bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 20
John 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 21 →
1
Siku ya kwanza ya juma Maria Magadalene akaenda mapema kaburini, kukingali gizagiza. Alipoliona lile jiwe, limekwisha ondolewa kaburini,
2
akapiga mbio, akamwendea Simoni Petero na yule mwanafunzi mwingine, Yesu aliyempenda, akawaambia: Wamemwondoa Bwana kaburini, nasi hatujui, walikomweka.
3
Ndipo, Petero na yule mwanafunzi mwingine walipoondoka kwenda kaburini,
4
wote wawili wakipiga mbio pamoja; lakini yule mwanafunzi mwingine akaja mbele kwa mbio, akamshinda Petero, akafika wa kwanza penye kaburi.
5
Akainama, akachungulia, akaiona sanda, imewekwa, lakini hakuingia.
6
Kisha Simoni Petero akafika akimfuata, akaingia kaburini, akaiona sanda, imewekwa;
7
lakini mharuma uliokuwa kichwani pake haukuwekwa pamoja na sanda, ila ulikuwa umekunjwa na kuwekwa mahali pake peke yake.
8
Ndipo, alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyefika wa kwanza penye kaburi, akaviona, akavisadiki.
9
Kwani hawajayajua bado yaliyoandikwa kwamba: Imempasa kufufuka katika wafu.
10
Kisha wale wanafunzi wakarudi tena kwao.
11
*Lakini Maria alikuwa amesimama nje penye kaburi akilia. Basi, alipokuwa akilia, akainama kuchungulia kaburini,
12
akaona malaika wawili wenye nguo nyeupe, wamekaa hapo, mwili wa Yesu ulipokuwa umewekwa, mmoja kichwani, mmoja miguuni.
13
Hao walipomwuliza: Mama, waliliani? akawaambia: Maana wamemwondoa Bwana wangu, nami sijui, walikomweka.
14
Alipoyasema hayo akageuka nyuma, akamwona Yesu, amesimama, lakini hakujua, ya kuwa ndiye Yesu.
15
Yesu alipomwambia: Mama, waliliani? Wamtafuta nani? alidhani, ni mlinzi wa kiunga, akamwambia: Bwana, kama wewe umemchukua, niambie, ulikomweka, nipate kwenda, nimchukue!
16
Yesu akamwambia: Maria! Ndipo, alipogeuka, akamwambia Kiebureo: Rabuni! maana yake: Mfunzi mkuu!
17
Yesu akamwambia: Usiniguse! Kwani sijapaa bado kwenda kwake Baba. Lakini uende kwa ndugu zangu, uwaambie: Ninapaa kwenda kwa Baba yangu aliye hata Baba yenu na kwa Mungu wangu aliye hata Mungu wenu.
18
Maria Magadalene akaenda, akawasimulia wanafunzi: Nimemwona Bwana, tena hayo ndiyo, aliyoniambia.*
19
*Siku ile ya kwanza ya juma kulipokuchwa, wanafunzi wakakutana, milango ya mle walimokuwa ikiwa imefungwa, maana waliwaogopa Wayuda. Mara Yesu akaja, akasimama katikati, akawaambia: Tengemaneni!
20
Naye alipokwisha kuyasema haya akawaonyesha maganja na ubavu. Wanafunzi walipomwona Bwana wakafurahi.
21
Yesu akawaambia tena: Tengemaneni! Kama Baba alivyonituma mimi, ndivyo, nami ninavyowatuma ninyi.
22
Naye alipokwisha kuyasema haya, akawapuzia, akawaambia: Pokeeni Roho takatifu!
23
Watu, mtakaowaondolea makosa, watakuwa wameondolewa. Nao watu, mtakaowafungia, watakuwa wamefungiwa.
24
Lakini Toma anayeitwa Pacha aliyekuwa mmoja wao wale kumi na wawili hakuwamo pamoja nao, Yesu alipokuja.
25
Wanafunzi wenzake walipomwambia: Tumemwona Bwana! akawajibu: Nisipoyaona makovu ya misumari maganjani mwake na kukitia kidole changu pale penye misumari, tena nisipoutia mkono wangu ubavuni mwake, sitamtegemea.
26
Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo tena, naye Toma alikuwa yumo pamoja nao. Yesu akaja, milango ilipokuwa imefungwa, akasimama katikati, akasema: Tengemaneni!
27
Kisha akamwambia Toma: Lete kidole chako hapa, uyatazame maganja yangu! Lete nao mkono wako, uutie ubavuni mwangu! Usiwe mtu asiyenitegemea, ila anitegemeaye!
28
Ndipo, Toma alipomjibu, akamwambia: Bwana wangu na Mungu wangu!
29
Yesu akamwambia: Umenitegemea, kwa sababu umeniona. Wenye shangwe ndio wanitegemeao pasipo kuona!
30
Viko vielekezo vingi vingine, Yesu alivyovifanya mbele ya wanafunzi, visivyoandikwa katika kitabu hiki.
31
Lakini hivyo vimeandikwa, mpate kuyategemea, ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wake Mungu, tena mpate uzima katika Jina lake kwa kumtegemea.*
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21