bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 7
John 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 8 →
1
Kisha Yesu alitembea huko Galilea, kwani hakutaka kutembea katika nchi ya Yudea, kwa kuwa Wayuda walitaka kumwua.
2
Lakini sikukuu ya Wayuda iitwayo ya Vibanda ilikuwa karibu.
3
Ndugu zake wakamwambia: Ondoka hapa, uende Yudea, wanafunzi wako nao wapate kuyaona matendo yako, unayoyafanya!
4
Kwani hakuna anayefanya kitu na kujifichaficha akitaka kujulikana waziwazi. Ukifanya hivyo watokee walimwengu, wakujue!
5
Kwani hata ndugu zake hawajamtegemea.
6
Kwa hiyo Yesu akawaambia: Siku zangu hazijafika bado; lakini siku zenu ziko siku zote.
7
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi hunichukia, kwani naushuhudia, ya kuwa matendo yake ni mabaya.
8
Ipandieni ninyi sikukuu hii! Mimi siipandii bado sikukuu hii, kwani siku yangu haijatimia.
9
Alipokwisha kuwaambia hivyo, akasalia Galilea.
10
Lakini ndugu zake walipokwisha kuipandia sikukuu, ndipo, naye alipopanda; lakini hakutokea wazi, alikuwa kama mtu anayejifichaficha.
11
Wayuda walimtafuta penye sikukuu, wakasema: Yuko wapi yule?
12
Kukawa na manung'uniko mengi katika makundi ya watu kwa sababu yake. Wengine walisema: Ni mtu mwema; wengine walisema: Sio, ila hupoteza watu tu.
13
Lakini hapana aliyemsemea mbele ya watu, kwa sababu waliwaogopa Wayuda.
14
Lakini siku za katikati za sikukuu Yesu akapanda kupaingia Patakatifu, akafundisha.
15
Wayuda walipostaajabu wakisema: Huyu anajuaje Maandiko, naye hakufundishwa?
16
Yesu akawajibu, akasema: Mafundisho yangu siyo yangu, ni yake yeye aliyenituma.
17
Mtu akitaka kuyafanya mapenzi yake yeye, atayatambua mafundisho haya, kama yametoka kwake yeye Mungu, au kama nayasema maneno yangu.
18
Mwenye kuyasema yake hutafuta, atukuzwe yeye mwenyewe; lakini mwenye kutafuta, aliyemtuma atukuzwe, huyo ni mtu wa kweli, upotovu wo wote haumo moyoni mwake.
19
Siye Mose aliyewapa Maonyo? Tena kwenu hakuna mtu anayeyafanya Maonyo. Mnatafutiani kuniua?
20
Watu wakajibu: Una pepo! Yuko nani anayetaka kukuua?
21
Yesu akajibu, akawaambia: Ni tendo moja tu, nililolifanya, nanyi nyote mkalistaajabu.
22
Kwa sababu hiyo Mose aliwaagiza kutahiri watu; tena siye Mose aliyeviagiza, ila baba zenu. Nanyi humtahiri mtu hata siku ya mapumziko.
23
Mtu akitahiriwa siku ya mapumziko, kwamba Maonyo ya Mose yasivunjwe, mbona mnanikasirikia mimi, kwa sababu nimeponya mwili wote wa mtu siku ya mapumziko?
24
Msiumbue kwa hivyo tu, mnavyoviona, ila umbueni maumbufu yapasayo!
25
Palikuwa na wenyeji wa Yerusalemu waliosema: Si huyu, wanayemtafuta kumwua?
26
Tazameni, anasema waziwazi, wasimjibu neno! Labda nao wakubwa wetu wametambua kweli, ya kuwa huyu ni Kristo?
27
Lakini huyu tunamjua, anakotoka; lakini Kristo atakapokuja, hakuna atakayetambua, atokako.
28
Ndipo, Yesu alipopaza sauti hapo alipofundishia Patakatifu, akasema: Mimi mnanijua, tena mnakujua, nilikotoka. Lakini sikujileta mwenyewe tu, ila yuko mwenye kweli aliyenituma, msiyemjua ninyi.
29
Mimi ninamjua, kwani nimetoka kwake, naye amenituma.
30
Walipojaribu kumkamata, hata mmoja hakumnyoshea mkono, kwani saa yake ilikuwa haijafika.
31
Lakini wengi waliokuwamo kundini mwa watu wakamtegemea, wakasema: Kristo atakapokuja atafanya vielekezo vingi kuliko hivyo, alivyovifanya huyu?
32
Mafariseo waliposikia, watu wakinong'onezana hayo mambo yake, ndipo, watambikaji wakuu na Mafariseo walipotuma watumishi, wamkamate.
33
*Yesu akasema: Nipo pamoja nanyi bado kidogo; kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma.
34
Mtanitafuta, msinione; napo hapo, nitakapokuwapo, ninyi hamwezi kupafika.
35
Ndipo, Wayuda waliposema wao kwa wao: Huyu anataka kwenda wapi, sisi tusimwone? Atawaendea wale waliotawanyika kwa Wagriki, awafundishe Wagriki?
36
Ni neno gani hilo, alilolisema: Mtanitafuta, msinione? Napo hapo, nitakapokuwapo, ninyi hamwezi kupafika?
37
Siku ya mwisho iliyokuwa kubwa katika sikukuu Yesu alikuwa amesimama, akapaza sauti akisema: Mtu akiwa na kiu na aje kwangu, anywe!
38
Mwenye kunitegemea, kama yalivyoandikwa, mwilini mwake yeye mtatoka mito ya maji yenye uzima.
39
Hivyo alisema kwa ajili ya Roho, watakayepewa waliomtegemea; kwani Roho alikuwa hajaonekana bado, kwa sababu Yesu alikuwa hajaupata utukufu wake.*
40
Wengine waliokuwamo kundini mwa watu walipoyasikia maneno hayo wakasema: Huyu ndiye kweli yule mfumbuaji.
41
Wengine wakasema: Huyu ndiye Kristo, wengine wakasema: Je? Kristo atatoka Galilea?
42
Je? Andiko halikusema: Kristo atatoka katika uzao wa Dawidi mle kijijini mwa Beti-Lehemu, alimokaa Dawidi?
43
Basi, watu wakakosana kwa ajili yake.
44
Wenzao wengine walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyemnyoshea mikono.
45
Kisha wale watumishi wakarudi kwa watambikaji wakuu na kwa Mafariseo; nao walipowauliza: Mbona hamkumleta?
46
watumishi wakajibu: Tangu kale mtu hajasema hivyo kama mtu huyo anavyosema.
47
Mafariseo wakawajibu: Nanyi mmepotezwa?
48
Je? Yuko mkubwa au Fariseo anayemtegemea?
49
Ni hili kundi la watu tu wasioyatambua Maonyo, ndio walioapizwa.
50
Ndipo, Nikodemo aliyemjia siku zile usiku, aliyekuwa mmoja wao, alipowaambia:
51
Maonyo yetu huhukumu mtu, asiposikiwa kwanza, yatambulikane aliyoyatenda?
52
Wakajibu, wakamwambia: Je? Nawe u mtu wa Galilea? Tafuta, uone, ya kuwa hakuna mfumbuaji anayetoka huko Galilea!
53
Wakaenda zao kila mmoja nyumbani kwake.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21