27
akawajibu: Nimekwisha kuwaambia; nanyi hamkusikia. Mnatakaje kuvisikia tena? Au nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?
28
Wakamtukana, wakasema: Wewe ndiwe mwanafunzi wake yule, lakini sisi tu wanafunzi wake Mose.
29
Sisi tunajua, ya kuwa Mungu alisema na Mose, lakini huyo hatumjui, alikotoka.
30
Yule mtu akajibu, akawaambia: Neno hili ni la kustaajabu, ya kuwa ninyi hamjui, alikotoka, naye amenifumbua macho!
31
Twajua, ya kuwa Mungu hasikii wakosaji; ila mtu akimwogopa Mungu na kuyafanya, ayatakayo, basi, huyo humsikia.
32
Tangu hapo kale haijasikiwa, ya kuwa mtu aliyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33
Huyo kama angekuwa hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya kitu.
34
Wakajibu, wakamwambia: Wewe uliyezaliwa wote mzima mwenye makosa, unatufundisha sisi? Wakamfukuza, atoke.
35
Kisha Yesu akasikia, ya kuwa wamemfukuza, atoke; alipomwona akasema: Unamtegemea Mwana wa mtu?
36
Yule akajibu, akasema: Ni yupi, Bwana, nipate kumtegemea?
37
Yesu akamwambia: Umekwisha kumwona, naye anayesema na wewe ndiye.
38
Ndipo, aliposema: Nakutegemea, Bwana! Akamwangukia.
39
Kisha Yesu akasema: Nimekuja katika ulimwengu huu, niuhukumu, wasioona wapate kuona nao waonao wapate kupofuka.
40
Wengine wao Mafariseo waliokuwa pamoja naye walipoyasikia haya wakamwambia: Je? Nasi tu vipofu?
41
Yesu akawaambia: Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa wenye makosa. Lakini sasa mkisema: Twaona, basi, makosa yenu yanawakalia.*
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21