bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 14
John 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 15 →
1
Mioyo yenu isizizimke! Mtegemeeni Mungu, nami mnitegemee!
2
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama visingekuwa hivyo, ningewaambia: Nakwenda kuwatengenezea mahali.
3
Nami ijapokuwa ninakwenda kuwatengenezea mahali, nitakuja tena, niwachukue kuwapeleka mwangu, kwamba nanyi mwepo hapo, nilipo mimi.
4
Nayo njia ya kwenda pale, nitakapokwenda mimi, mmeijua.
5
Ndipo, Toma alipomwambia: Bwana, tusipopajua, unapokwenda, njia tutaijuaje?
6
Yesu akamwambia: Mimi ndiyo njia na kweli na uzima; hakuna atakayefika kwa Baba asiponishika mimi.*
7
Kama mngenitambua mimi, mngemjua hata Baba yangu. Tangu sasa mwamtambua, tena mmemwona.
8
Filipo akamwambia: Bwana, tuonyeshe Baba! hivi vitatutosha.
9
Yesu akamwambia: Miaka hii yote nipo pamoja nanyi, nawe hujanitambua, Filipo? Aliyeniona mimi amekwisha kumwona Baba. Unasemaje: Tuonyeshe Baba?
10
Huyategemei, ya kuwa mimi nimo mwa Baba, naye Baba yumo mwangu mimi? Maneno, ninayowaambia, siyasemi kwa mawazo yangu mwenyewe, ila Baba anayekaa mwangu ndiye anayezitenda kazi zake.
11
Nitegemeeni, ya kuwa mimi nimo mwake Baba, naye Baba yumo mwangu mimi! Lakini mkishindwa, nitegemeeni kwa ajili ya kazi zizo hizo!
12
Kweli kweli nawaambiani: Mwenye kunitegemea naye yeye atazifanya kazi, ninazozifanya mimi, naye atafanya zilizo kubwa kuliko hizi, maana mimi nakwenda kwa Baba.
13
Tena lo lote, mtakaloliomba katika Jina langu, nitalifanya, Baba apate kutukuzwa, kwa kuwa yumo mwake Mwana.
14
Mtakaloniomba katika Jina langu, nitalifanya.
15
*Mkinipenda yashikeni maagizo yangu!
16
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa mtuliza mioyo mwingine, akae pamoja nanyi kale na kale.
17
Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni, wala haumtambui. Ninyi mnamtambua, kwani anakaa kwenu, naye atakuwamo mwenu.
18
Sitawaacha peke yenu, nitakuja kwenu.
19
Bado kidogo ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mtaniona, kwani mimi nipo ninaishi, nanyi mtakuwa mnaishi.
20
Siku ile mtatambua ninyi, ya kuwa mimi nimo mwake Baba yangu, nanyi mmo mwangu, nami nimo mwenu.
21
Aliye na maagizo yangu, akiyashika, huyo ndiye mwenye kunipenda. Lakini mwenye kunipenda atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda nimwonyeshe, nilivyo.*
22
Yuda, lakini siye Iskariota, akamwambia: Bwana, imekuwaje, ukitaka kutuonyesha sisi, ulivyo, usipovionyesha wao wa ulimwengu?
23
*Yesu akajibu, akamwambia: Mtu akinipenda atalishika Neno langu, naye Baba yangu atampenda, nasi tutamfikia, tufanye makao kwake.
24
Asiyenipenda hayashiki maneno yangu; nalo Neno, mnalolisikia, silo langu, ila la Baba aliyenituma.
25
Haya nimewaambia nikingali kwenu.
26
Lakini yule mtuliza mioyo, yule Roho Mtakatifu, Baba atakayemtuma katika Jina langu, ndiye atakayewafundisha yote na kuwakumbusha yote, mimi niliyowaambia ninyi.
27
Nawaachia utengemano, utengemano wangu nawapani. Mimi siwapi, kama ulimwengu unavyowapa. Mioyo yenu isizizimke, wala isiogope!
28
Mmesikia, nilivyowaambia: Nakwenda zangu, tena nitawajia. Kama mngenipenda, mngefurahi, ya kuwa nakwenda kwa Baba, kwani Baba ni mkubwa kuliko mimi.
29
Sasa nimewaambia, yanapokuwa hayajafanyika bado, mpate kunitegemea, yatakapofanyika.
30
Sitasema nanyi mengi tena, kwani mtawala ulimwengu huu anakuja; lakini hakuna tena, anachokiweza kwangu mimi,
31
ni kwamba tu, ulimwengu upate kutambua, ya kuwa nampenda Baba, nikafanya hivyo, Baba alivyoniagiza., Inukeni, tutoke humu!*
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21