bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 2
John 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 3 →
1
*Siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya arusi huko Kana wa Galilea, hata mamake Yesu alikuwako,
2
naye Yesu na wanafunzi wake wakaalikwa arusini.
3
Mvinyo ilipopunguka, mamake Yesu akamwambia: Hawana mvinyo.
4
Yesu akamwambia: Mama, tuko na jambo gani, mimi na wewe? Saa yangu haijaja bado.
5
Ndipo, mama yake alipowaambia watumishi: Lo lote atakalowaambia, lifanyeni!
6
Pale palikuwa na mitungi sita ya mawe iliyokuwa imewekwa kwa desturi ya kunawa kwao Wayuda; kila mmoja ulienea mabuyu mawili au matatu.
7
Yesu akawaambia: Ijazeni mitungi maji! Walipokwisha kuijaza mpaka juu,
8
akawaambia: Sasa tekeni, mmpelekee mwandaliaji! Basi, wakampelekea.
9
Lakini mwandaliaji hakujua, ilikotoka, watumishi tu waliokuwa wameyateka yale maji walijua. Mwandaliaji alipoyaonja yale maji yaliyogeuka kuwa mvinyo akamwita bwana arusi,
10
akamwambia: Kila mtu hutoa kwanza mvinyo nzuri; watu wakiisha kushiba, huileta isiyo nzuri sana; lakini wewe iliyo nzuri umeiweka mpaka sasa.
11
Huo ndio mwanzo wa vielekezo, Yesu alivyovifanya, nao ulifanyika Kana wa Galilea; ndivyo, alivyoufunua utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamtegemea.*
12
Kisha wakashuka kwenda Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake, wakakaa huko siku zisizokuwa nyingi.
13
*Pasaka ya Wayuda ilipokuwa karibu, Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.
14
Alipoona hapo Patakatifu wenye kuuzia palepale ng'ombe na kondoo na njiwa, hata wavunjaji wa fedha waliokuwapo wamekaa,
15
akaokota kamba, akazisuka kambaa, akawafukuza wote hapo Patakatufu, hata kondoo na ng'ombe, akazimwaga fedha za wavunjaji na kuziangusha meza zao.
16
Wenye kuuza njiwa akawaambia: Yaondoeni haya hapa! Msiigeuze Nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya uchuuzi!
17
Hapo wanafunzi wake wakakumbuka, ya kuwa imeandikwa:
18
Kwa ajili ya Nyumba yako wivu unanila!* Wayuda walipomwuliza wakimwambia: Unatuonyesha kielekezo gani, kwa kuwa unafanya hivyo?
19
Yesu akajibu akiwaambia: Livunjeni Jumba hili la Mungu! Nami nitalijenga tena muda wa siku tatu.
20
Wayuda wakasema: Jumba hili la Mungu lilijengwa kwa miaka 46, nawe utalijenga kwa siku tatu?
21
Lakini yeye alilisema Jumba la Mungu lililo mwili wake.
22
Hapo, alipokwisha kufufuliwa katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka, ya kuwa aliyasema hayo. Wakayategemea Maandiko na neno hilo, Yesu alilolisema.
23
Lakini alipokuwako Yerusalemu siku za sikukuu ya Pasaka, wengi wakaja kulitegemea Jina lake walipoviona vielekezo vyake, alivyovifanya.
24
Lakini Yesu mwenyewe hakuwategemea, kwamba wanamtegemea, kwani yeye aliwatambua wote;
25
kwa hiyo hakutaka kushuhudiwa na mwingine mambo ya mtu, maana aliyatambua mwenyewe yaliyomo moyoni mwa mtu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21