bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 5
John 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 6 →
1
*Kisha ilipokuwa sikukuu ya Wayuda, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.
2
Kule Yerusalemu karibu ya Lango la Kondoo kulikuwako kiziwa kiitwacho Kiebureo Betesida; hapo palikuwa na vibanda vitano.
3
Humo mlikuwa na wagonjwa wengi, kama vipofu na viwete na wenye kupooza; wote walilala mle wakingoja, maji yatukuswe.
4
Kwani mara kwa mara palishuka malaika kiziwani, akayatikisa maji; hapo, maji yalipoisha kutikiswa, aliyeingia wa kwanza akapona ugonjwa wo wote uliomshika.
5
Pale palikuwa na mtu aliyekuwa hawezi miaka 38.
6
Yesu alipomwona huyo, anavyolala, akatambua, ya kuwa imemwishia hapo miaka mingi, akamwambia: Unataka kuwa mzima?
7
Mgonjwa akamjibu: Bwana, sina mtu wa kunitia kiziwani, maji yanapotikiswa. Kila mara mimi ninapokwenda, mwingine hushuka mbele yangu.
8
Yesu akamwambia: Inuka, jitwishe kitanda chako, upate kwenda zako!
9
Papo hapo yule mtu akawa mzima, akajitwisha kitanda chake, akaenda zake.
10
Lakini siku ile ilikuwa ya mapumziko. Kwa hiyo Wayuda walimwambia yule aliyeponywa: Leo ni siku ya mapumziko, huna ruhusa ya kukichukua kitanda.
11
Lakini akawajibu: Yule aliyenipa kuwa mzima ameniambia: Jitwishe kitanda chako, upate kwenda zako!
12
Wakamwuliza: Nani huyo mtu aliyekuambia: Jitwishe, upate kwenda zako?
13
Lakini yule aliyeponywa hakumjua. Kwani Yesu alikuwa amepaepuka, kwa sababu hapo palikuwa na kundi la watu wengi.
14
Kisha Yesu akamwona Patakatifu, akamwambia: Tazama, umepata kuwa mzima! Usikose tena, maana lisikujie jambo lililo baya kuliko lile!*
15
Ndipo, yule mtu alipoondoka, akawaambia Wayuda: Ni Yesu aliyenipa kuwa mzima.
16
Kwa hiyo Wayuda wakamnyatia Yesu, kwa sababu alivifanyia hivyo siku ya mapumziko.
17
Lakini Yesu akawajibu: Baba yangu hufanya kazi mpaka sasa, nami naifanya.
18
Kwa hiyo Wayuda walikaza kutafuta njia ya kumwua, kwani hakuvunja mwiko tu wa siku ya mapumziko, ila Mungu naye alimwita Baba yake akijilinganisha na Mungu.
19
*Yesu akajibu, akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Hakuna, Mwana awezacho kukifanya kwa nguvu yake, asipokuwa amemwona Baba, anavyokifanya. Kwani yule anavyovifanya, hivyo naye Mwana huvifanya vile vile.
20
Kwani Baba anampenda Mwana, akamwonyesha vyote, anavyovifanya. Nayo matendo yaliyo makubwa kuliko haya atamwonyesha, ninyi mpate kushangaa.
21
Kwani Baba, anavyowaamsha wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo naye Mwana huwapa uzima, anaowataka.
22
Kwani hata kuhukumu Baba hamhukumu mtu, ila hukumu yote amempa Mwana,
23
wote wapate kumheshimu Mwana, kama wanavyomheshimu Baba. Mtu asiyemheshimu Mwana hamheshimu naye Baba aliyemtuma.
24
Kweli kweli nawaambiani: Mtu anayelisikia neno langu na kumtegemea aliyenituma anao uzima wa kale na kale, hafiki penye hukumu, ila ametoka penye kufa na kuingia penye uzima.
25
Kweli kweli nawaambiani: Saa inakuja na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti yake Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watapata kuwa wazima.
26
Kwani kama Baba alivyo Mwenye uzima, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa Mwenye uzima naye.
27
Akampa nao uwezo wa kuhukumu, kwani ndiye Mwana wa mtu.
28
Msilistaajabu hilo la kwamba: Saa inakuja, ndipo, wote waliomo makaburini watakapoisikia sauti yake.
29
Nao walioyafanya mema watatoka na kufufukia uzima, nao walioyafanya maovu watatoka na kufufukia hukumu.*
30
Mimi siwezi kufanya cho chote kwa shauri langu; nahukumu, kama ninavyosikia; nayo hukumu yangu huwa yenye wongofu, kwani siyatafuti, niyatakayo mimi, ila yeye aliyenituma ayatakayo.
31
Mimi ninapojishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu sio wa kweli.
32
Yuko mwingine anayenishuhudia, nami naujua ushuhuda wake, alionishuhudia, ya kuwa ndio wa kweli.
33
Ninyi mlituma kwa Yohana, naye akayashuhudia yaliyo ya kweli.
34
Lakini mimi sitaki, mtu anishuhudie, ila nayasema haya, ninyi mpate kuokoka.
35
Yule alikuwa taa inayowaka na kuangaza; lakini ninyi mlitaka kushangilia kitambo penye mwanga wake.
36
Lakini mimi ninao ushuhuda ulio mkubwa kuliko wa Yohana. Kwani zile kazi, Baba alizonipa, nizimalize, kazi zizo hizo, ninazozifanya, hunishuhudia, ya kuwa Baba amenituma.
37
Naye Baba aliyenituma yeye amenishuhudia. Ninyi hamjaisikia bado sauti yake, wala hamjaiona sura yake,
38
wala Neno lake hamnalo mioyoni mwenu, likae humo. Kwani yule, aliyemtuma, ndiye, ninyi msiyemtegemea.
39
*Chunguzeni katika Maandiko! Kwani ninyi hudhani: Humo ndimo, mtakamopatia uzima wa kale na kale. Nayo ndiyo kweli yanayonishuhudia.
40
Lakini ninyi hamtaki kuja kwangu, mpate uzima.
41
Mimi sitaki kutukuzwa na watu.
42
Lakini nimewatambua ninyi, ya kuwa hamnao upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
43
Mimi nimekuja kwa Jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei. Mwingine atakapokuja kwa jina lake mwenyewe, huyo ndiye, mtakayempokea.
44
Mwawezaje kunitegemea ninyi mnaotukuzana? Lakini utukufu utokao kwake Mungu wa pekee hamwutafuti.
45
Msiniwazie ya kwamba: Mimi nitawasuta kwa Baba; yuko msutaji wenu, ndiye Mose, ninyi mliyemngojea.
46
Kwani kama mngemtegemea Mose, basi, mngenitegemea nami, kwani yeye aliandika mambo yangu mimi.
47
Lakini msipoyategemea, aliyoyaandika yeye, mtayategemeaje, ninayoyasema mimi?*
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21