bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 12
John 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 13 →
1
Siku sita mbele ya kuwa Pasaka Yesu akaenda Betania, ndiko kwao Lazaro, Yesu aliyemfufua katika wafu.
2
Kule wakamwandalia chakula cha jioni, naye Marta alikuwa akiwatumikia; lakini Lazaro alikuwa mmoja wao waliokaa chakulani naye.
3
Ndipo, Maria alipoleta kichupa cha mafuta ya maua yanayoitwa Narada, ni yenye bei kubwa, nayo yalikuwa hayakuchanganywa na mengine. Akampaka Yesu miguu, kisha akaisugua miguu yake kwa nywele zake; namo nyumbani mote pia mkanukia hayo mafuta ya maua.
4
Yuda Iskariota, mmoja wao wanafunzi wake, ndiye aliyemchongea halafu, akasema:
5
Kwa sababu gani mafuta haya hayakuuzwa kwa shilingi 300, wakapewa maskini?
6
Lakini akisema hivyo, si kwa sababu ya kutunza maskini, ila kwa sababu ya kuwa mwizi; naye ndiye aliyeushika mfuko akivichukua, walivyopewa.
7
Yesu akasema: Umwache! Maana alikuwa ameyawekea siku ya kuzikwa kwangu.
8
Kwani maskini mnao kwenu siku zote, lakini mimi hamwi nami siku zote.*
9
Kundi la Wayuda wengi walipotambua, ya kuwa yuko kule, wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila walitaka kumwona naye Lazaro, aliyemfufua katika wafu.
10
Kwa hiyo watambikaji wakuu wakala njama ya kumwua hata Lazaro.
11
Kwani kwa ajili yake yeye Wayuda wengi wakaenda kule, wakamtegemea Yesu.
12
*Kesho yake wale watu wengi walioijia sikukuu waliposikia, ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,
13
wakachukua makuti ya mitende, wakatoka kumwendea, wakapaza sauti: Hosiana! Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana! Ndiye mfalme wa Isiraeli!
14
Yesu alipoona kipunda akampanda, kama ilivyoandikwa:
15
Usiogope, binti Sioni! Tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwana wa punda!
16
Hayo wanafunzi wake kwanza hawakuyatambua, ila Yesu alipokwisha kuupata utukufu wake, ndipo, walipokumbuka, ya kuwa aliandikiwa hayo, tena ndiyo, waliyomfanyizia.
17
Hata wale watu wengi waliokuwa pamoja naye, alipomfufua Lazaro katika wafu na kumwita, atoke kaburini, wakavishuhudia.
18
Kwa sababu hiyo watu wengi wakamwendea, kwani walikuwa wamesikia, ya kuwa yeye amekifanya kielekezo hicho.*
19
Mafariseo wakasemezana wao kwa wao: Tazameni, hakuna mnayoyaweza! Tazameni, watu wote pia wamekwenda kumfuata!
20
*Miongoni mwao waliopanda kutambika siku za ile sikukuu mlikuwa na Wagriki.
21
Hao wakamjia Filipo wa Beti-Saida wa Galilea, wakambembeleza wakisema: Bwana, twataka kumwona Yesu.
22
Filipo akaenda, akamwambia Anderea. Anderea na Filipo wakaenda, wakamwambia Yesu.
23
Ndipo, Yesu alipowajibu akisema: Saa imefika, Mwana wa mtu atukuzwe.
24
Kweli kweli nawaambia: Punje ya ngano isipoanguka mchangani kufia mle, hukaa peke yake yenyewe tu; lakini inapokufa huleta mbegu nyingi.
25
Mwenye kuipenda roho yake huiangamiza; naye mwenye kuichukia roho yake humu ulimwenguni ataiponya, aifikishe penye uzima wa kale na kale.
26
Mtu akinitumikia, sharti anifuate mimi; napo hapo, nilipo mimi, papo hapo hata mtumishi wangu sharti awepo. Mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.*
27
Sasa roho yangu imezizimka, nami nisemeje? Niseme: Baba, uniokoe, nisiifikie saa hiyo? Lakini kwa sababu hiyo nimeijia saa hiyo.
28
Basi, niseme: Baba, ulitukuze Jina lako! Kisha sauti ikaja toka mbinguni kwamba: Nimelitukuza, kisha nitalitukuza tena.
29
Kundi la watu waliokuwako walipoyasikia wakasema: Kumepiga ngurumo; wengine wakasema: Malaika amesema naye.
30
Yesu akajibu akisema: Sauti hii haikutoka kwa ajili yangu, ila kwa ajili yenu.
31
Sasa hukumu ya ulimwengu imetimia; hivi sasa mtawala ulimwengu huu atasukumwa, autoke.
32
Mimi nitakapokwezwa, nitoke nchini, ndipo, nitakapowavuta wote, waje kwangu.
33
Neno hili alilisema, aonyeshe, kama ni kufa gani kulikomngoja.
34
Watu wakamjibu: Sisi tumesikia katika Maonyo: Kristo atakaa kale na kale; tena inakuwaje, wewe ukisema: Mwana wa mtu sharti akwezwe juu? Huyo Mwana wa mtu ni nani?
35
Yesu akawaambia: Mwanga ungaliko kwenu siku chache. Fanyeni mwendo mnapokuwa mnao mwanga, giza isiwaguie!
36
Anayejiendea gizani hajui, anakokwenda. Mkiwa mnao mwanga utegemeeni mwanga, mpate kuwa wana wa mwanga!
37
Yesu alipokwisha kuyasema haya, akaenda zake, akajificha, wasimwone tena. Lakini ijapokuwa amefanya mbele yao vielekezo vingi kama hivyo, hawakumtegemea.
38
Imekuwa hivyo, neno, mfumbuaji Yesaya alilolisema, lipate kutimia: Bwana, yuko nani anayeutegemea utume wetu? Tena yuko nani aliyefumbuliwa, mkono wa Bwana unayoyafanya?
39
Kwa sababu hii hawakuweza kumtegemea, kwani Yesaya alisema tena:
40
Amewapofua macho, akaishupaza mioyo yao, wasije wakaona kwa macho yao, au wakajua maana kwa mioyo yao, au wakageuka, nami nikawaponya.
41
Yesaya aliyasema hayo, kwani aliuona utukufu wake, akayasema mambo yake yeye.
42
Vivyo hivyo hata katika wakubwa walikuwamo wengi waliomtegemea, lakini kwa ajili ya Mafariseo hawakuungama, wasikatazwe kuiingia nyumba ya kuombea.
43
Kwani kutukuzwa na watu walikupenda kuliko kutukuzwa na Mungu.
44
Lakini Yesu alipaza sauti, akasema: Anayenitegemea hanitegemei mimi, ila humtegemea yule aliyenituma.
45
Tena, anayeniona mimi humwona yule aliyenituma.
46
Mimi nimekuja ulimwenguni kuwa mwanga, kila anitegemeaye asikae gizani.
47
Mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu. Kwani sikujia kuuhukumu ulimwengu, ila nimejia kuuokoa ulimwengu.
48
Anikataaye, asiyapokee maneno yangu, anaye atakayemhukumu. Neno, nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
49
Kwani mimi sikuyasema maneno yangu, ila Baba mwenyewe aliyenituma ameniagiza, nitakayoyasema na kuyafundisha.
50
Nami nayajua, aliyoyaagiza, ya kuwa ni uzima wa kale na kale. Basi, ninayoyasema, ninayasema, kama Baba alivyoniambia.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21