bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 19
John 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 20 →
1
Ndipo, Pilato alipomchukua Yesu, akampiga viboko.
2
Kisha askari wakasuka kilemba cha miiba, wakamvika kichwani, wakamvika hata nguo ya kifalme,
3
wakamjia wakisema: Pongezi, mfalme wa Wayuda! wakampiga makofi.
4
Pilato alipotoka tena nje, akawaambia: Tazameni, ninampeleka kwenu nje, mpate kutambua, ya kuwa sioni kwake neno la kumhukumu.
5
Yesu akatoka nje, amekivaa kilemba cha miiba na nguo ya kifalme. Pilato akawaambia: Mtazameni mtu huyu!
6
Watambikaji wakuu na watumishi walipomwona wakapiga makelele wakisema: Mwambe msalabani! Mwambe msalabani! Pilato alipowaambia: Mchukueni ninyi, mmwambe msalabani! Kwani mimi sioni kwake neno la kumhukumu.
7
Wayuda wakamjibu: Sisi tuko na Maonyo, kwa Maonyo hayo sharti afe, kwani amejifanya kuwa Mwana wa Mungu.
8
Pilato alipolisikia neno hili akakaza kuogopa,
9
akaingia tena bomani, akamwuliza Yesu: Umetoka wapi? Lakini Yesu hakumjibu neno.
10
Pilato alipomwambia: Husemi na mimi? Hujui, ya kuwa nina nguvu ya kukufungua na nguvu ya kukuwamba msalabani?
11
Yesu akajibu: Hungekuwa na nguvu ya kunihukumu, kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo yule aliyenitia mikononi mwako yuko na kosa linalolipita lako.
12
Toka hapo Pilato alitafuta njia ya kumfungua. Lakini Wayuda wakapiga makelele wakisema: Unapomfungua huyu hu mpenzi wake Kaisari. Kila mwenye kujifanya kuwa mfalme humkataa Kaisari.
13
Pilato alipoyasikia maneno haya akampeleka Yesu nje, akaketi katika kiti cha uamuzi mahali panapoitwa Kiwanja cha Mawe, lakini Kiebureo: Gabata.
14
Lakini ilikuwa siku ya kuandalia Pasaka kama saa sita; alipowaambia Wayuda: Mtazameni mfalme wenu!
15
wale wakapiga makelele: Mwondoe! Mwondoe! Mwambe msalabani! Pilato alipowaambia: Nimwambe mfalme wenu msalabani? watambikaji wakuu wakajibu: Hatuna mfalme pasipo Kaisari.
16
Basi, hapo ndipo, alipomtoa, awambwe msalabani. Wakampeleka Yesu;
17
naye akajichukulia mwenyewe msalaba wake alipotoka kwenda mahali panapoitwa Fuvu la Kichwa, jina lake Kiebureo: Golgota.
18
Ndipo, walipomwamba msalabani; tena pamoja naye wakawamba misalabani wengine wawili, huku na huko, lakini Yesu katikati.
19
Pilato akaandika mwandiko, akaubandika msalabani juu; hapo palikuwa pameandikwa: YESU WA NASARETI, MFALME WA WAYUDA.
20
Mwandiko huo Wayuda wengi waliusoma, kwani mahali pale, Yesu alipowambwa msalabani, palikuwa karibu na mji. Nao ulikuwa umeandikwa Kiebureo na Kiroma na Kigriki.
21
Watambikaji wakuu wa Wayuda walipomwambia Pilato: Usiandike: Mfalme wa Wayuda, ila: Huyu amesema: Mimi ni mfalme wa Wayuda!
22
Pilato akajibu: Niliyoyaandika, basi, nimekwisha kuyaandika.
23
Askari walipokwisha kumwamba Yesu msalabani wakayachukua mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kila askari fungu moja, wakaichukua hata kanzu. Lakini ile kanzu ilikuwa pasipo mshono, toka juu yote ilikuwa imefumwa tu.
24
Kwa hiyo wakaambiana: Tusiipasue, ila tuipigie kura, ajulike atakayeipata. Imekuwa hivyo, litimie lililoandikwa: Wakajigawanyia nguo zangu, nalo vazi langu zuri wakalipigia kura. Ndio askari waliofanya hivyo.
25
Lakini penye msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama akina mama yake na ndugu ya mama yake, jina lake Maria wa Klofa, na Maria Magadalene.
26
Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi, aliyempenda, akisimama karibu, akamwambia mama yake: Mama, tazama, mwana wako huyu!
27
Kisha akamwambia yule mwanafunzi: Tazama, mama yako huyu! Tokea saa ileile yule mwanafunzi akamchukua, akampeleka nyumbani mwake.
28
Baadaye Yesu alipojua, ya kuwa yote yamekwisha timizwa, akasema: Nina kiu, kwamba nayo hayo yaliyoandikwa yapate kutimia.
29
Palikuwa pamewekwa chombo kilichojaa siki. Basi, wakachukua mwani, wakauchovya sikini, wakautia katika kivumbasi, wakampelekea kinywani.
30
Yesu alipokwisha pewa ile siki, akasema: Yamemalizika. Kisha akainama kichwa, akakata roho.
31
Kwa Wayuda siku ile ilikuwa ya kuandalia Pasaka, kwa hiyo wakamwomba Pilato, miguu yao waliowambwa misalabani ivunjwe, waondolewe, miili yao isikae misalabani siku ya mapumziko, kwani siku ile ya mapumziko ilikuwa kuu.
32
Wakaja askari, wakawavunja miguu wa kwanza na wa pili, waliowambwa misalabani pamoja naye.
33
Lakini walipofika kwa Yesu, wakiona, ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu;
34
ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, mara ikatoka damu na maji.
35
Yeye aliyeyaona hayo ameyashuhudia, nao ushuhuda wake ni wa kweli, naye anajua, ya kuwa anasema kweli, nanyi mpate kuyasadiki.
36
Kwani hayo yalikuwa, yatimie yaliyoandikwa: Hakuna mfupa wake utakaovunjwa.
37
Tena liko neno jingine lililoandikwa la kwamba: Watamtazama yule, waliyemchoma.
38
Hayo yalipokwisha, akatokea Yosefu wa Arimatia aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini alikuwa amejifichaficha kwa kuwaogopa Wayuda; yeye ndiye aliyemwomba Pilato ruhusa ya kuuondoa mwili wa Yesu. Pilato alipompa ruhusa, akaenda, akauondoa mwili wake.
39
Pakaja Nikodemo naye, ni yule aliyemjia usiku hapo kwanza, akaleta manemane iliyochanganyika na uvumba, yapata kama mizigo miwili.
40
Kisha wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga kwa sanda pamoja na yale manukato, kama Wayuda walivyozoea kuzika.
41
Mahali pale, alipowambwa msalabani palikuwa na kiunga, namo mle kiungani mlikuwa na kaburi jipya, ambalo hajazikwa mtu bado ndani yake.
42
Kwa sababu ni siku ya kuandalia kwa Wayuda, wakamweka Yesu mle, kwani lile kaburi lilikuwa karibu.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21