bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 11
John 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 12 →
1
*Kulikuwa na mtu mgonjwa, ndiye Lazaro wa Betania, ni kijiji chao Maria na ndugu yake Marta;
2
Maria ndiye yule aliyempaka Bwana mafuta na kuisugua miguu yake kwa nywele zake. Huyo umbu lake Lazaro alikuwa mgonjwa.
3
Dada zake wakatuma kwake kwamba: Bwana, tazama, unayempenda ni mgonjwa!
4
Yesu alipovisikia akasema: Ugonjwa huu sio wa kufa, ni wa kuuonyesha utukufu wake Mungu, Mwana wa Mungu apate kutukuzwa nao.
5
Lakini Yesu alikuwa amewapenda akina Marta na ndugu yake na Lazaro.
6
Aliposikia, ya kuwa ni mgonjwa, akakaa siku mbili hapo, alipokuwapo.
7
Kisha ndipo, alipowaambia wanafunzi: Twende Yudea tena!
8
Wanafunzi walipomwambia: Mfunzi mkuu, sasa hivi Wayuda walitafuta kukupiga mawe, nawe unarudi huko tena?
9
Yesu akajibu: Saa za mchana sizo kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai, kwani huuona mwanga wa ulimwengu huu;
10
lakini mtu akienda usiku hujikwaa, kwani mwanga haumo mwake.
11
Alipokwisha kusema hivyo akawaambia: Mpenzi wetu Lazaro amelala, lakini nakwenda, nimwamshe.*
12
Wanafunzi wakamwambia: Bwana, akiwa amelala atapona.
13
Lakini Yesu alikuwa amesema kufa kwake, lakini wale walidhani: alisema kulala usingizi.
14
Ndipo, Yesu alipowaambia waziwazi: Lazaro amekufa.
15
Nami nafurahi kwa ajili yenu, ya kuwa sikuwako kule, mpate kunitegemea. Lakini twende, tufike kwake!
16
Toma anayeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenziwe: Twende nasi, tufe pamoja naye!
17
Yesu alipokuja akamkuta, amekwisha kuwa kaburini siku nne.
18
Lakini kule Betania kulikuwa karibu ya Yerusalemu, ni mwendo wa nusu saa;
19
kwa hiyo Wayuda wengi walikuwa wamekuja kwao Marta na Maria, wawatulize mioyo kwa ajili ya umbu lao.
20
*Marta aliposikia, ya kuwa Yesu anakuja, akaenda kumkuta njiani; lakini Maria alikuwa akikaa nyumbani.
21
Marta akamwambia Yesu: Bwana, kama ungalikuwapo hapa, umbu langu hangalikufa.
22
Lakini na sasa najua, ya kuwa yote, utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.
23
Yesu alipomwambia: Umbu lako atafufuka,
24
Marta akamwambia: Najua, ya kuwa atafufuka, wafu watakapofufuka siku ya mwisho.
25
Yesu akamwambia: Mimi ndio ufufuko na uzima; anitegemeaye atapata uzima, ajapokufa.
26
Kila aliye mzima na kunitegemea hatakufa kale na kale. Unavitegemea hivi?
27
Akamwambia: Ndio, Bwana, mimi nimeyategemea, ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, anayekuja ulimwenguni.*
28
Alipokwisha kusema hivyo akaondoka, akamwita ndugu yake Maria na kufichaficha, akasema: Mfunzi yuko, anakwita.
29
Naye alipovisikia akainuka upesi, akamwendea;
30
maana Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado hapo, Marta alipomkuta.
31
Wayuda waliokuwa pamoja naye nyumbani na kumtuliza moyo walipomwona Maria, alivyoinuka upesi na kutoka, wakamfuata wakiwaza, ya kuwa anajiendea kaburini, alie huko.
32
Maria alipofika hapo, Yesu alipokuwa, akamwangukia miguuni alipokwisha kumwona, akamwambia: Bwana, kama ungalikuwapo hapa, umbu langu hangalikufa.
33
Yesu alipoona, anavyolia, nao Wayuda waliokuja pamoja naye wanavyolia nao, akachemka rohoni, akajisisimua,
34
akauliza: Mmemzika wapi? Wakamwambia: Njoo, Bwana, utazame!
35
Naye Yesu machozi yakamtoka.
36
Ndipo, Wayuda waliposema: Tazameni, alivyompenda!
37
Lakini wengine wao wakasema: Huyu aliyemfumbua kipofu macho hakuweza kuzuia, huyu naye asife?
38
Yesu akachemka tena moyoni, akafika penye kaburi; hilo lilikuwa pango lenye jiwe lililowekwa mlangoni pake.
39
Yesu aliposema: Liondoeni hili jiwe! Marta, dada yake aliyekufa, akamwambia: Bwana, ameanza kunuka, kwani leo ni siku ya nne.
40
Yesu akamwambia: Sikukuambia: Ukinitegemea utauona utukufu wake Mungu?
41
Basi, wakaliondoa jiwe. Kisha Yesu akayaelekeza macho juu, akasema: Baba, nakushukuru, ya kuwa umenisikia.
42
Mimi nimekujua, ya kuwa unanisikia po pote; lakini kwa ajili ya kundi la watu wanaosimama hapa ninasema hivyo, wapate kuyategemea, ya kuwa wewe umenituma.
43
Alipokwisha kuyasema haya akaita na kupaza sauti: Lazaro, toka nje!
44
Ndipo, yule aliyekufa alipotoka nje hivyo, alivyokuwa amefungwa kwa sanda miguu na mikono, nao uso wake ulikuwa umefunikwa kwa mharuma. Yesu akawaambia: Mfungueni, mmwache, aende zake!
45
Wayuda wengi waliomjia Maria walipoliona, alilolifanya, wakamtegemea,
46
lakini wengine wao wakaenda zao kwa Mafariseo, wakawaambia, Yesu aliyoyafanya.
47
*Ndipo, watambikaji wakuu na Mafariseo walipoikusanya baraza ya wakuu wote, wakasema: Tufanyeje? Kwani mtu huyu anafanya vielekezo vingi.
48
Tukimwacha hivyo, wote watamtegemea, kisha Waroma watakuja, waichukue nchi yetu pamoja na watu wetu.
49
Lakini mwenzao Kayafa aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule akawaambia: Ninyi hamjui kitu,
50
wala hamfikiri, ya kuwa inawafalia ninyi, mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kabila lote lisiangamie.
51
Lakini neno hili hakulisema kwa mawazo yake, ila kwa kuwa alikuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule, alifumbua yajayo, kwani Yesu alitumwa afe kwa ajili ya kabila lote;
52
lakini siko kufa kwa ajili ya kabila lake tu, ila ni kwamba, apate kuwakusanya pamoja nao watoto wa Mungu waliotawanyika.
53
Basi, tangu siku ile walikula njama ya kumwua.
54
Naye Yesu hakutembea tena waziwazi kwa Wayuda, ila akaondoka kule, akaenda katika nchi iliyokuwa karibu ya nyikani, akaingia mji uitwao Efuraimu. Mle akakaa pamoja na wanafunzi.
55
Lakini Pasaka ya Wayuda ilikuwa karibu; kwa hiyo wengi wa nchi ile wakapanda kwenda Yerusalemu, Pasaka ilipokuwa bado, wapate kujieua.
56
Kwa kumtafuta Yesu wakasemezana wao kwa wao wakisimama hapo Patakatifu: Mwaonaje? Hatakuja sikukuu hii?
57
Lakini watambikaji wakuu na Mafariseo walikuwa wameagiza, mtu akitambua, alipo, sharti aseme, wapate kumkamata.*
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21