bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 4
John 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 5 →
1
Ilikuwa hapo, Bwana akitambua, ya kama Mafariseo wamesikia, ya kuwa Yesu anapata wanafunzi wengi, tena ya kuwa anabatiza kumpita Yohana,
2
ijapo Yesu mwenyewe hakubatiza mtu, ni wanafunzi wake tu.
3
Ndipo, alipoondoka Yudea, akaenda kufika tena Galilea,
4
lakini hakuwa na budi kushika njia ya kupita katikati ya Samaria.
5
*Akafika penye mji wa Samaria, jina lake Sikari, ulio karibu ya kiunga, Yakobo alichompa mwanawe Yosefu;
6
hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Kwa hivyo, Yesu alivyokuwa amechoka kwa mwendo, akakaa pale kisimani; ilikuwa kama saa sita.
7
Alipokuja mwanamke Msamaria kuchota maji, Yesu akamwambia: Nipe, ninywe!
8
kwani wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.
9
Ndipo, yule mwanamke Msamaria alipomwambia: Wewe uliye Myuda waniombaje ya kunywa mimi niliye mwanamke wa Kisamaria? Kwani Wayuda na Wasamaria huziana.
10
Yesu akajibu, akamwambia: Kama ungekijua kipaji cha Mungu, tena kama ungemjua anayekuambia: Nipe, ninywe! wewe ungemwomba, naye angekupa maji yenye uzima.
11
Akamwambia: Bwana, hunacho cha kutekea, nacho kisima ni kirefu, basi, utayapata wapi hayo maji yenye uzima?
12
Je? Wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki? Naye alikunywa humu mwenyewe na watoto wake na nyama wake wa kufuga.
13
Yesu akajibu, akamwambia: Kila anayeyanywa maji haya ataona kiu tena;
14
lakini atakayeyanywa maji, nitakayompa mimi, hataona kiu kale na kale. Ila maji yale, nitakayompa, yatakuwa mwilini mwake chemchemi ya maji yabubujikayo, yamfikishe penye uzima wa kale na kale.*
15
Yule mwanamke alipomwambia: Bwana, nipe maji hayo, nisipate kuona kiu tena, wala nisije hapa tena kuchota!
16
akamwambia: Nenda, umwite mumeo! Kisha urudi hapa!
17
Yule mwanamke alipojibu na kusema: Sina mume, Yesu akamwambia: Umesema kweli: Sina mume.
18
Kwani waume watano ulikuwa nao, naye uliye naye sasa, siye mume wako; hili umesema kweli.
19
Ndipo, yule mwanamke alipomwambia: Bwana, nakuona, ya kuwa wewe u mfumbuaji.
20
Baba zetu walitambikia mlimani huku, nanyi husema: Yerusalemu ndipo, panapopasa kupatambikia.
21
*Yesu akamwambia: Nitegemea mama, ya kuwa saa inakuja, itakapokuwa, msimtambikie Baba wala huku mlimani wala Yerusalemu!
22
Ninyi hutambikia, msichokijua; sisi hutambikia, tunachokijua, kwani wokovu umeanzia kwa Wayuda.
23
Lakini saa inakuja, tena sasa iko, wenye kutambika kweli watakapomtambikia Baba kiroho na kikweli, kwani naye Baba huwataka wanaomtambikia hivyo.
24
Mungu ni Roho, nao wanaomtambikia imewapasa kumtambikia kiroho na kikweli.*
25
Ndipo, yule mwanamke alipomwambia: Najua, ya kuwa Masiya anakuja anayeitwa Kristo; yeye atakapokuja atatufunulia yote.
26
Yesu akamwambia: Mimi ndiye ninayesema nawe.
27
Hapo wanafunzi wake wakaja, wakashangaa, ya kuwa anasema na mwanamke; lakini hakuna aliyeuliza: Watafuta nini? au: Wasemaje naye?
28
Lakini yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda mjini, akawaambia watu:
29
Njoni, mtazame mtu aliyeniambia yote, niliyoyafanya, kama yeye siye Kristo!
30
Ndipo, walipotoka mjini, wakamwendea.
31
*Walipokuwa hawajafika, wanafunzi wakamhimiza wakisema: Mfunzi mkuu, ule!
32
Alipowaambia: Mimi ninacho chakula, msichokijua ninyi,
33
wanafunzi wakasemezana: Yuko mtu aliyemletea chakula?
34
Yesu akawaambia: Chakula changu ni kuyafanya, ayatakayo yeye aliyenituma, niimalize kazi yake.
35
Ninyi hamsemi: Iko miezi minne bado, mavuno yatakapokuwapo? Tazameni, nawaambiani: Yainueni macho yenu, myatazame mashamba! Yamekwisha kuwa meupe, yavunwe.
36
Mvunaji hupokea mshahara, akakusanya vyakula, vimfikishe penye uzima wa kale na kale; hivyo mwishoni mpanzi hufurahi pamoja na mvunaji.
37
Kwani hapo lile fumbo ni la kweli: Mwingine hupanda, mwingine huvuna.
38
Mimi naliwatuma, mvune, msiyoyafanyia kazi; wengine wamefanya kazi, ninyi mkaingia kazini mwao.
39
Kisha Wasamaria wengi wa mji ule wakamtegemea kwa ajili ya neno, yule mwanamke alilomshuhudia kwamba: Ameniambia yote, niliyoyafanya.
40
Kwa hiyo Wasamaria walipomjia wakamtaka, akae kwao. Akakaa huko siku mbili.
41
Kisha waliomtegemea kwa ajili ya neno lake mwenyewe wakawa wengi sana,
42
wakamwambia yule mwanamke: Hatumtegemei tena kwa vile, ulivyotuambia, kwani wenyewe tumemsikia, tukamjua: Ni kweli, huyu ndiye mwokozi wa ulimwengu.*
43
Siku mbili zilipopita, akatoka huko kwenda Galilea.
44
Kwani Yesu mwenyewe alishuhudia, ya kuwa mfumbuaji haheshimiwi kwao, mwenyewe alikokulia.
45
Alipofika Galilea, Wagalilea wakampokea, kwani walikuwa wameyaona yote, aliyoyatenda Yerusalemu siku za sikukuu; kwani nao walikuwa wamekwenda kule siku za sikukuu.
46
Akafika tena Kana wa Galilea, alikogeuza maji kuwa mvinyo. *Kulikuwa na mtu wa kifalme aliyeuguliwa na mwana wake huko Kapernaumu.
47
Huyo aliposikia, ya kuwa Yesu ametoka Yudea, akafika Galilea, akaondoka, akamwendea, akambembeleza, ashuke, amponye mwanawe, kwani alitaka kufa.
48
Lakini Yesu akamwambia: Msipoona vielekezo na vioja hamnitegemei.
49
Yule mtu wa kifalme alipomwambia: Bwana, shuka, mtoto wangu asije kufa!
50
Yesu akamwambia: Jiendee, mwana wako yuko mzima! Yule mtu akalitegemea neno, Yesu alilomwambia, akaenda zake.
51
Angali akishuka, watumwa wake wakaja kukutana naye wakisema: Mtoto wako yuko mzima!
52
Akawauliza saa, alipoanzia kuwa hajambo kidogo. Walipomwambia: Jana saa saba joto limemtoka,
53
baba akatambua, ya kuwa ni saa ileile, Yesu alipomwambia: Mwana wako yuko mzima. Ndipo, yeye nao waliokuwamo mwake walipomtegemea wote.
54
Hiki ndicho kielekezo cha pili, Yesu alichokifanya alipotoka Yudea kwenda Galilea.*
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21