bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 21
John 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
1
Kisha Yesu akajijulisha tena kwa wanafunzi kwenye bahari ya Tiberia. Alivyojijulisha ni hivyo:
2
walikuwako pamoja Simoni Petero na Toma anayeitwa Pacha na Natanaeli wa Kana wa Galilea na wana wa Zebedeo na wanafunzi wake wengine wawili.
3
Simoni Petero alipowaambia: Nakwenda kuvua, wakamwambia: Nasi tunakwenda pamoja na wewe. Basi, wakaondoka, wakaingia chomboni, lakini usiku ule hawakupata kitu.
4
Kulipoanza kucha, Yesu alikuwa amesimama ufukoni, lakini wanafunzi hawakumjua, ya kuwa ndiye Yesu.
5
Yesu alipowauliza: Wanangu, hamna kitoweo? wakamjibu: Hatuna.
6
Ndipo, alipowaambia: Utupeni wavu kuumeni kwa chombo, ndiko, mtakakopata! Walipoutupa, tena hawakuweza kuuvuta kwa ajili ya samaki wengi.
7
Ndipo, yule mwanafunzi, Yesu aliyempenda, alipomwambia Petero: Ni Bwana! Simoni Petero aliposikia, ya kuwa ni Bwana, akajifunga vazi, kwani alikuwa uchi, akajitupa baharini.
8
Wanafunzi wenziwe wakaenda kwa chombo wakiuvuta wavu uliojaa samaki, kwani pwani hapakuwapo mbali, palikuwa kama mikono 200 tu.
9
Nao waliposhuka pwani wakaona: moto wa makaa ulikuwa umewashwa, navyo visamaki vilikuwa vimewekwa juu pamoja na mkate.
10
Yesu akawaambia: Leteni kidogo katika visamaki hivyo, mlivyovivua sasa hivi!
11
Simoni Petero akapanda chomboni, akauvuta wavu ufukoni; wakawamo samaki wakubwa tu 153. Nao wavu haukupasuka, wangawa wengi kama hao.
12
Kisha Yesu akawaambia: Njoni, mle! Miongoni mwao hao wanafunzi hakuwamo hata mmoja aliyejipa moyo wa kumwuliza: Wewe u nani? Walimjua, ya kuwa ndiye Bwana.
13
Kisha Yesu akaenda, akautwaa mkate, akawagawia, na kitoweo vilevile.
14
Hii ndiyo mara ya tatu, Yesu akijijulisha kwa wanafunzi alipokwisha fufuka katika wafu.
15
*Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petero: Simoni wa Yohana, wanipenda kuliko hawa? Akamwambia: Ndio, Bwana, wewe unajua, ya kuwa ninakupenda. Akamwambia: Walishe wana kondoo wangu!
16
Alipomwuliza tena mara ya pili: Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia: Ndio, Bwana, wewe unajua, ya kuwa ninakupenda. Akamwambia: Vichunge vikondoo vyangu!
17
Alipomwuliza mara ya tatu: Simoni wa Yohana, Wanipenda? Petero akasikitika, kwa sababu alimwuliza mara ya tatu: Wanipenda? akamwambia: Bwana, wewe unayajua yote, wewe unatambua, ya kuwa ninakupenda. Yesu akamwambia: Vilishe vikondoo vyangu!
18
Kweli kweli nakuambia: Ulipokuwa kijana ulijifunga mwenyewe, ukaenda, ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utainyosha mikono yako, mwingine akuvike, akupeleke, usikotaka.
19
Neno hili alilisema, amwonyeshe kufa, alikotakiwa, amtukuze Mungu nako. Alipokwisha kuyasema haya akamwambia; Nifuate!*
20
Petero alipogeuka akaona, anafuata naye yule mwanafunzi, Yesu aliyempenda, ni yule aliyekuwa ameegamia kifuani pake, walipokuwa wakila jioni, aliyemwuliza: Bwana, ni nani, atakayekuchongea?
21
Basi, Petero alipomwona huyu akamwuliza Yesu: Bwana, na huyu je?
22
Yesu akamwambia: Nikitaka, huyu akae, mpaka nitakapokuja, wewe unavikataliaje? Wewe nifuate tu!
23
Basi, neno hili likaenea katika ndugu la kwamba: Mwanafunzi huyu hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia: Hatakufa, ila: Nikitaka, huyu akae, mpaka nitakapokuja, wewe unavikataliaje?
24
Huyu ndiye mwanafunzi aliyeyashuhudia haya na kuyaandika. Nasi twamjua, ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.
25
Lakini yako hata mengine mengi, Yesu aliyoyafanya. Nayo kama yangaliandikwa moja moja, nadhani, ulimwengu wote usingevitoshea vitabu vitakavyoandikwa.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21